Kwanini TUZO zote za muziki zinazoanzishwa Tanzania zinakufa

Kwanini TUZO zote za muziki zinazoanzishwa Tanzania zinakufa

tuzo ni wadhamini sasa kama wadhamin hawataki? achana na mambo ya tuzo tu hata mashindano kama Bongo Star Search yanakufa miguu juu sababu wahusika hawawezi kujisimamia wenyewe uwezo wa kifedha ni mdogo. alafu kwa jina walilonalo EATV ilipaswa tuzo zao ziwe kubwa kuliko zote africa mashariki na ziwe endelevu. nadhani nextime wataporudi tena waingie mkataba na wadhamini kwa miaka 5 hivi na kuendelea kama wanavyofanya marekani sio mdhamini anadhamini mwaka huu mwaka kesho anapiga-DASH!.

CONCLUSION
AZAM pekee ndo watauweza mchezo huu maana wanajiweza kila kitu. ngoma inaweza kwenda kavu kavu bila mdhamini. [HASHTAG]#DadIsComing[/HASHTAG]
 
ni..wasanii..wenyewe..wanaziua,kutokana..na..wivu..pia..waandaaji..wanakuwa..hawajajipanga,na..hawana..plan..ya..muda..mrefu.
 
Habari wanajamvi...
Bila kupoteza muda nidondoke kwenye mada yangu!!Imekua ni kawaida kuona TUZO zikianzishwa hapa Tanzania lakini hazidumu.Toka Tuzo za kilimanjaro Music Awards zilipopotea tulikaa muda mrefu kidogo bila kuwepo na tuzo hapo kati kati mpaka pale kituo cha EATV kilipoleta zile "EATV Awards" mwaka jana ilikua kama sijakosea!!
Wengi kama si wote tulikuwa tukitegemea kuziona tena TUZO hizo kwa mwaka huu na miaka mingine ijayo huku tukitarajia kuziona zinakua siku hadi siku lakini imekua tofauti na tulivotarajia!!Hakukuwa na matangazo ya kwanini labda zimeahirishwa jambo linalonifanya niseme zimekufa pia(Binafsi kwa upande wangu sikuona matangazo yoyote labda kwa wenzangu).
Ni sifa kwa wasanii wetu kutoka nje na kuleta Tuzo nyumbani lakini pia ni sifa kwa wasanii wa nchi za wenzetu kuja kwetu pia ku-experience kilichopo Tanzania lakini pia kupata ushindani!!
Kinaweza kikaonekana kama kitu kidogo lakini kina manufaa kwa upande mwingine,Nini sababu ya Tuzo zinazoanzishwa Tanzania kuishia njiani,kwa lugha nyingine kwanini hazidumu na kukua!!??
Umesahau vilevile TUZO ZA WATU za Bongo5 nazo zimekufa kifo cha mende
 
Sio kwa Tanzania tu.

Vitu vingi vinavyoanzishwa na Mtu au Watu weusi havidumu asilani.

Hatujui Handling na Management ya programs au projects tunazozianzisha.
 
Mimi nime sikitika kwa kitukua na tuzo za EATV hawa jamaa walikuja vizuri...sijui hawajiani nawanacho fanya

EATV wange fanya marekebisho tu kidogo kwenye nomination baadala ya msanii kupendekeza mwenyewe wangeunda chombo cha kupendekeza wasani washiriki...(waige hata bet na mtv wanavyo fanya sio thambi)
EATV amken acheni kujikita kwenye uteam na beef za kijinga nyie mpo vizuri na mna support kubwa sana.
Hizi tuzo zilionekana kibwego baada ya kuja kuinekana kama nibtuzo zilizoanzishwa kukoleza mabifu ya wasanii coz sikuona utofauti wa tuzo za EATV na zile za ktma kuwa yule mwenye kura nyingi ndo anakuwa mshindi wangeunda jopo la majaji wananchi wakawa na aslimia hata 40 alafu sitini za majaji hiyo inapunguza mihemuko.

Halafu nilikuja kuzidharau baada ya wcb wasafi kukacha kushiriki na wala siyo wao tu maana kuna wasanii kibao walizitosa badala wachukuloe changamoto ikawa beef tena ndo hapo nikaona hizi tuzo zilikuw zimeandaliwa ki team na kukoleza ma beef.
 
Back
Top Bottom