Kwanini tunaamini dini tulizoletewa na Wazungu na waarabu ni njema?

Kwanini tunaamini dini tulizoletewa na Wazungu na waarabu ni njema?

Walikuwa wanaabudu chini ya mti ulioteuliwa na wazee wa mila au mlima. Wazungu wakaona ni ujinga tukakubali. Vitu viwili nisivyovipenda vya wazungu ni Ukristu na ukoloni Mamboleo. Nimejibu swali lako Irokos
 
Nani kakuletea dini? Utamaduni wenu nimeacha na mmevamia Utamaduni wa magharibi, madawa/tiba is European technology, hiyo simu unayotumia ya mzungu....
Simu nayotumia ni ya mchina mkuu
 
Hata wao hawajui zimetoka wapi lakini wanaziheshimu. Na wewe heshima hizo imani za mababu kama vipi chochote unachoamini hata kama ni mlima. Hata atheist ana anachoamini
Ndiyo maana nasema haya ni masuala ya imani kila mtu ana uhuru wa kufuata anapoona panafaa,sasa zikianza mada za sijui kuna imani za kigeni kutoka kwa waarabu na wazungu basi pia lazima wengine tuanze kujiuliza pia mababu zetu imani zao walizitoa wapi nao?

Kila mmoja aheshimu anachoamini mwenzie.
 
Walikuwa wanaabudu chini ya mti ulioteuliwa na wazee wa mila au mlima. Wazungu wakaona ni ujinga tukakubali. Vitu viwili nisivyovipenda vya wazungu ni Ukristu na ukoloni Mamboleo. Nimejibu swali lako Irokos
Wazee wetu wangekuwa nao na dini yao basi hata baada ya ukoloni leo hii nasi tungebaki na dini yetu kama ilivyofanyika sehemu zengine.
 
Sisi kwanza sio watu wa ku reason, tunapenda kuletewa tu.
 
Wakati wa ukoloni na utumwa, hawa watu walitupatia elimu mbovu, walitupatia malazi na mavazi mabaya, walitupatia chakula kibovu, walituibia malighafi nyingi kwa udanganyifu
Bila kusahau madhila mengi waliyotufanyia kama vile watumwa wa kiume kuhasiwa na wengine kuuwawa kwa kutupwa porini na baharini.

Sasa swali linakuja, Je, kwa nini tunaamini walitupatia Dini nzuri? Kwamba mengine yote tunaona na tunakubaliana kuwa walitufanyia mabaya na ya kikatili, halaf Dini pekee ndio kitu pekee kizuri waliyotufanyia?


"During slavery and colonial, they didn't give us good education, good housing, good clothes or good food, what makes you think that they gave us GOOD RELIGION?
Hivi mkuu haujui kuwa kuna jukwaa LA dini.
 
Mkuu maovu(dhambi) hata bila hayo madhehebu jamii inayapinga na haiyataki, halaf mkuu mbona machafuko na mitafaruku mingi imesababishwa na hizo dini au hilo hulioni?
Hapana kamanda.Mitafuruko ni michache kulinganisha na faida.Viongozi wa dini wanafanya kazi nzuri ya kutukumbusha kuishi kwa maadili.Dini zote zinafanya kazi nzuri isipokuwa chache kama Free mason.
 
Arudipo kwa mara ya pili ndipo kila mmoja akilini mwake hakuna atakachofikiria isipokuwa kama alimkiri ni Mungu kwa kinywa chake na akaamwamini.

Heri upumuaye sasa, mkiri Yesu kristo kuwa ni Bwana na uamini ndani ya Moyo wako kuwa atarudi kuja kuchukua kanisa lake.
 
Hapana kamanda.Mitafuruko ni michache kulinganisha na faida.Viongozi wa dini wanafanya kazi nzuri ya kutukupungusha kuishi kwa maadili.Dini zote zinafanya kazi nzuri isipokuwa chache kama Free mason.
Kwani Freemason ni dini?
Unajua freemason wanafanyaga nin?au unaongelea hearsay
 
Kwani Freemason ni dini?
Unajua freemason wanafanyaga nin?au unaongelea hearsay
Unatoka nje ya box.Dini zote za kiislamu ,kikristu na kihindi zinakemea maovu na kusisitiza matendo mema na utu.Hata kama si dini zetu za asili ila zinatusaidia katika kukumbusha maadili.
 
Kumekuwa na baadhi ya watu,wao hupinga hizi dini zilizoletwa na waarabu na wazungu. Huku wakitaka waafrika tujikubali na kuthamini dini za mababu zetu kabla ya kuja wakoloni. Binafsi sijui hao mababu walikuwa wafuasi wa dini zipi. Ila kwa masikitiko makubwa miongoni mwa hao watu wapinga dini,wengi wao ni wasomi. Na wanapata huo msukumo wa kupinga hizi dini kwasababu ya kuelimika kwao. Lakini hiyo elimu waliyonayo pia ililetwa na hao hao waliotuletea dini. Kwanini tuwe na msimamo wa kubagua vya kuviacha ilihali vyote tumeletewa? Kwanini tusipinge na huu mfumo wa elimu tulioletewa na kufuata ule mababu zetu kabla ya ukoloni? Tuanzie hapa kwenye elimu,tutumie jando na unyago kuelimisha vijana wetu.

Naomba kuwasilisha.
 
Kwani elimu imeletwa na nani kati ya wamisional na maustadhi waarabu? Naomba unijuze
 
Mwafrika akipiga tambiko la kufa mtu , mvua inanyesha na ukame unapotea , lakini ukipasua sala hizi za kigeni hata upige magoti mpaka magoti yachubuke hakuna kitu . Ni kwa nini mwafrika ukapuuza mila yako ? Maafa yote yanayotupata ni kupuuza utamaduni wetu na kukumbatia wa kizungu .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom