Mkuu suala la kuvaa pete mkono wa kushoto ni la karibu dunia nzima ila hilo suala la mkono wa kushoto kuwa najisi sijui mchafu ni la jamii ya nchi fulani tu
Sasa huwezi kujadili suala linalohusu utaratibu wa karibu dunia nzima kwa kutumia imani za jamii ya watu fulani tu
Kama ulivyosema si watu wote wana hizo imani kuhusu mkono wa kushoto, ila ni watu karibu wote duniani huvaa pete mkono wa kushoto wanapofunga ndoa, hasa ukizingatia hizo imani zinazohusu mkono wa kushoto ni dhana potofu tu zilizotungwa na zisizo na uhalisia wowote