Kwanini tukio liwe karibu na Ubalozi wa Ufaransa?

Sikatai mkuu ila jamaa hadi anachukua silaha kwa askari wawili waliokuwa nazo ni shida sana.

Haiwezekani askari awe na silaha kisha abweteke, wanatakiwa kuwa makini sana wawapo na silaha zao.
 
Waliwahi kuua fisi kwa risasi arobain wakati wananchi huua fisi kwa mkuki mmoja tu.
 
Akili za kupiga risasi na kujua silaha alikua nazo ila wengi watu wa aina yake wanapata vichaa kutokana na trauma za vitaa, wanashindwa ku balance akili zao na wanakua na chuki na police.
Hapo nimekuelewa.
 
Askali polisi ndiyo wazembe. Nadhani walijisahau. Kwa kawaida, ukiwa askali lindoni akikukaribia mtu lazima umuamuru mita kazaa asimame na mikono juu aseme shida yake. So askali ni wazembe!!!!!
 
1. Angekuwa Hana akili timamu asingeweza kupiga risasi yule jamaaa aliyemfuata kwenye kibanda
2. Angekuwa Hana akili timamu angeua raia hovyo kwenye daladala, magari binafsi na bajaji..lakini yeye shida yake ilikua ni Askari tu
 
Askali polisi ndiyo wazembe. Nadhani walijisahau. Kwa kawaida, ukiwa askali lindoni akikukaribia mtu lazima umuamuru mita kazaa asimame na mikono juu aseme shida yake. So askali ni wazembe!!!!!
Mudawote: Sio uzembe wa askari. Kumbuka pale askari wanapokaaga ni kibanda cha nje upande wa baharini, na watu huwa wanapita pale.

Kuna bodaboda mmoja alimgonga mtu maeneo ya pale pale leo, baada ya askari kupima ajali, askari akamwambia bodaboda aache pikipiki hapo ili ampeleke aliyemngonga hospitali.

Jamaa alivyorudi kutoka hospitali amekuta yule askari aliyemwachia pikipiki ndiye kapigwa risasi. Sasa jamaa anaumiza kichwa hiyo pikipiki anaipataje au na yeye atajumuishwa kwenye hiyo issue.
 
Hivi bongo hatunaga sniper..mbona Ile ilikua kazi ya dakika mbili tu..kuliko kurusha risasi hovyo
Ninachoelewa mimi, hata mtu awe mlenga shabaha vipi, kulenga mtu anayetembea ni kazi kubwa na hasa unapolenga na kujibanza kwa kuibia.
 
Mkuu achana na ambush...ni kitu mbaya...
 
Mkuu achana na ambush...ni kitu mbaya...
Ni ambush kweli, japo askari waliamini jamaa ana shida kweli, lakini kumbe alikuwa ana lake kichwani.

Yule askari aliyepigwa bega kumbe alikuwa anakimbia ndiyo akawashwa ya nyuma na kudondoka akikimbilia baharini.
 
Inawezekana! Japo sijafurahia askari wetu. Walivyompiga risasi na jamaa akadondoka, ilitakiwa kumnyang'anya silaha na kuokoa maisha yake ili wapate mengi kutoka kwake.
Askari wa Africa hawa heshimu wahai wa watu, kwaza kulikua hamna haja ya kumumiminia lisasi nyingi mtu tayari kasha pingwa chini, askri wetu wanakosa uledi na professionalism.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…