Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Waingereza wana msemo wao mmoja "imitation is the sincerest form of flattery".
Mimi nina tatizo tofauti kidogo na wewe, sitaki kuonekana naiga.
Halafu jirani zangu huwa kama wananijua nataka kufanya nini.
Kuna wakati nilikuwa nataka kununua Range Rover Evoque,nikasema Evoque imekaa kama mtu mwenye kibiongo, ninunue Sport. He, ile najikusanya kusanya na kuangalia reviews, jirani yangu mmoja si akanunua Range Rover Sport!
Nikasem asinunui tena, nikinunua itakuwa kama naiga.
Akahama.
Akahamia mwingine.
Akawa na Mercedes Benz SUV.
Nikasema mimi nitanunua ya tofauti, sedan.
Sijakaa vizuri boyfriend wake akawa anakuja na Mercedes Benz AMG 65.
Nikasema isiwe tabu, nakwenda kivingine, tusifanane kabisa.
Nikaishia na BMW X5.
Sasa hivi naona kuna jamaa mwingine naye ana BMW X5, najikusanya niende na Porsche Macan maana naona ndiyo gari ambayo mtaani hakuna.
Damn homie...
You ain’t cop that Macan yet?
I thought you did a couple years ago....[emoji2]