Hata tabia ya kuosha vyupi kwa maji ya mwisho baada ya kuoga ni tabia ya hovyo. Hapo jambo la msingi andaa maji mengine safi na mengi, ifue hiyo kyupi kwa muda reasonable na sio unapakapaka sabuni na kukamua huo ni zaidi ya uchafu extraordinary.
Halafu watu wajitahidi wasiwe wanavaa vyupi viwili kwa wiki huo ni zaidi ya uhuni na uchafu wa hali ya ajabu, ukichukua harufu ya voo.z(i), jasho la sehemu za siri,misuguano ya nguo na kyupi yaani shombo la hapo ni zaidi ya dampo.
Jambo la msingi kutokana na bei ya vyupi kuwa ndogo jitahidi uwe nazo hata saba unavaa moja moja kila day, sababu ya msingi ni usafi. Soksi na vyupi ni vitu rahisi sana kuvifua kama wewe ni me husije hata siku moja kumtupia mkeo hayo majukumu ,jifunze kuwa msafi wewe mwenyewe.
Jambo la mwisho tujitahidi kuwa wasafi kwakuoga na at least usiwakere wenzio na harufu za mdomo, kyupi soksi, na harufu nyingine nyingi za hovyo hovyo.
©2021