Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Huwa nazungumza sana akiba ya pesa za kigeni sababu ni kitu muhimu sana kwa nchi. Nchi inatakiwa kutumia kwa busara sana pesa za kigeni. Hizo ndizo tunaagizia mafuta, madawa, kulipa madeni na mahitaji mengine muhimu. Ukisikia serikali haina pesa ujue hasa inamaanisha haina hizo reserve currencies.
Tukienda kununua umeme nje hatutalipa kwa pesa zetu. Tutalipa kwa reserve currencies tulizopata kwa shida.
Hizi pesa zinapatikana kwa shida sana. Mpaka tuuze maparachichi, korosho, chai, kahawa, pamba, dhahabu na watalii waje ndiyo tuzipate.
Sasa kama tuna umeme humu ndani wa kutosha na ziada kwa nini tutumie akiba ya maana kuagiza umeme nje? Sababu ya mikoa ya kaskazini kuwa mbali na vyanzo vya uzalishaji wa umeme haiingii akilini kabisa. Hii ishu kama ipo in motion tuiangalie upya.