Kwanini tuliacha kurithi kutoka upande wa mama/kwa wajomba?

Kwanini tuliacha kurithi kutoka upande wa mama/kwa wajomba?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,884
Reaction score
21,175
Zamani wabantu wengi wa pwani ya Tanzania ya leo walikiwa ni matrilineal societies.

Zamani kwa Wazaramo na watu wengine wa Pwani mtu mwenye wapwa aliheshimika kuliko mwenye watoto. Yaani watoto wa dads yako walikuwa na thamani kuliko wako. Hata ukifa mali walirithi watoto wa dada yako. Na kwenye mazishi yako ndiyo walioplay part kubwa.

Pia ikitokea umezingua basi mpwa wako ndiyo alichukuliwa na kuuzwa utumwani. Kwa nini tuliacha mila hizi?

Ukitaka ujue zaidi mila hizi za watu wa mwambao tafuta kitabu Desturi za Wasuaheli na Masimulizi juu ya Wazaramo.
 
Kwasababu mmeiga kwa wachaga.

Wachaga hata mtoto wa kike hapati mgao wa urithi.

Binti wa kichaga akifariki hawamziki kwenye makaburi ya familia. ( Can u imagine wanabagua mpaka maiti)

Je nyie wazaramo mmefikia hatua hiyo?
 
  1. Dini
    • Dini zilizoingia kupitia Waarabu, Waswahili na wamisionari zilisisitiza zaidi mfumo wa patrilineal (uko wa baba) na urithi kupitia wanaume.
    • Hii iliathiri mila za Wazaramo polepole.
  2. Ndoa za kikabila mchanganyiko
    • Wazaramo waliishi karibu na makabila mengine (Wamakonde, Wakwere, Wamatumbi, waswahili wa pwani, wamashomvi).
    • Mchanganyiko huu ulipelekea kuchukua desturi za ukoo wa baba.
  3. Mabadiliko ya kiuchumi
    • Zamani mali kuu zilikuwa ardhi ya ukoo wa mama.
    • Baadaye, kwa ujio wa biashara (hasa karne ya 19–20), wanaume walipata nafasi kubwa ya uchumi (ushirikiano na Waarabu, biashara ya karafuu, kazi mijini).
    • Hii ilibadilisha mizani ya urithi kuelekea upande wa baba.
  4. Ukoloni (Wajerumani na Waingereza)
    • Serikali za kikoloni ziliweka mifumo ya sheria na ardhi iliyopendelea baba kama “mkuu wa kaya”.
    • Hii ilipunguza nguvu za ukoo wa mama.
  5. Mabadiliko ya kijamii na ndoa za kisasa
    • Ndoa rasmi na ndoa za kidini zilihitaji baba kutambulika kama “mkuu wa familia”.
    • Watoto mara nyingi walianza kutumia ukoo wa baba
Nafasi ya mjomba ‘makolo’ bado ipo kwenye ndoa wakati wa mahali nk
 
Back
Top Bottom