Kwanini tukio hili la kuvunjwa miguu halipo katika injili ya Marko, Mathayo wala Luka? Yohana kajichanganya kwenye simlizi

Covax

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2021
Posts
13,682
Reaction score
41,162
(Yohana 19:31-33)
Kwa kuwa ilikuwa siku ya maandalizi, Wayahudi hawakutaka miili ibaki msalabani siku ya Sabato, hasa kwa sababu Sabato hiyo ilikuwa siku kuu ya ibada. Hivyo waliomba kwa Pilato miguu ya wale waliokuwa wamesulubiwa ivunjwe na miili iondolewe. Kisha askari wakavunja miguu ya wa kwanza na wa pili waliokuwa wamesulubiwa pamoja naye. Lakini walipomjia Yesu wakaona kuwa tayari alikuwa amekufa, hawakuvunja miguu yake.

Kumbuka Yohana aliandika awali:
"Hapo wakamsulubisha yeye, na pamoja naye wengine wawili, mmoja upande huu na mwingine upande huu, Yesu katikati yao." (Yohana 19:18)

Swali: Kama Yesu alikuwa kati ya hao wawili, kwa nini askari walianza kuvunja miguu ya wa kwanza, wakamruka Yesu, wakamfuata wa pili, kisha warudi kwa Yesu? Je, Yohana alikuwa na “uchovu wa kuhariri” (redaction fatigue)?

Swali la pili Na kwa nini tukio hili la kuvunjwa miguu halipo katika Marko, Mathayo wala Luka? Kama kweli limetokea na si hi hadeeth ya kutunga?
 
Swali hili linahoji usahihi wa mpangilio wa simulizi ya Yohana. Kama Yesu alikuwa katikati, haieleweki kwa nini askari wangeanza na mmoja wa pembeni, wamruke Yesu, wamfuate wa pili, kisha ndio waje kwa Yesu.

Kwa kulinganisha na Injili nyingine (Marko, Mathayo, Luka), tukio la kuvunjwa miguu halijatajwa kabisa. Hili linaonyesha tofauti za kisimulizi ambazo huenda zinatokana na malengo tofauti ya waandishi wa Injili, au uandishi wa marejeo ya baadaye uliojaribu kutimiza unabii wa “mfupa wake haitavunjika” (Yohana 19:36).

Hii ni hoja halali ya kuonyesha kuwa si kila simulizi kwenye Injili ni uthibitisho wa tukio la kihistoria, bali mara nyingine ni juhudi ya kiteolojia au uhariri wa baadaye, sio ufunuo wa roho mtukufu kama wa kuristo wengi wanavo dai.
 
Siwezi kuheshimu wala kumuamini mtu anaekataa kula nguruwe lakini anaenda kuoa katoto kenye miaka 12 na kujipatia uhalali wa kuua ili akapate mademu 72 siku akifariki.
9b056ed4a81d104d74a110c49140d4fc~2.jpg

----JASUSI COHEN
 
Siwezi kuheshimu wala kumuamini mtu anaekataa kula nguruwe lakini anaenda kuoa katoto kenye miaka 12 na kujipatia uhalali wa kuua ili akapate mademu 72 siku akifariki.

----JASUSI COHEN
Mkuu acha ugomvi rudi kwenye Mada unataka kupingana na maandiko ya biblia, chuki Zako dhidi ya Imani za wengine wake pambeni hapa tuko kiacademic Zaidi, mihemko peleka kwenye vita ya Iran na Israel.
 
Mbona kwenye Uislamu kitimoto ni haram ila kuua n halal?
 
Tunapo waambia biblia sio neno la roho mtakatifu mnabisaha sasa angalia mkanganyiko kama huo wa mpangilio wa Yohana ni dhahili kwamba ni wa kutunga tu.
 
Hata kuran pia
 
Mkuu katika tukio la kusulibiwa Yesu Kristo mhusika mkuu alikuwa ni Yesu, Ilikwisha kujulikana kwamba Yesu hakuwa mtu wa kawaida. Waliomsulibisha walijua huyu Mtu ni wa kipekee.

Yesu aliwekwa katikati ya waovu kuonesha dharau na dhihaka dhidi yake. Lakini pia tukio hilo lilikuwa na maana kubwa sana kiroho. Tukio la Bwana Yesu Kristo kuwekwa katikati ya waovu liliashiria utawala wa Nuru katikati ya uovu.

Yesu alikata Roho mapema kuliko wale wawili aliosulibishwa pamoja nao hivyo hakukuwa na ulazima wa kumvunja miguu.

Vitabu na maandiko ya injili ya Luka, Mathayo na Yohana vinalenga kuzungumzia ujumbe Mkuu mmoja, ingawa baadhi ya taarifa ndogondogo zinaweza kuachwa au kuandikwa kutokana na kusudio kuu la Mwandishi. Jambo kuu ni kufikisha ujumbe uliokusudiwa.

Ndiyo maana Biblia inavipa nafasi sawa vitabu vyote vya injili ambavyo aghalabu huzungumzia hoja mfanano ili kumpa msomaji taarifa sahihi na kukoleza uzito wa jumbe zilizomo.
 
