Decree Holder
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 2,559
- 3,745
Inawezekana kabisa TAL aliamua kugombea uenyekiti wa Chama taifa mapema zaidi lakini hakutangaza kutokana na historia ndani ya chadema. Historia inaonesha viongozi wote ndani ya chadema walioonesha kuutaka uenyekiti mapema waliundiwa zengwe na kupewa kesi za usaliti kuwazuia kugombea uenyekiti.
Kwa mfano kilichompata Chacha Wangwe kwani alionesha nia mapema sana mwaka 2008 takribani mwaka mzima kabla ya uchaguzi wenyewe. Aliundiwa zengwe akavuliwa uongozi na kuwa labeled msaliti.
Mwingine ni Zitto Kabwe alionesha nia mapema sana akawa labeled msaliti akavuliwa uanachama kabla hata hajagombea.
Kwa kutambua historia hiyo Lissu aliamua kuficha nia yake ya kuutaka uenyekiti wa Chadema na badala yake akatangaza na kutia nia nafasi ya makamu mwenyekiti wa Chama mapema zaidi. Hata alipoulizwa kuhusu uenyekiti alikataa katakata na kuapa kwamba asingempinga mbowe kwenye uenyekiti kwani amemsaidia sana.
Mbowe akaingia katika mtego na kuamini kuwa Lissu atatetea nafasi ya makamu mwenyekiti wa Chama taifa na siyo kugombea uenyekiti wa Chadema.
Ni Lissu peke yake Kati ya wanasiasa waandamizi ndani ya chadema aliyefanikiwa kuchukua fomu na kurudisha tena katika namna ambayo ni ya kushtukiza.
Katika hili Lissu amecheza kama Pele.