Kwanini tunapenda kushabikia vita?

Waulize wanajifunga mabomu kulipua wasiohusika, Kisha wanaficha silaha kwenye makazi ya watu
 
Sasa iwapo Hamas wameenda wenyewe kuipiga Israel na kisha wakajinadi kuwa wanaenda kuifuta Israel kwenye uso wa dunia unadhani hiyo ni habari ndogo?

Unadhana haina athari kwenye uhusiano wa kimataifa?
 
Waulize wanajifunga mabomu kulipua wasiohusika, Kisha wanaficha silaha kwenye makazi ya watu
Ukraine wanajilipua? Hind Rajab alijipua?

Ninazungumzia kushabikia mauaji ya wananchi bila kujali ni wa upande gani. Kama binadamu hicho sio kitu cha kushangilia.

Mwisho wake tunakuwa kama Omega Mwaikambo ambae wakati wenzake wanapigana kuokoa maisha ya waliotharika na moto uliotokea katika ghorofa la Grenfell yeye alikuwa amekana kupiga picha maiti na kuzirusha kwenye social media platforms!

Unapoona maisha ya binadamu yeyote hayana thamani kabisa ndio mwanzo wa kukosa ubinadamu.

Amandla...
 
Hivi akija alien akakuuliza umuelezee sababu au chanzo cha vita ya Israel na Palestine, utamuelezea vipi ili aone binadamu ni kiumbe mwenye akili timamu?
 
Ni namna ya mwisho ya kushikishana adabu,baada ya manunda kufikia kiwango cha kutokuelewa katika utaratibu wa kawaida
 
Mi nazani vita yenye mtazamo wa Derby ndio yenye mapenzi zaidi kuliko vita zingine, mfano vita ya Urusi na Ukraine sizani kama Kuna ushabiki kama hi inayoonekana ni Derby.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…