Kwanini tunaenzi wanasiasa peke yao?

Kwanini tunaenzi wanasiasa peke yao?

Kwa nini? Waenziwe hao tu? Kwa nini walio nje ya CCM wasienziwe? Mikoani na mijini naona shule zina majina ya kina Mary Nagu, maghembe etc hao ni viongozi wakuu?
Hilo ndio swali ninalo uliza. Mary Nagu na Maghembe waliwahi kuwa mawaziri kwa hiyo nao ni viongozi ingawa sio wakuu.

Amandla...
 
Kuna taarifa kuwa stesheni za SGR zitapewa majina ya marais wetu. Huu ni muendelezo wa karibu kila kitu cha maana kupewa jina la aliyekuwa Rais (hivi karibuni ni Rais aliyekuwa madarakani).

Tuna shule zinazoitwa Mkapa, Vitengo vya Hospitali vinavyoitwa Kikwete, stesheni za basi za Magufuli, Kiwanja cha ndege cha Nyerere, na sasa hivi tunajenga uwana wa michezo wa Samia Suluhu Hassan Arusha! Hivi ni wana siasa peke yao ndio walioifikisha nchi yetu hapa tulipo?

Kwa nini hizi stesheni hazikupewa majina kama Shaaban Robert (Dar es Salaam), Mbaraka Mwinshehe (Morogoro), Isike (Tabora) na mashujaa wetu wengine ambao tumewasahau! Ingekuwa nafasi nzuri yakuibua watu waliochangia historia yetu kutoka kila sehemu ambayo reli inapita. Kutumia majina ya wanasiasa kunageuza kitu ambacho watanzania wote tumechangia kuwa na sura ya kichama maana hamna mwanasiasa wa upinzani atapewa heshima kama hiyo.

Inabidi tubadilike na tuandike upya historia yetu kwa kutambua kuwa sio lazima uwe Rais ndio uthaminiwe na nchi yetu.

Amandla.

Pia, soma: Si kila jengo, eneo na barabara lazima ipewe jina la Mwanasiasa au Kiongozi. Kuna Wanamichezo na Wasanii wanaopaswa kuenziwa ili kulinda historia yetu
Mkuu, umenena vyema. Nadhani ni vyema mtu jina lake kupewa sehemu moja katika mji husika., vinginevyo tutachanganyikiwa. Kwa mfano, kwa Dar akapewa sehemu nyingi atatu changanya na haipendezi pia, na sio lazima wawe wana siasa.
 
Uliza kwa nini tunaenzi wanasiasa wa CCM tu na siyo wanasiasa. Wakati kuna wanasiasa mahiri waliopigania maendeleo nchi hii na hawapo CCM... Refer Oscar kambona, babu, Mbowe Fundikira, Mapalala etc
jenga shule yako iite jina lako kama mkono secondary Rugambwa Galanous, kulikuwa na danguro linaitwa Mbowe Night Club tulilivunjilia mbali kwa kukiuka maadili
 
Kwa nini hizi stesheni hazikupewa majina kama Shaaban Robert (Dar es Salaam), Mbaraka Mwinshehe (Morogoro), Isike (Tabora) na mashujaa wetu wengine ambao tumewasahau! Ingekuwa nafasi nzuri yakuibua watu waliochangia historia yetu kutoka kila sehemu ambayo reli inapita. Kutumia majina ya wanasiasa kunageuza kitu ambacho watanzania wote tumechangia kuwa na sura ya kichama maana hamna mwanasiasa wa upinzani atapewa heshima kama hiyo.

CCM walishafikia ukomo wa kuleta mambo mapya...
 
Mkuu, umenena vyema. Nadhani ni vyema mtu jina lake kupewa sehemu moja katika mji husika., vinginevyo tutachanganyikiwa. Kwa mfano, kwa Dar akapewa sehemu nyingi atatu changanya na haipendezi pia, na sio lazima wawe wana siasa.
vibao vya anuani za makazi mbona mna bandika majina yenu na hamna shida, au mlitaka na stand zianze kuitwa kingwendu, mzee ojwang, sugu kajenga hotel yake kwani hajaiita mbilinyi?
 
Back
Top Bottom