Kwanini tusiwe na maduka ya hadhi nchini ili mawaziri na viongozi wakubwa wasiagize kutoka nje ya nchi?

Kwanini tusiwe na maduka ya hadhi nchini ili mawaziri na viongozi wakubwa wasiagize kutoka nje ya nchi?

Biashara zinaendeshwa Kariakoo kwa sasa hazina tofauti na biashara zilizokuwa zinafanyika miaka ya 1990 za ulanguzi.

Soko linazidi kudorora, maduka yenye hadhi yanazidi kupotea na kuzaliwa vibanda vidogo vidogo visivyo kidhi.

Mpangilio wa biashara nao unachangia soko kukosa mvuto huku bidhaa zenye ubora mdogo zikipewa kipaumbele.

Matokeo yake ni kuibuka kwa wafanyabiashara wachache waliopo serious wanaokwenda kwenye masoko nchi jirani kuchukua bidhaa na kuziingiza nchini kinyemela kisha kuziuza kwa bei kubwa kwa wateja serious.

Upotevu huu wa mapato unachangiwa kwa kiasi kikubwa na kodi nyingi, kukosekana kwa viongozi imara na sera mbovu.

Nchi nzima kuna maduka ya nguo za hadhi yasiyozidi kumi na mengi yanamilikiwa na mtu au kampuni moja. Kwanini tusiwasaidie Watanzania kufungua maduka yaliyopo kwenye ulimwengu wa kwanza hapa nchini?

Mawaziri na viongozi wengine wanaolipwa vizuri wanaenda kununua nguo nje. Kwanini badala ya kununua nje, wasitengeneze mazingira ya biashara kama ya nje? Tulitegemea kwa kuwa na bandari, watu wa madaraja yote wangeingia nchini kufanya biashara, ila sivyo. Tumebaki kutukuza vya Uturuki, Dubai na kadhalika.

Tubadili fikra.
Huku ndo watu wanatajirikia kiongozi mtu anakafrem tu cha laki tatu lakini godown Ana Mali ya millions 300 .tra analipa kodi ya lakin 6 kwa mwaka
 
Kwa Sasa maduka hayo makubwa yaliyopo yanaitwaje.... Japo tukiwa tunapita nje ya hayo maduka tuwe tunnajua.... Haya maduka kwa ajili ya shopping za vigogo😋😂🙊😴
Hayapo hapa Tanzania, ndiyo maana wanaagizia nje...
 
Wateja watapatijana tu, maana nguo za Kariakoo. Kama unapiga hesabu vizuri ni hasara sana na very expensive in long run.

Bora hata ununue shati laki lakini lidumu, kuliko kununua shati 20,000 halafu ukifua mara moja linapauka.
Nafuu nivae branded mtumba original kulikio counterfeit brand ya Kariakoo.
 
Nafuu nivae branded mtumba original kulikio counterfeit brand ya Kariakoo.
Hata mie msimamo wangu ndio huo, ronya za kariakoo zinakera ukifua mara nne tu ishapauka hata pasi haikubali tena
Mitumba ni bora sana ila kupata nguo sahihi lazima na muda uwe nao
 
Back
Top Bottom