Kwanini tunachaguana wenyewe kwa kupendana lakini ndoa zetu hazidumu?

Kwanini tunachaguana wenyewe kwa kupendana lakini ndoa zetu hazidumu?

Nikwasababu mnachagua kwa kuangalia vigezo vya kimwili...

Mfano...Mzuri, kalio kubwa, Hb, anapesa, anajua mambo kitandani...

Wakati wa kuoa au kuolewa inapaswa kuomba sana, japo kuomba tunapaswa iwe sikuzote za maisha ya duniani...

Hapo Mungu atakupa mume na mke wako aliyekupangia...

Na sio mliochaguana kwa tamaa za mwili...

Mke mwema nani amjuaye...kima chake chapita majirani moyo wa mumewe humwamini...

Methali31: 10

Mbona ndoa za zamani nyingi zilidumu?

Au hii principal haiku apply zamani?

#YNWA
 
Nilidhani wanaoachana siku zote ni wale wasiopendana but wengi Hadi wanakufa wanaficha maumivu kuwa wameachana ila wanapendana.... Jibu ni lile lile "MAARIFA" +"HEKIMA"
 
Hata mimi ninashangaa vijana wa siku hizi wanachaguana wenyewe na mazoezi ya ndoa wanafanya kabla yaani kutikisa kabla ya kuitumia sisi wa zamani hiyo haikuwepo lakini ndoa hazidumu mafeli wapi vijana wa kidigitali.
 
Ukikubali kupita peku njia yenye miiba kubali mauvi
Wengi wananatarajio makubwa kuliko uhalisia ulioko kwenye ndoa

Movies zinawadnganya sana
 
Utandawazi unaharibu kizazi cha sasa, Haya Ma Simu hasa Simu Janja, TV, mitandao ya Kijamii inaharibu ndoa nyingi. Wanandoa wanashinda mitandaoni wakilinganisha maisha ya marafiki/watu mashuhuri na maisha halisi wayaishio mathalani mwisho wa siku kupelekea migogoro isiyokwisha.

Pia Vijana wa sasa hawana fikra sahihi kwa wakati sahihi wanaponzwa na mihemuko.... Jambo dogo linashindwa kuhimilika. Wenyewe wanasema mafriji yao hayagandishi... Hawawezi tunza siri.

Wazee wetu waliishi maisha yasiyo na mitandao .. hakuna wa kujilinganisha nae. Maisha yalikua murua sana.
 
Jpili iliyoisha nilihudhuria sherehe ya ndoa ya kutimiza miaka44,ktk ufunguz wa sherehe waliweka clip iliyorekod wanandoa wakisimulia namna ya ndoa yao ilivyoanza na nadhan walitumia njia ya kurekod labda kwa vile walishindwa kuhadithia moja kwa moja mbele ya hadhira.
Sababu ni moja tu.

Mfumo dume ulifanya wanawake wa zaman kuwa daraja la pili kwahyo walionewa snaa..

Na hawakua na option dhidi ya kuvumilia..

Huyo mzee hajaeleza yote . Aseme amecheat mara ngap.. ana watoto wa nje wangap?

Wakupewa sifa hapo ni huyo mama ndo kafanya hyo ndoa imedumu.

Karne hii huwez mfanyia mwanamke hayo.. ana elimu. Ana kaz.. ukimchefua anaenda zake..

Hii ndo sababu kuu.
 
Tatizo la sasa ni mabadiliko ya tabia nchi na sera za uchumi wa kisasa. Zama zile wazee wetu walikulia kwenye ujamaa. Kilikuwa ni kitu cha nchi nzima na uchumi ulikuwa centralized kwa serikali tu.

Kitu ambacho raia walijivunia ni maadili mazuri kwenye jamii na ilikuwa ni sifa kwa familia kuwa na vijana waadilifu. Hakukuwa na mashindano yeyote sababu kila mtu alikuwa hana hela kwahio social classess zilikuwa kama hazipo nchini.

Leo hii sera za uchumi zimeshift toka ujamaa na wengi wameushika ubepari. Hii imepelekea utandawazi na muingiliano mkubwa kimataifa. Sahizi trends zimeelekea kwenye nguvu za kiuchumi tu na social classess zimezaliwa kwa wingi. Haya matabaka ndio yameleta balaa.

