Kwanini tunaiamini Mahakama kutoa haki?

Kwanini tunaiamini Mahakama kutoa haki?

King Jim

Member
Joined
Aug 12, 2024
Posts
6
Reaction score
16
"If the Court still makes mistakes by condemning the Innocents, Why do we still allow it to provide rights?"

Kama tunajua na kukubali kuwa kuna watu wasio na hatia wako jela, kwanini bado tunaiamini na tunaiachia mahakama kutupatia au kuhukumu kwa haki?

Naamini tunaweza pata suluhisho jingine zaidi ya mahakama.
 
Nanukuu. "Naamini tunaweza pata suluhisho jingine zaidi ya mahakama".
OK. Kwa imani hiyo 👆 👆 👆 hebu toa mapendekezo au ushauri.
*Mimi ninaanza -napendekeza hivi:
1. Kesi ya jinai iwe inasikilizwa katika mahakama 3 tofauti (hiyo sio rufaa) halafu hukumu zikitoka (from each separate mahakama) endapo kama hukumu hizo 3 hazifanani wala hazilingani, basi kesi husika ipelekwe mahakama ya juu moja kwa moja kwa gharama ya Serikali bila kucheleweshwa na iwe ni ndani ya muda mfupi.
2. Magereza na Mahakama kuwe na kitengo cha siri cha "Inteligensia" kitakachoshughulikia masuala ya wafungwa ambao inadhaniwa au inaonekana ni kama vile wamejikuta wanafungwa kutokana na kutokujua sheria(Ujinga) au kukosa "mfadhili" au kukandamizwa na "mkubwa mwenye sauti" i.e. kukomolewa n.k. n.k . Kitengo hiki cha siri kiwe na uwezo wa kutoa Taarifa ya UKWELI ulivyotakiwa uwe. Kitengo kiwe ni cha Siri kiasi kwamba hata mkuu wa Gereza au Jaji/hakimu wa Mahakama asiwafahamu waliomo.
Taarifa za kitengo ziwe zinasomwa na Mwanasheria mkuu wa Serikali au Mteule mwingine.
 
Haki hakuna kama serikali ina maslahi yake!
Mahakimu na majaji wamekuwa sehemu ya kuhujumu haki kwa kupokea matakwa ya Serikali.
 
Haki hakuna kama serikali ina maslahi yake!
Mahakimu na majaji wamekuwa sehemu ya kuhujumu haki kwa kupokea matakwa ya Serikali.
Ndo mana katika kutoa Hukumu huwaga wanesema: "Umepatikana na kosa chini ya Sheria .......... " Hawasemagi eti "Kwa haki unahukumiwa kwenda jela.........."
 
Haki hakuna kama serikali ina maslahi yake!
Mahakimu na majaji wamekuwa sehemu ya kuhujumu haki kwa kupokea matakwa ya Serikali.
Nilidhani tunajadili mahakama kama mahakama na hatujadili serikali. Mahakama, nadhani, kazi yake ni kutafsiri sheria na baadae kutoa haki kwa mujibu wa sheria husika.
 
Back
Top Bottom