SeliSelina
JF-Expert Member
- Jun 27, 2014
- 419
- 902
Mpaka hii leo nashindwa kufanya shughuli zangu, nashindwa kula vizuri, nashindwa karibu kufanya mambo yote kwa sababu ya mambo yanayoendelea katika nchi yangu Tanzania.
Nina maumivu makubwa mno moyoni mwangu kiasi kwamba upande wa kushoto wa moyo wangu haupo vizuri.
Najikuta nashinda mitandaoni muda mwingi kwa sababu ya kusoma kinachoendelea.
Yaliyofanyika kuanzia mchakato wa kura mpaka kumalizika kwa maandamano ni mtihani mkubwa kwa taifa letu tukijumuisha Zanzibar na Tanganyika (Tanzania).
Nilichokiona katika siku hizi kumi zaidi ni mambo mazito na yaliyojaa huzuni.
Nitaanza kuzungumzia kuhusu ubaguzi ulioanza kushika kasi kipindi hiki.
Jamani ndugu zangu Watanzania,
Tanzania Bara na Tanzania Visiwani ni watu waliochanganya damu sana kuliko inavyodhaniwa mtandaoni wamezaliana sana.
Tukisema kuwa Wazanzibari wanatubagua, Mzanzibari ni nani?
Mzanzibari ni Mtanzania. Hakuna pasi ya kusafiria ya Mzanzibari, bali kuna pasi ya Mtanzania.
Watanganyika wapo Zanzibar na Wazanzibari wapo Tanganyika.
Mfano:
Tukianza na Rais wa Zanzibar, Hussein Ali Hassan Mwinyi baba yake, Mzee Mwinyi, na mama yake wote wametokea Bara (kwa ushahidi wa Wikipedia).
Mke wa Rais wa Zanzibar, Maryam Harman, kizazi chake chote kinatokea Bara.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, George J. Kazi.
Tukisema Wazanzibari waende kwao na wa Bara warudi Bara kwa hiyo Mwinyi na mkewe, pamoja na George Kazi, wanaenda wapi?
Mimi binafsi, wazee wangu, mama na wajomba wote wameoana kati ya Zanzibar na Bara.
Ndugu zangu wa kuzaliwa wameolewa na kuoa huko na huku.
Kwa hiyo tusibaguane kikanda, kikabila, au kidini haya mambo yananivunja moyo sana.
Kama Jeshi la KMKM limekuja Bara kuua, maana yake ni kwamba aliyepeleka ni Mwinyi, ambaye asili yake ni Bara kama mkewe. Kwa nini alifanya hivyo kwenda kuangamiza kizazi kiasi hicho?
Kwa maana hiyo, tukisema Wazanzibari wametuua, aliyeongoza maamuzi ya mauaji hayo ni Rais wa Zanzibar, Mwinyi, kwa kupeleka jeshi Bara kuwaangamiza wa Bara.
Tusibaguane kikanda, kikabila, au kidini.
Tuangalie namna ya kuiondoa CCM madarakani hilo ndilo jambo la msingi la kuzingatia.
Kuhusu hoja ya serikali tatu jambo lililokuwa likipigiwa debe sana na Wazanzibari, likiwemo kundi la Uamsho, lakini walionekana magaidi na wakawekwa ndani miaka karibu tisa yote ni kwa sababu ya kuzungumzia serikali tatu.
Tukijikita kwenye ubaguzi, hatuwezi kufikia lengo letu hata siku moja la kuiondoa CCM madarakani.
Ubaguzi unazalisha chuki, na ukikosa wa kumbagua, utambagua mkeo, mumeo au mwanao.
Tuwe na subira kwa msiba uliotupata tumepoteza ndugu na mali zetu.
Tafakari ni nini cha kufanya. Tusichukuliwe na visasi; havitotufikisha popote, tutazidi kudidimia.
Tuseme wazi CCM imefanya mauaji makubwa, bila kuangalia nani ni nani: Samia, Mafwele, Mkunda, Polisi, au Jeshi. Kwa pamoja ndipo tutakapofikia lengo.
Tusilenge familia za polisi au mtu mmoja mmoja, tukitaka kulipiza kisasi. Hivyo hatutafika.
Tushikamane, tudai haki yetu kwa njia za salama na amani si kwa kuvunja au kuchoma moto, kwani tutazidi kuuliwa.
Naomba radhi sana kama kuna mtu atakuwa nimekwaza kwa posti yangu hii.
Naomba tupunguze matusi hayatusaidii kitu.