Kwanini tuna watakatifuza (kuwapa utakatifu) viongozi waovu?

Kwanini tuna watakatifuza (kuwapa utakatifu) viongozi waovu?

Mfumo hauwezi ishinda tabia
Unamaana hata hawa Mama anatwanga maji kwenye kinu tu kwa sababu tabia ndiyo inayo tamalaki?

FtDX74wX0AQK8IT.jpeg


FtF0boxXwAISPXm.jpeg
 
Uko sahihi kwa upande mmoja lakini hao wote ambao walikua waovu hapo mwanzo waliongoka, wakashika njia za Mungu na wakawa ni mfano wa matendo mazuri yampendezayo Mungu. Shida ni kwa hawa viongozi wetu, je walitubu na kuongoka na jamii ikaona uwepo wa Mungu kwao?
Hapo huwezi kujua bayana na kwa uhakika kwani toba ya kweli ni baina ya anayetubu na muumba wake. Dakika moja ya mwisho inatosha sana kwa mtu kuupokea wokovu e.g. Wale majambazi wawili waliosulubiwa pamoja na Yesu msalabani -mmoja alitoa kebehi lakini yule wa pili aliomba msamaha na alisamehewa papo hapo na kupewa zawadi ya kuwa peponi....
 
Amani iwe nanyi

Maandiko matakatifu yanasema, tutahukumiwa kwa kadiri ya matendo yetu. Kwani ata mambo tuyafanyayo sirini, mwenye-enzi Mungu ambaye ndiye hakimu wa haki anayaona.

Kwa muktadha huo basi, sisi wanadamu tunapata wapi mamlaka ya kuwatakatifuza viongozi wetu? Nina pata ukakasi ninaposikia kiongozi huyu au yule anafanyiwa mchakato ili atangazwe mtakatifu au yuko mbinguni.

Huu ujasiri tunautoa wapi, je sisi ni mawakala au wasaidizi wa huyo hakimu wa haki? Je hatuoni kama tuna mpangia nini cha kufanya wakati anatekeleza majukumu yake? Ni nani anayeweza kumpangia Mungu kitu cha kufanya au kushawishi namna ya kutekeleza majukumu yake.

Mungu wetu ni mwenye huruma na si mwepesi wa hasira na ni mwingi wa rehema, lakini hatupaswi kumdhihaki. Utakatifu ni kufanana na Mungu, kuwa na matendo yanayo fanana na ya Mungu. Je tuna weza shuhudia hayo kwa hao wapendwa wetu?

Katika mizania ya kibinadamu viongozi wetu waliotangulia mbele ya haki hawakutufanyia haki, walishindwa kuongoza nchi yetu kiuadilifu na hawakutumia rasilimali zetu vizuri.

Kwa miaka zaidi ya hamsini ya uhuru, nchi yetu bado ni masikini na watu wetu bado ni mafukara. Walishindwa kuweka na kutetea haki, watu walidhulumiwa mali zao kwa misingi ya sera za kisiasa ( ujamaa na kujitegemea), watu walikufa kwa njaa kwa kutekeleza sera za vijiji vya ujamaa na uchumi wetu uliporomoka kwa kupigana vita isiyo na msingi na yule joker Idd Amini.

Kwa kuamua kupigana vita peke yake, maisha ya askari, watu, wanawake na watoto wasio na hatia yalipotea. Watu wengi walipoteza mali na wapendwa wao kwa sababu ya vita ambayo ingeweza kuepukika.

Ukiachilia udhalimu wa awamu hiyo, awamu ya tano ndiyo mbaya zaidi, watu walikatwa mikia, waliporwa mali zao, account zao kwenye benki zilifilisiwa na wenyewe kutishiwa vifungo, wanasiasa waliwekwa magerezani, wengine hawajulikani walipo mpaka sasa. Kiasi cha zaidi ya 4 Trillion kimepotea... kimsingi serikali iligeuka jambazi, na mpaka sasa hela za plea bargain hazijulikani zilipo.

Kwa moyo mkunjufu kabisa, nina waomba ndugu zangu, tusimdhihaki Mungu kuingiza siasa zetu za kibinadamu kwenye michakato ya Mungu. Wapo watu wanyonge, wajane na yatima wanaomlilia Mungu kwa madhila ya udhalimu wa viongozi weu, je mnataka Mungu asiwasikilize kwa sababu zenu za kisiasa za kutaka kutukuza na kutakatifuza udhalimu?

Tusimtanie Mungu.
St. Magufuli utuombee
 
Hapo huwezi kujua bayana na kwa uhakika kwani toba ya kweli ni baina ya anayetubu na muumba wake. Dakika moja ya mwisho inatosha sana kwa mtu kuupokea wokovu e.g. Wale majambazi wawili waliosulubiwa pamoja na Yesu msalabani -mmoja alitoa kebehi lakini yule wa pili aliomba msamaha na alisamehewa papo hapo na kupewa zawadi ya kuwa peponi....
Je utakatifu ni nini? Mfano wa maisha mema au kuingia mbinguni tu? Je yule jambazi aliyetubu msalabani ni mtakatifu au ni mkazi wa mbinguni?
 
1.Je utakatifu ni nini? 2.Mfano wa maisha mema au kuingia mbinguni tu? 3.Je yule jambazi aliyetubu msalabani ni mtakatifu au ni mkazi wa mbinguni?
1. Ni hali ya mtu kujitahidi kuishi maisha yanayozingatia maelekezo ya Muumba wake.
2. Unaanza kuishi (ukiwa hai)maisha yampendezayo Mungu a.k.a maisha mema na hatimaye ukifa unapewa tuzo la kuingia mbinguni. Lakini pia inawezekana(hili ni kwa mtizamo wangu tu) ukapata msamaha kutokana na toba ya kweli na hivyo ukastahilishwa kuingia mbinguni kwa neema tu na wala sio kwa mastahili yako. Hilo ni Mungu peke yake analijua.
3. Ni vyote kwa pamoja. Huyo aliitwa Dismas na kwa RC sikukuu yake huadhimishwa tar.25March.
 
Back
Top Bottom