A
Anonymous
Guest
Kuna jambo ambalo sijalielewa kuhusu uendeshaji wa treni ya mwendokasi (SGR) kati ya Dar es Salaam na Morogoro.
Kwa kawaida, safari hii hutumia treni yenye behewa 14 (ordinary). Hata hivyo, kumekuwa na nyakati ambapo treni ya mchongoko yenye behewa 16 imekuwa ikitumika kwenye route hii. Sina uhakika imefanya safari hizo mara ngapi, lakini binafsi tayari nimeisafiria mara mbili.
Kinachonishangaza zaidi ni kwamba, kwenye mfumo wa ukataji tiketi bado huonekana treni ya ordinary, ambayo mara nyingi hujaa mapema. Hivyo najiuliza, ikiwa treni hiyo imepata hitilafu au haiwezi kutoa huduma kwa siku husika, kwa nini taarifa hiyo isitolewe mapema na mfumo wa ukataji tiketi usisasishwe ili abiria wapate nafasi ya kukata tiketi na kusafiri?
Kwa hali ilivyo sasa, unakuta treni ya mchongoko inafanya safari ikiwa na idadi ndogo ya abiria, jambo ambalo linaweza kulisababishia shirika kupoteza mapato ambayo yangeweza kupatikana kama mfumo ungeboreshwa na taarifa kutolewa kwa wakati.
Naomba mamlaka husika zitoe ufafanuzi kuhusu utaratibu huu ili wananchi na watumiaji wa huduma ya SGR waelewe sababu ya hali hiyo.