Uchaguzi 2020 Kwanini Tume ya Taifa ya Uchaguzi imjibie tuhuma Mgombea?

Mkuu Zygot bado una safari ndefu ya kuelewa haya mambo. Hakuna hata nchi moja iliyo endelea ambayo haina katiba. Nchi kutawaliwa na dikiteta haina maana nchi hiyo haina sheria. Britain ina constitution siyo kama unavyofikiria na zote Japan na Korea zote mbili zina katiba zao. Na popote penye katiba pana sheria. Ni dhahiri wewe huijui dunia. Bado una nafasi ya kujifunza haya mambo, kusoma sayansi isiwe sababu ya kutojua haya mambo.
 
Chezea ugali wewe...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji119].Mwendo wa spana tu[emoji373][emoji373][emoji373]
 
Yapi? Maendeleo yapatikane kwa kurekebisha sheria! Ipi hiyo? Mwambie atoe ahadi za sayansi na teknolojia, Mwanbie atoe ahadi za elimu bora kwa kila mtu. Sheria, sheria, sheria, nonsense!

Wana JF wenzangu wakubwa kwa wadogo, kuna kitu kinaitwa Environmental research, utafiti wa kimazingira. Watu wanaoishi na makada wa ccm wamethibitisha hali hii ambayo haijawahi kutokea ndani ya chama cha mapinduzi, kuwa takribani kila kada wa ccm ndani ya dakika tano anamfikiria Tundu Lissu eidha kwa mabaya au mema.

Hakuna hata kada yoyote wa ccm ambaye ameweza kukaa kwa muda mrefu bila kumuwazi Tundu Lissu. Mjomba wangu ambaye ni kada maarufu na mfia ccm amedai kuwa Tundu Lissu anamsababishia presha maana akimuwazia tu moyo unashituka, hivyo anamkosesha raha maana ana wasi wasi na jinsi anavyoungwa mkono na watu wengi. Mbaya zaidi ni pale anapoona baadhi ya makada wenzake kumuongelea vizuri kwamba Tundu Lissu ni msafi na ndiye anayemkabili Mh. Magu vilivyo.

Baba yangu mdogo yeye ni kada mtiifu wa CCM lakini wanatofautiana sana na mjomba wangu kwa kumuwaza Lissu kila mara kama mkombozi na mwenye uthubutu wa kumsema Mh.Magu bila kuogopa, maana baba mdogo anasema kuwa Magu anafanya kazi vizuri lakini ana kauli na kiburi cha kufikiri yeye ndio mtanzania anayejua mambo yote kuliko wengine na mwenye uchungu kuliko wote kitu ambacho anasema siyo kweli. Jambo lingine baba mdogo anasema ndani ya ccm wapo watu wengi ambao wanampenda Lissu kwa sababu hana tuhuma halafu amekuwa akitetea rasilimali na wananchi siku zote. Utafiti wa kimazingira umeonyesha makada wa ccm wanamuwazia Lissu sana kila baada ya 1-5 hadi tano lazima wafanye hivyo.

Hitimisho ni kwamba hakuna aliyetarajia ndani ya chama cha mapinduzi kama angetokea mtu yeyote katika uchaguzi huu ambaye angeweza kuleta changamoto kama Lissu anavyofanya leo. Kila mmoja alitarajia kuwa ccm isingeweza kutumia nguvu kubwa kunadi mgombea wao, ila mambo yamekuwa tofauti na matarajio. Hali ilivyo sasa inatisha maana kuna wasi wasi kwamba Lissu anaweza kuchukua nchi ndio maana imeanza kutumika nguvu kubwa ya vyombo vya dola na tume ya uchaguzi. Kumbuka mwanzoni mwa kampeni, mgombea wa Urais ccm alidai picha za mafuriko ya Lissu ni za 2015, makada wengine wakasema ni zakuedit, leo wanadai wanaofurika kwa Lissu siyo wapiga kura maana hawajaandikishwa. Lissu makada wa ccm wanakuwaza sana.
 
Utafiti! Nani afanye utafiti? Mnyika, no! Lissu, no! Msigwa, no! Mbowe, no! Nyarandu, no! Nawataja hawa ili usijiaminishe kwamba kila unachohisia ni utafiti.
 
Kusoma sheria na historia isiwe sababu ya kutojifunza sayansi! Najua ni ngumu sana lakini komaa tu! Machache utakayovuna yatakufaa. Angalau ujue kwa nini mkojo wako una rangi tofauti na maji unayokunywa.
 
Tunasema kila siku humu hamuelewi[emoji23][emoji23][emoji119][emoji119],huu uchaguzi ni geresha tu,nyie mnashupaza shingo,eti ni yeyeee[emoji23][emoji23]!!.hata hakuna haja ya kupiga kura.wastage of time ...
Wewe piga Kura matokeo tuachie sisi,Mwaka huu tushawaandalia chungu yao.
 

Kwa sababu tume = CCM na CCM = tume.

Yale mambo ya a=b=c=D ya yule kamanda wa Arusha.
 
Kusoma sheria na historia isiwe sababu ya kutojifunza sayansi! Najua ni ngumu sana lakini komaa tu! Machache utakayovuna yatakufaa. Angalau ujue kwa nini mkojo wako una rangi tofauti na maji unayokunywa.
Naona umetoka kabisa nje ya mada ya msingi. Kwa taarifa tu taaluma yangu ni biomedical sciences yangu na nikatop na degree ya social sciences. Hivyo naongelea from an informed position.
 
Lissu ni mwanasherai kila sehemu anadhani ni mahakamani. Anazua kesi! MWambieni atoe ahadi za maendeleo. Rais gani anaahidi kurekebisha sheria, kwani yeye ni Bunge?
Wale wengine wanaotumia pesa za umma kama za kwenye wallet zao hadi kuamua kujijengea kiwanja cha ndege kwao kwani wenyewe ni bunge.
 
Hakuna tume huyo Charles MHera ni boya moja lipo lipo tu yaani limewekwa pale kuthibitisha kwamba limejiandaa kuingiza nchi vitani yaani na lile domo lake linaropoka tu halijuwi repercusion yake yaani mkurugenzi wa tume unakiri kabisa kwamba wananchi watapigwa mabomu yaani unadeclare vita. Aisee huyo wa kufungwa jiwe shingoni na kutoswa baharini muuaji kabisa
 

Yaani ingewezekana huyu akapige kampeni uwanjani tu maana anatamani sana kufanya hivyo. Kama bosi wake na wafuasi wake wamepigishwa kwata na mtu mmoja mpaka wanagongana vichwa wenyewe na kuishiwa pumzi mapama hivi, sijui wangekuwepo wapinzani kama 4 wenye nguvu nafikiri watu wangelazwa motuary
 
Sheria ni sheria, haijalishimahakamaniwalavyombovinavyotumiasheria ie tume ya taifa ya uchaguzi....uliona wapi kanuni inasema fomu za mgombea urais zithibitishwe na mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi halafu ikathibitishwa na msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya?Haitakiwi kuwa na degree ya sheria kujua tofauti ya taasisi hizo mbili.
Lissu ni mwanasherai kila sehemu anadhani ni mahakamani. Anazua kesi! MWambieni atoe ahadi za maendeleo. Rais gani anaahidi kurekebisha sheria, kwani yeye ni Bunge?
 
umesema Mtanzania
 

Umeandika maneno mengi alafu ujinga mtupu tofautisha kati ya tume ya uchaguzi na mapenzi binafsi ya kwenu na CCM embu muwe mnasoma kinachoandikwa kwanza sio mnavamia muonekane na nyie mnakomenti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…