Coexistence na social interactions leo zinategemea sana uchumi na ndio unaendesha kila kitu. Ujamaa was all about equity and sharing, mtashea nguvu, mtashea uchumi, mtashea almost kila kitu sababu ndio utamaduni wetu ulivyokuwa. Kila Mtanzania ni ndugu ndio ilikuwa mode of operand.

Tukija kwenye effects za mabadiliko ya sera za uchumi na utandawazi kwenye mahusiano ya kijamii ndio sasa mambo ya uchumba hayafati maadili kama zama zile ambako wachumba tulikuwa tunachaguliana. Zamani ilikuwa kuoa mpaka uchaguliwe mke kijijini leo hii huu utaratibu
hauko hivyo kila kijana ana uhuru wa kumchagua mwanamke amtakaye. Muingiliano umekuwa mkubwa sana wa makabila.

Sikuhizi trend imekuwa kuzingatia strong social class kiuchumi ina maana katika selection kuanzia wazazi mpaka vijana wamekuwa focus ni hio. Swala la maadili haliangaliwi sana as long as kijana yuko well off basi ataoa binti yeyote anayemtaka. Wazazi hawana kipingamizi. Matokeo yake ndio kushindwana mbele ya safari sababu kiini cha mahusiano ni tamaa iliokuwa backed of na nguvu za kifweza. Kama mjuavyo kwenye hela haina upambe. Mtu hajui history ya binti ila kwakuwa ana umbile zuri anajitwisha kumbe kaoa malaya.

Ndoa za zamani zilidumu sababu wazazi walikuwa na ufahamu na mwenendo wa binti toka akiwa katika stage za ukuaji. Ina maana tabia zake nzuri ndio ilikuwa fahari ya wazazi. Wakimpointi jua wanakuunga na malisafi. Haina kufeli.
 
Sababu ni moja tu.

Mfumo dume ulifanya wanawake wa zaman kuwa daraja la pili kwahyo walionewa snaa..

Na hawakua na option dhidi ya kuvumilia..

Huyo mzee hajaeleza yote . Aseme amecheat mara ngap.. ana watoto wa nje wangap?

Wakupewa sifa hapo ni huyo mama ndo kafanya hyo ndoa imedumu.

Karne hii huwez mfanyia mwanamke hayo.. ana elimu. Ana kaz.. ukimchefua anaenda zake..

Hii ndo sababu kuu.
Na umalaya umesahau kuungolea inshort tu nguvu za kiuchumi mwanamke haoni sababu ya kuwa submissive so anaweza fanya lolote ambalo ana wish kufanya hata kama litamuumiza ME wake au kuhatarisha ndoa yake.

Wanawake hata wa kileo ukimkata nguvu za kiuchumi akawa anakutegemea wewe by 1OO% anakuwa na adabu vizuri sana.
 
Kwa experience yangu ndogo ukimuoa mty au kuolewa kisa ummpemda ndoa nyingi hazidumu sbb ziko wazi wivu na ukiangalia hawa wazee wetu wlioa kwa sbb maalum co mapenz.
Mfano mzee wang alnmbia almuoa bmkubwa kwa sbb kwao kulkua na elimu mshua wafugaji kwaio akatman apate wasomi na kafanikiwa.
Father mkubw alnmbia almuoa m/ mkubwa kwa sbb ukoo wao wlkua shupavu altk mtu wa kmsaidia kuangalia mifugo mpk xx n tajiri wa mifugo so mantik iyo inaonesha ukioa cjui nmmpenda blah blah ni disaster. Mwenye experience tofaut na hiyo share[emoji120][emoji120]
Mzee Mimi naona mtu aoe mwanamke anayekupenda na siye unayempenda..maana mwanamke ukishampenda Sana utakosa sauti kwake,Ila akikupenda yeye atakua na utii na adabu kwako.
 
Mzee alishanihadithia hadithi Kama hiyo kuhusu yeye..alipokua kijana aliendaga mkoa kupambana huko bahati nzuri Mambo yakamnyookea akarudi kwa wazee wake akiwa na picha ya mchumba ake na tayari walikua washazaa mtoto mmoja kufika alipowaeleza na kutoa picha walipoiona wakaichana Kisha wakamwambia asirudi Tena kule kwanza amezini pili ametafuta mwanamke asiye faa..hivyo akapewa mke brand new akaoa wapo mpaka leo.
 
Zamani walioana ili wajenge familia na ukoo!

Siku hizi wanaoa kwa show off tu
 
Back
Top Bottom