Mc Justine Mwakibiki
Member
- May 19, 2024
- 14
- 9
Kwa miaka ya hivi karibuni, tumeshuhudia wimbi kubwa sana la wageni wa kiarabu, kutokea nchini Misri wakizungusha Vyombo/bidhaa zao, kwenye Ofisi,shule,hospital na hata majumbani, wakiuza na kukopesha kama Wamachinga.
Hivi ni kweli kuwa Sera zetu za uwekezaji zinaruhusu hili? Maana kinachoonekana ni kuwa wanakuja nchini kwa sura ya uwekezaji, ila mwisho wa siku wanakuwa wamachinga wa kawaida mtaani, hii imesababisha athari nyingi sana kama ifuatavyo;
1. Biashara za wazawa kufa.
2. Serikali kukosa Mapato Hasa Kodi.
3. Wananchi kuichukia Serikali yao.
4. Kushuka utendaji kazi kwa Wafanyakazi.
5. Hali ya Usalama wa Nchi kuwa Matatani.
-BIASHARA ZA WAZAWA KUFA
Wanapoingia hawa waarabu kama wamachinga, wanasababisha biashara za wazawa kufa, kwakuwa wazawa wanalipa kodi kwa kuweka Fremu za Maduka, ila hawa waarabu wanatembeza bidhaa zao kwenye Magari, wanapita mashuleni,ofisini,mahospitalini n.k yaani shughuli ambayo angefanya Mtanzania anafanya mgeni, ili hali natambua kuwa wageni wanapoingia nchini wanapaswa kuja na kitu cha kipekee/ziada ambacho sisi kama wazawa hatukiwezi.
Nb; Picha hapo juu ni Duka la mlipa kodi, chanzo cha picha ni Facebook
-SERIKALI KUKOSA MAPATO HASA KODI.
Kutokana na kuendesha hizi biashara zisizo rasmi, hii imechangia pia kama nchi kukosa KODI inayotokana na hizi biashara zao, na wakati mwingine hata vibali vyao vya kazi vina walakini mwingi, wanavipata kwa njia za panya hasa pale vinapokuwa vimeisha muda wake, kama wanataka kuwekeza basi wafungue maduka kwenye maeneo yanayotambulika, ili biashara zao ziweze kuwa rasmi, tunawahitaji sana ila wafuate taratibu za nchi.
Nb; Picha hii ni namna wanavyotembeza bidhaa zao hao waarabu.
-WANANCHI KUICHUKIA SERIKALI YAO
Inafika kipindi wananchi wanaamini kuwa, ni serikali yao ndiyo inayaruhusu haya, chukulia mfano Mfanyabiashara wa kitanzania anauza Blender ya JUICE dukani kwake anapolipia kodi, na huyu Muarabu anatembeza bidhaa hiyo hiyo kwenye Gari, mwisho wa siku ni lazima huyu wa Dukani aichukie serikali, kwakuwa Analipa Kodi ya Pango, Alipe wafanyakazi na Kodi ya TRA, ila huyu wa Kiarabu ni kizungumkuti, ndiyo maana maeneo fulani mteja akishindwa kulipa kwa wakati wamekuwa wakiwatishia hata kwa Bastola au hata kuwachania nguo zao, tena wakiwa kwenye vituo vyao vya kazi, je kwa hili wataipenda serikali yao?
-KUSHUKA KWA UTENDAJI KAZI KWA WAFANYAKAZI.
Hii inasababishwa na hawa waarabu, kufanya biashara isiyo ya halali, Waarabu huwa wanajichukulia sheria mikononi, Hasa inapotokea mteja kushindwa kulipa kwa wakati, Waalimu au Wateja Wengi wanakimbia vituo vyao vya kazi kwa kuhofia vurugu zinazoweza kutokea endapo waarabu wakija kudai, kwakuwa hawajui kumsikiliza mteja wao ni pesa tu, wamewahi kuvamia Ofisi ya mkuu wa shule na kuharibu Nyaraka za Ofisini kwake, kisa tu aseme amemficha wapi Mwalimu wanaemdai, lakini ukweli ni kuwa hakumficha, ila hiyo ndiyo tabia yao ya USUMBUFU, wa Tanzania hawana amani na hawa Waarabu kabisa.
WAARABU WAMEKUWA UGONJWA WA TAIFA kila mahali ni kilio.
-HALI YA USALAMA WA NCHI KUWA MATATANI.
Tunaporuhusu hawa wageni kufanya umachinga, tunajihakikishia vipi kuwa lengo lao ni hilo tu? Je kama nyuma ya pazia ni Majasusi waliojipenyeza kwa kivuli cha kuuza vyombo? Isije tokea tukashtuka baada ya madhara mabaya kutokea, ni wakati sahihi wa kuchukua hatua, sasa hivi kila mkoa wa Tanzania, hutakosa WAARABU WAUZA VYOMBO, nchi yetu kiufupi ni kuwa tumeingiliwa jamani.
NINI KIFANYIKE?
Tanzania nchi yangu niipendayo, ni ile itakayotengeneza na kufuata taratibu, za kuwadhibiti hawa wageni wanaokuja kwenye nchi yetu, kufanya biashara ambazo hata watanzania tunaziweza, tunawakaribisha kuja kama wawekezaji wawekeze kwenye maeneo ambayo, kama nchi tutajifunza na kupiga hatua zaidi kimaendeleo..
Ili hata tatizo la Ajira kwa vijana, Ufanisi wa wafanyakazi kushuka, Serikali kukosa Mapato stahiki na hali ya mashaka ya kukosa Amani ISIWEPO TENA, kwakuwa wakija kama wawekezaji watatoa nafasi za Ajira kwa vijana, Serikali itapata mapato, Amani itatawala sehemu za kazi kwa watumishi na Ulinzi kama taifa hautatia shaka tena, ila tukiwaacha waendelee na huu umachinga wao, basi kelele hizi hazitakoma kamwe.

Attachments
Upvote
4