Hayo aliyosema Mkurugenzi wa Uchaguzi ni makatazo kama yalivyo ndani ya Kanuni na Taratibu walizokubaliana wadau wa Uchaguzi huu wa 2020. Wadau hao ni pamoja na vyama vya siasa, serikali na NEC, wote walitia sahihi makubaliano hayo ambayo yanawataka wadau kuyaheshimu na kuyaishi. Makubaliano hayo, pamoja na mambo mengine ni kutumia lugha ya staha au kistaarabu, kuepuka UCHOCHEZI, UONGO na UZUSHI. Hayo matatu ndiyo amekuwa anayasema Lissu popote apitapo badala ya kusema sera za CHADEMA. Kwa vile hazipo, basi Lissu kajikita kwenye uongo, uzushi na kuzungumzia mtu/watu binafsi! Hivyo Mkurugenzi wa Uchaguzi kama "refa" ana haki ya kukemea hayo.
Zaidi ya hayo, CCM na mgombea wao wa Urais hawawezi kumkemea Lissu, hiyo ni kazi ya NEC; hao ndio wanaweza na ndicho walichofanya. LAKINI kwa sababu Lissu anayo maelekezo maalum kutoka kwa akina AMSTERDAM, basi hasikii na hasa hasa ukitilia maanani kuwa akina Amsterdam wana MONITOR asemayo na aropokayo kwa maelekezo ya hao mabeberu, kupitia kamtambo kadogo alikofungiwa Lissu, hivyo HAWEZI KUACHA UPUUZI HUO. This is because he is paid to do that kwa nia na lengo la kuuvuruga uchaguzi wetu. Hiki kinaonekana na namna viongozi wote wakuu wa CHADEMA walivyo mtenga na kumuacha Lissu on his own; wamemuacha aendelee na mabeberu wake kwani wao (hao viongozi wakuu wa CHADEMA) hawana mahali popote pa kukimbilia kutokana na mipango ya Lissu ya kutaka kuleta vurugu nchini. Huu ndio UHALISIA wa mambo ya Lissu, CHADEMA na akina AMSTERDAM. Nawasilisha kwa mjadala wenye HOJA!