Hoja hiyo haijitoshelezi kimaandiko wala kihistoria. Kwanza, tukikubali kuwa Yesu alikuwa wa kipekee na wa kiroho sana, hilo halielezi kwa nini masimulizi ya tukio hilo muhimu kama kusulubiwa kwake yanatofautiana katika Injili tofauti.
Kwa mfano:
1. Mathayo 27:44 na Marko 15:32* wanasema kuwa wale wezi wawili walimtukana Yesu wote wawili
2. Lakini Luka 23:39-43 anasema kuwa mmoja alimkashifu Yesu na mwingine akatubu na kuahidiwa paradiso.
 
Mkuu katika tukio la kusulibiwa Yesu Kristo mhusika mkuu alikuwa ni Yesu, Ilikwisha kujulikana kwamba Yesu hakuwa mtu wa kawaida. Waliomsulibisha walijua huyu Mtu ni wa kipekee.

Yesu aliwekwa katikati ya waovu kuonesha dharau na dhihaka dhidi yake. Lakini pia tukio hilo lilikuwa na maana kubwa sana kiroho. Tukio la Bwana Yesu Kristo kuwekwa katikati ya waovu liliashiria utawala wa Nuru katikati ya uovu.

Yesu alikata Roho mapema kuliko wale wawili aliosulibishwa pamoja nao hivyo hakukuwa na ulazima wa kumvunja miguu.

Vitabu na maandiko ya injili ya Luka, Mathayo na Yohana vinalenga kuzungumzia ujumbe Mkuu mmoja, ingawa baadhi ya taarifa ndogondogo zinaweza kuachwa au kuandikwa kutokana na kusudio kuu la Mwandishi. Jambo kuu ni kufikisha ujumbe uliokusudiwa.

Ndiyo maana Biblia inavipa nafasi sawa vitabu vyote vya injili ambavyo aghalabu huzungumzia hoja mfanano ili kumpa msomaji taarifa sahihi na kukoleza uzito wa jumbe zilizomo.
Mkuu Hii ni tofauti ya wazi, siyo "kutoa taarifa ndogo tu." Kama tukio lilikuwa muhimu hivi, kwa nini mashahidi wa tukio (mitume au wafuasi wao) waandike tafsiri tofauti juu ya watu waliokuwa pale?

Pia hoja kuwa Yesu hakuvunjwa miguu kwa sababu alikufa mapema ni sahihi, lakini bado haielezi ni kwa nini Injili zingine hazitaji jambo hilo au kutaja tukio tofauti.

Huwezi kusema Injili zina ujumbe mmoja, kisha kupuuza kutofautiana kwao katika maelezo ya msingi ya tukio hilo kuu. Kama ujumbe ni mmoja, ushahidi unapaswa kufanana pia.

Haya ni mapungufu ya kihistoria yanayoonyesha kuwa maandiko haya yameandikwa kwa mitazamo tofauti ya binadamu, si kwa ufunuo thabiti wa Roho Mtakatifu.
 
(Yohana 19:31-33)
Kwa kuwa ilikuwa siku ya maandalizi, Wayahudi hawakutaka miili ibaki msalabani siku ya Sabato, hasa kwa sababu Sabato hiyo ilikuwa siku kuu ya ibada. Hivyo waliomba kwa Pilato miguu ya wale waliokuwa wamesulubiwa ivunjwe na miili iondolewe. Kisha askari wakavunja miguu ya wa kwanza na wa pili waliokuwa wamesulubiwa pamoja naye. Lakini walipomjia Yesu wakaona kuwa tayari alikuwa amekufa, hawakuvunja miguu yake.

Kumbuka Yohana aliandika awali:
"Hapo wakamsulubisha yeye, na pamoja naye wengine wawili, mmoja upande huu na mwingine upande huu, Yesu katikati yao." (Yohana 19:18)

Swali: Kama Yesu alikuwa kati ya hao wawili, kwa nini askari walianza kuvunja miguu ya wa kwanza, wakamruka Yesu, wakamfuata wa pili, kisha warudi kwa Yesu? Je, Yohana alikuwa na “uchovu wa kuhariri” (redaction fatigue)?

Swali la pili Na kwa nini tukio hili la kuvunjwa miguu halipo katika Marko, Mathayo wala Luka? Kama kweli limetokea na si hi hadeeth ya kutunga?
Biblia inasema Yohana alimpenda Yesu pengine kuliko wenzake hivyo tangu alivyotiwa nguvu hadi kifo chake yohana alikuwepo akifatilia kila hatua.Petro akamkana Yesu mara tatu na kuondoka kwenye tukio.Wale wahalifu walikatwa miguu ili kuiwahi sabato kwa sababu walichelewa kufa wakati Yesu alikuwa tayari kalala na yote haya yohana aliyashuhudia.
 
Sawa hatukatae mwanzo aliasema Yesu alikua kati kati ya wahalifu sawa, ila kwenye kukata miguu yesu alikua watatu kutoka kwa muhalifu wa kwanza, siuoni kama anajixhanganya mwenyewe ka simlizi Zake????
 
Waandishi wa injiri wamejitambulisha kwa majina yao na historia inawatambua.

Qurani haijulikani aliandika nani kila sura.
Waandishi wake wamejificha kwa sababu ya kuto taka kujulikana:

Tunasoma tu Sura ya Vichuguu, Sura ya Majini, Sura ya ng'ombe jike, sura ya wanawake nk.

Uandishi wa kitapeli unajulikana tu:

Nani aliandika sura ya wanafiki ? Kimya:
Hivi hamsikii aibu kuqestion Biblia ?
Shame on you:
 
Back
Top Bottom