Kwanini tuna watakatifuza (kuwapa utakatifu) viongozi waovu?

Hapo huwezi kujua bayana na kwa uhakika kwani toba ya kweli ni baina ya anayetubu na muumba wake. Dakika moja ya mwisho inatosha sana kwa mtu kuupokea wokovu e.g. Wale majambazi wawili waliosulubiwa pamoja na Yesu msalabani -mmoja alitoa kebehi lakini yule wa pili aliomba msamaha na alisamehewa papo hapo na kupewa zawadi ya kuwa peponi....
 
St. Magufuli utuombee
 
Je utakatifu ni nini? Mfano wa maisha mema au kuingia mbinguni tu? Je yule jambazi aliyetubu msalabani ni mtakatifu au ni mkazi wa mbinguni?
 
1.Je utakatifu ni nini? 2.Mfano wa maisha mema au kuingia mbinguni tu? 3.Je yule jambazi aliyetubu msalabani ni mtakatifu au ni mkazi wa mbinguni?
1. Ni hali ya mtu kujitahidi kuishi maisha yanayozingatia maelekezo ya Muumba wake.
2. Unaanza kuishi (ukiwa hai)maisha yampendezayo Mungu a.k.a maisha mema na hatimaye ukifa unapewa tuzo la kuingia mbinguni. Lakini pia inawezekana(hili ni kwa mtizamo wangu tu) ukapata msamaha kutokana na toba ya kweli na hivyo ukastahilishwa kuingia mbinguni kwa neema tu na wala sio kwa mastahili yako. Hilo ni Mungu peke yake analijua.
3. Ni vyote kwa pamoja. Huyo aliitwa Dismas na kwa RC sikukuu yake huadhimishwa tar.25March.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…