Kwanini uchawi/ulozi/ ushirikina unapigwa marufuku na kuharamishwa katika mpira Tanzania?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Tanzania ni nchi huru kidini na kiimani, kila mtu yuko huru kufanya mambo ya kiimani anayoona yanamfaa,

Sasa kwa nini kwenye mpira wachezaji wakifanya matendo ya ibada ya dini mbili za Ukristo na Uislamu ni sawa lakini wakifanya vitendo vinavyoitwa vya ushirikina, ulozi, uganga, matambiko au uchawi inakuwa sio sawa, shida na kelele nyingi??
 
Tanzania ni nchi huru kidini na kiimani, kila mtu yuko huru kufanya mambo ya kiimani anayoona yanamfaa, sasa kwa nini kwenye mpira wachezaji wakifanya matendo ya ibada ya dini mbili za Ukristo na Uislamu ni sawa lakini wakifanya vitendo vinavyoitwa vya ushirikina, ulozi, uganga, matambiko au uchawi inakuwa shida na kelele nyingi??

Unafiki tu!
 
Kwani kufanya matendo ya kiimani lazima uwe na dini inayotambulika?

Dini ngapi zinatambuliwa Tanzania?

Inaaminika kwamba uchawi unaleta madhara katika jamii, ndo mana hata serikali imetunga sheria ya kupunguza vitendo vya kichawi..!
 
Mbona waganga wa kienyeji wanapewa vibali vya kufanya uganga/uchawi/ushirikina??
 
Hakuna kitu inaitwa ushirikina inaitwa asili mambo ya dini ni asili za wengine
 
Tanzania ni nchi huru kidini na kiimani, kila mtu yuko huru kufanya mambo ya kiimani anayoona yanamfaa, sasa kwa nini kwenye mpira wachezaji wakifanya matendo ya ibada ya dini mbili za Ukristo na Uislamu ni sawa lakini wakifanya vitendo vinavyoitwa vya ushirikina, ulozi, uganga, matambiko au uchawi inakuwa shida na kelele nyingi??
Wanasema nchi haina dini ila wananchi wana dini.
Nembo ya taifa ni ya Adamu na Hawa/Eva, hao bila ya imani au dini tungewajua?
Waafrika babu na bibi zetu waliamini kwenye hiyo mizimu, lakini haikutusaidia na tuliwezwa na kufanywa watumwa na kuwa makoloni ya hawa wenye imani nyingine, sasa kitu kikiwa hakikusaidii kwa nini uking'ang'aniye?
Na mpira ni mchezo unaohitaji uwezo na ujuzi wa kuucheza si hila na mbinu za kurogana ili upate matokeo. Na tatizo hili limezidi toka mpira kuwa ni moja ya chanzo cha mapato makubwa duniani, watu wanafanya lolote ili waweze kupata matokeo ikiwa pamoja na kufanya ulozi.
 
Tanzania ni nchi huru kidini na kiimani, kila mtu yuko huru kufanya mambo ya kiimani anayoona yanamfaa, sasa kwa nini kwenye mpira wachezaji wakifanya matendo ya ibada ya dini mbili za Ukristo na Uislamu ni sawa lakini wakifanya vitendo vinavyoitwa vya ushirikina, ulozi, uganga, matambiko au uchawi inakuwa shida na kelele nyingi??
Ni imani sawa lakini inaendana kinyume na mapenzi ya MUNGU na muda mwingine inavunja sheria za nchi... Na ndio maana serikalini imeukana uchawi kukwepa tuhuma kama hizi.

Ni imani ambayo haina upendo wala hajui haki hivyo siyo ya kutegemea(corrupt system)

Hebu fikilia ili shida/jambo likamilike(lifanikiwe) vinahitajika vitu ambovyo upatikanaji wake lazima uvunje sheria au utende dhambi!

Mfano masharti yake unataka kiungo cha mtu(mkono nyeti kichwa). Ivi viungo unavipataje?
 
Ndio maana huwa tunaambiwa uhuru lazima uwe na mipaka, huo uhuru wa kutaka kudhuru wengine ili wewe ufanikiwe kwa kisingizio kwamba nchi yetu ina uhuru ni upunguani, siku zote unaambiwa fanya unachotaka mradi usidhuru mtu wala usivunje sheria za nchi
 
Sio waganga wote huwa wanataka viungo vya binadamu
 
Ndio maana huwa tunaambiwa uhuru lazima uwe na mipaka, huo uhuru wa kutaka kudhuru wengine ili wewe ufanikiwe kwa kisingizio kwamba nchi yetu ina uhuru ni upunguani, siku zote unaambiwa fanya unachotaka mradi usidhuru mtu wala usivunje sheria za nchi
Mbona kuna wachungaji na masheikh wanadhuru watu kwa utapeli??
 
Imani zote za Kiafrika zinaitwa "ushirikina" basi ukristu na uislamu ni ushirikina. Ni kwa nini ushirikina wa kizungu na kiarabu ukubalike?
 
Sisi ndiyo Simba SC AKA;

1. Makolokolo SC.
2. Mbumbumbu SC.
3. Mipang'ang'a SC.
4. Malalamiko (Lialia) SC.
5. Makelele SC.
6. Madunduka SC.
7. Manyaunyau (mapaka) SC.
8. Mwakarobo SC.
9. Mikia SC.
10. Miso Misonda SC.
11. Manyang'au SC.
12. Mazumbukuku SC.
13. Mazombi SC.
14. Kinyume nyume SC.
15. Ngada SC.
16. Kolowizard SC.
17. Zuwena SC.
18. Bebwabebwa (Mbeleko) SC.
19. Panya roads SC.
20. Kikanuni SC.
21. Kufa Kiume SC.
22. Ubaya ubwege SC.
23. 5imba SC.
24. Visingizio SC (Visababu)
25. Manguruwe SC.
JamiiForums-1769471325.jpeg
 
Tanzania ni nchi huru kidini na kiimani, kila mtu yuko huru kufanya mambo ya kiimani anayoona yanamfaa, sasa kwa nini kwenye mpira wachezaji wakifanya matendo ya ibada ya dini mbili za Ukristo na Uislamu ni sawa lakini wakifanya vitendo vinavyoitwa vya ushirikina, ulozi, uganga, matambiko au uchawi inakuwa shida na kelele nyingi??
Tupe mfano hai nini kilifanyika wakakataza.

Kwani hufahamu kazi za kamati za ufundi?
 
Back
Top Bottom