Kwanini tunachaguana wenyewe kwa kupendana lakini ndoa zetu hazidumu?

Kwanini tunachaguana wenyewe kwa kupendana lakini ndoa zetu hazidumu?

Muuza viatu

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2020
Posts
3,840
Reaction score
7,920
Jpili iliyoisha nilihudhuria sherehe ya ndoa ya kutimiza miaka44,ktk ufunguz wa sherehe waliweka clip iliyorekod wanandoa wakisimulia namna ya ndoa yao ilivyoanza na nadhan walitumia njia ya kurekod labda kwa vile walishindwa kuhadithia moja kwa moja mbele ya hadhira.

Ktk simuliz yao Mzee anadai mwaka 78 alipata ajira ya serikal na kumlazimu kutoka mkoan kuja dar kuanza maisha ya utumish,lkn baada ya kufika dar ukizingatia tayar alikua na kipato+makaz bora akaona isiwe tabu akakwanyua bint ambaye anatoka nae mkoa mmoja na kuanza nae maisha.

Baada ya miez kadhaa tangu aje Dar akatembelewa na kaka zake wawil ambao walikuja kwa lengo la kupajua anapoish kitinda mimba wao na baada ya kufika anapoish wakakaribishwa na shemej yao mtoto wa haja mtoto lain mtoto mteke kwa mujibu wa maelezo ya Kaka wa Mzee.

Baada ya salam na kukaribishana jamaa akaona isiwe tabu aanze kuwatambulisha wagen wake kwa mwenyej wao na hapo kipind cha maswal na majibu kikaanza kati ya bint na shemej zake.

Mashemej; kwa nin upo hapa?

Bibie;km alivyosema mwenzangu kwa vile mim na yy tunatoka mkoa mmoja ukizingatia tunapendana kwa dhati na umri unashabihiana tumeona bora tuanze maisha pamoja

Mashemej;nyumban kwenu wanajua km unaish na mtu?

Bibie;hawajui

Mashemej;unapata wap ujasir wa kwenda kuish kwa mwanaume ambae hajajitambulisha kwenu ukizingatia mila za kwetu unazijua vzr tu?

Bibie;[emoji17][emoji17][emoji17]

Mashemej;kwenye familia yenu kuna ambae alishawah kufanya maamuz km haya ambayo ww umeyafanya?

Bibie;[emoji17][emoji17][emoji17]

Mashemej;kijana kachukue nguo za huyu bibie aende kwake.

Majadiliano yakaisha hivyo na jamaa akaahidiwa kuwa baada ya miez kadhaa ataletewa mke.

Baada ya miez kadhaa jamaa akaambiwa kuwa msichana ameshapatikana wanafata taratibu za kifamilia ili ndoa ifanyike.Baada ya siku jamaa akapelekewa mke mpaka pale kwake na maisha yakaanza rasmi ya mke na mume.

Kwa sasa wana wajukuu 19 huku wakisubir kifo kiwatenganishe.

Najiuliza hivi sisi wa sasa tunafeli wap?

Kwanini tunachaguana wenyew tena kwa kupendana lkn ndoa zetu hazidumu???
 
Nilishawahi kuwaza kama wewe. Siku hizi kuna Uhuru Sana na utandawazi hakuna kuchaguliana mpewa mamlaka ya kumchagua yule akufananae na wakuendana nae but

Shida inaanzia hawadumu ulimtafuta mwenyewe nanukajithibitishia na kuridhia kila Jambo juu yake iweje mshindwane.

Tofauti na zamani walichaguliwa mke na mume na waliishi muda mrefu kwa maelewano na Upendo je kipi tatizo Hapa

Mifano halisi ni wazazi wetu 1995 kurudi nyuma
 
Nina suaruali mbili ambazo nilizinunua zaidi ya miaka 10 iliyopita... naamini nilizipenda!!

Baada ya kufika home kila ninayojaribu niivae, naishia kuivua na kuirushia popote pale itakapotua!! Moja kati ya hizo sijawahi kutoka nayo nje hata mara moja, na nyingine labda nimewahi kutoka nayo nje mara mbili tatu lakini around tu!!

Sasa ikiwa nguo tu tunaweza kununua kwa kuamini tumezipenda lakini ukifika home unagundua kumbe uliingia cha kike, seuze ndoa!!+
 
Nikwasababu mnachagua kwa kuangalia vigezo vya kimwili...

Mfano...Mzuri, kalio kubwa, Hb, ana pesa, anajua mambo kitandani...

Wakati wa kuoa au kuolewa inapaswa kuomba sana, japo kuomba tunapaswa iwe siku zote za maisha ya duniani...

Hapo Mungu atakupa mume na mke wako aliyekupangia...

Na sio mliochaguana kwa tamaa za mwili...

Mke mwema nani amjuaye...kima chake chapita majirani moyo wa mumewe humwamini...

Methali31: 10
 
Kwa experience yangu ndogo ukimuoa mty au kuolewa kisa ummpemda ndoa nyingi hazidumu sbb ziko wazi wivu na ukiangalia hawa wazee wetu wlioa kwa sbb maalum co mapenz.
Mfano mzee wang alnmbia almuoa bmkubwa kwa sbb kwao kulkua na elimu mshua wafugaji kwaio akatman apate wasomi na kafanikiwa.
Father mkubw alnmbia almuoa m/ mkubwa kwa sbb ukoo wao wlkua shupavu altk mtu wa kmsaidia kuangalia mifugo mpk xx n tajiri wa mifugo so mantik iyo inaonesha ukioa cjui nmmpenda blah blah ni disaster. Mwenye experience tofaut na hiyo share[emoji120][emoji120]
 
Utandawazi, kukosa uvumilivu miongoni mwa wapenzi , Wanaume sikuhizi tumekosa busara ya kudeal na changamoto za kimahusiano.

Mahusiano ni matamu sana ukimpata akupendae na wewe ukampenda ila swala la migogoro ni constant busara na hekima na namna unavyotatua hiyo migogoro ndo huamua mdumu kwa muda gani.
 
Nina suaruali mbili ambazo nilizinunua zaidi ya miaka 10 iliyopita... naamini nilizipenda!!

Baada ya kufika home kila ninayojaribu niivae, naishia kuivua na kuirushia popote pale itakapotua!! Moja kati ya hizo sijawahi kutoka nayo nje hata mara moja, na nyingine labda nimewahi kutoka nayo nje mara mbili tatu lakini around tu!!

Sasa ikiwa nguo tu tunaweza kununua kwa kuamini tumezipenda lakini ukifika home unagundua kumbe uliingia cha kike, seuze ndoa!!+
WELL SAID mkuu..!!
 
Back
Top Bottom