Urusi alituma maombi kujiunga NATO akakataliwa, NATO si hawasemi wapo dhidi ya nani basi Russia ikawadhihaki kwa kutaka uanachama. Tatizo la Russia huwa ana ego na hujikuta ana mamlaka juu ya majirani. Russia iliitwa na Marekani iwe inashiriki kwenye mazoezi ya pamoja ya majeshi ya Ulaya ikaweka masharti magumu. Mwaka 2003 washirika walipoenda Iraq ikaonekana kuna majeshi yana mafunzo mabovu hasa Ukraine na Poland. Marekani ikaanzisha program ya kufundisha majeshi ya Ulaya yenye changamoto, wakafanya na exchange program kutembelea training facilities, weapons storage sites na mambo ya kijeshi yasiyo ya siri. Kwenye programu hizo Urusi ilikubali ziara za kutembeleana na makamanda wake wakajionea standards za majeshi kadhaa mengine ila haikutaka training ya pamoja, nayo ilitembelewa na wakashauriana vitu kadhaa ambavyo kimojawapo kilitekelezwa ni ujenzi wa training ground mpya ya Mulino. Rheinmetall kampuni ya Ujerumani ndio ilipewa tenda ikaweka NATO standards.
Russia wala hachukiwi, ila the way anaishi na majirani ndio wasiwasi wao. Kuna uwezekano Russia ikaingia mgogoro na Kazakhstan jirani wa Kusini, kuna uwezekano China na Russia warudie kugombania mipaka ila hakuna uwezekanowa Marekani kupigana na Canada.
BRICS sio ushirika wa kijeshi ni wa kiuchumi, kama ambavyo NATO ni wa kijeshi tu. Wala usitarajie South Africa itaziacha Marekani, Ufaransa, UK, Canada eti iende kwa China na Russia.
Na usitarajie Brazil iikumbatie Russia iiache Marekani, kasome ushirikiano wa Brazil kwenye silaha na Westerns companies. Tafuta hata kampuni yao pendwa ya Embraer inapewa hata tenda za silaha na wazungu ila sio Warusi, na ina license kibao za wazungu.
Wala usitarajie India kujiweka kwa Urusi pekee. Tazama weapons sales za tangu Trump anaondoka madarakani mpaka sasa, za Urusi kadhaa zimefutwa na za Marekani zimetekelezwa.
China tu ndio anabaki kwenye BRICS akiwa na uwezo wa kufanya alliance ya kijeshi na Russia. Ila naye kashauriwa asitoe msaada kwa Urusi kwenye vita ya Ukraine akakubali. Russia leo hii anaenda kwa Iran kuomba msaada wa drones wakati China ina drones za kila aina