Kwanini tunaamini dini tulizoletewa na Wazungu na waarabu ni njema?

Kwanini tunaamini dini tulizoletewa na Wazungu na waarabu ni njema?

XaviMessIniesta

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
2,231
Reaction score
2,778
Wakati wa ukoloni na utumwa, hawa watu walitupatia elimu mbovu, walitupatia malazi na mavazi mabaya, walitupatia chakula kibovu, walituibia malighafi nyingi kwa udanganyifu
Bila kusahau madhila mengi waliyotufanyia kama vile watumwa wa kiume kuhasiwa na wengine kuuwawa kwa kutupwa porini na baharini.

Sasa swali linakuja, Je, kwa nini tunaamini walitupatia Dini nzuri? Kwamba mengine yote tunaona na tunakubaliana kuwa walitufanyia mabaya na ya kikatili, halaf Dini pekee ndio kitu pekee kizuri waliyotufanyia?


"During slavery and colonial, they didn't give us good education, good housing, good clothes or good food, what makes you think that they gave us GOOD RELIGION?
 
na wewe kwanini unaiamini hyo smartphone yako ya kikorea/kichina/ yenye teknolojia ya kimarekani
 
Sasa swali linakuja, Je, kwa nini tunaamini walitupatia Dini nzuri? Kwamba mengine yote tunaona na tunakubaliana kuwa walitufanyia mabaya na ya kikatili, halaf Dini pekee ndio kitu pekee kizuri waliyotufanyia..
Hata simu au computer hiyo unayotumia kupost umeletewa na mzungu. Kwa kuwa imani haipo kisheria, unaweza ukaacha tu
 
Mkuu TE="Faru Kabula, post: 27328167, member: 14729"]Hata simu au computer hiyo unayotumia kupost umeletewa na mzungu. Kwa kuwa imani haipo kisheria, unaweza ukaacha tu[/QUOTE]
Mkuu dini ililetwa wakati wa utumwa na ukoloni, kitu gani kinakufanya uiamini wakat mzungu kipindi hicho hakuwa na jema kwako?
 
Mkuu nikuulize kuna kitu gani ambacho chetu tumekishikiria mda wote?
Madawa yanatoka nje, technology inatoka nje.
Kwahiyo usihoji sana hilo
 
Tupe kwanza tafsiri ya neno DINI ndio tuamini ni jambo zuri...!

Mbona Mchina, Muhindi, Mkorea n.k
awaabudu dini uliyoletewa na Mkoloni na maisha yanaendelea..?
 
kuna watu wanataka waiendeshe dunia ktk misingi wanayoitaka wao,ukianza kufuatilia dini utagundua mambo mengi yakiudhaifu ambayo hata hao wenye dini wamekuwa wakijigawanya ili wajipatie ridhiki nakuleta mitafaruku!. dini ni njia tu ya kiulaghai ili utawaliwe, a something called Mungu ni dhana. kama wana Mungu kweli anaetupenda angetutetea si kwa mateso yale. na wala si hili tu ikibidi huko mbeleni tunaweza kupata adui mmoja ambae ataunga dunia ili tupambanenae lkn huenda akawa ni adui wa kutengeneza.
 
Hatuamini ktk dini ila tunaamini ktk Jina la Yesu Kristo.

Kwa Moyo mtu huamini na kwa kinywa mtu hukiri hata kupata wokovu - Warumi 10:9-10

Yesu alikuja kuukomboa ulimwengu wote na sio wayahudi pekee, Yohana 3:16.

Tunaamini ktk Wokovu kwa njia ya Yesu Kristo na sio dini.
 
Tupe kwanza tafsiri ya neno DINI ndio tuamini ni jambo zuri...!

Mbona Mchina, Muhindi, Mkorea n.k
awaabudu dini uliyoletewa na Mkoloni na maisha yanaendelea..?
Ndio maana ni kauliza kwanini sie tumezing'ang'ania hizi madhehebu ya wazungu na waarabu?
 
Tupe kwanza tafsiri ya neno DINI ndio tuamini ni jambo zuri...!

Mbona Mchina, Muhindi, Mkorea n.k
awaabudu dini uliyoletewa na Mkoloni na maisha yanaendelea..?
Naongelea n haya madhehebu ya kikristo na kiislamu
 
Baada ya kudanganywa kuna moto wa milele baada ya kifo kama hutaamini. Tulidanganyika, mimi sidanganyiki, naamini ninachokiamini tangu zama za mababu
 
Hata simu tunaziamini sana kuliko mahusiano
 
Back
Top Bottom