Maana kubwa kabisa ya jina nikumu identify mwenye jina.
Ukimnyima uhuru wa kuandika jina lake kama anavyotaka yeye, umemnyima uhuru wa kuchagua jinsi ya kuji identify. Jambo la msingi kabisa katika jina.
Cassius Clay aliona jina lake halimfai, akabadili na kuitwa Muhammad Ali. Jina tofauti kabisa na alilokuwa nalo. Mnashangaa tofauti za spelling? Je wangeamua kujiita von Masssoueai (kutoka Masawe) na O'meera (kutoka Omera) mngesemaje?
Ndiyo maana hata kisheria kuna provisions za kubadili jina ukiona jina lako halikufai, sasa ukielewa hilo huwezi ku obsess over the evolution of African names spelling.
Bottom line, kama jina ni lake, yeye ndiye muamuzi wa linaandikwaje.
Majina yenyewe tumeanza kuyaandika baada ya ukoloni. It's not like tuna rekodi za miaka elfu na elfu yanavyoandikwa.
Mnajuaje kwamba wanavyoweka hizo double letters si sahihi zaidi phonetically kwa kufuata mkazo na yalivyoandikwa bila double consonants yalikuwa hayako phonetically zaidi?
Sidhani kama hoja hapa ni kuwalazimisha kuandika majina bila hizo double latters
Hoja hapa ni mleta mada kutaka kujua kwanini ikawa hivyo
Mohamed Ali alipobadili jina alikua na sababu pia
Ni hulka ya binaadamu kujiuliza kila kitu kwanini ilikua hivi na sasa ikawa hivi, watu wanabadili dini kwa hiyari zao lakini kuna wataalamu wanatafiti kwanini watu wanabadili dini,makazi, jinsia nk
Hoja ya wao kuwa na uhuru wa kubadili watakavyo haiondoi uhalali wa watu kutaka kujua kwanini wakaamua kubadili