Kwanini ukiwasaidia watu ambao sio ndugu zako unabarikiwa sana ?.

Kwanini ukiwasaidia watu ambao sio ndugu zako unabarikiwa sana ?.

Ukiwasaidia ndugu zako, hilo ni jukumu lako, ukiwasaidia wasio ndugu zako kwako unakuwa umetenda jambo la ziada, lakini hao wasio ndugu zako kama ni maombi kinywani mwao yatatoka pasi na unafiki, kama ni baraka zitatoka pasi na unafiki, lakini watamshukuru Mungu kwa ajili yako hivyo baraka zinakuja automatically.

Kuwasaidia ndugu kama nilivyosema inakuwa ni jukumu lako, lakini pia hao ndugu wataona unawajibika kwao, tena wanaweka kukusema kama umetoa wasivyotarajia, hapawezi kuwa na baraka hapo.

Kumbe kusaidia ndugu ni jukumu 😃
 
Habari .

Mimi ni muumini mkubwa wa kutoa , Ila katika utoaji wangu huwa nikimsaidia mtu ambaye hatuna undugu wowote , baraka huwa zinarudia kwa kiwango kikubwa Sana.

I need to understand kwa wataalamu wa mambo ya kiroho .
Kumpa Ndugu ,unatoa bila moyo kuugulia sababu unahisia za Undugu .

Kumpa MTU wasokua wa Damu yako, inahitaji upendo na huruma za hali ya juu sana, hivo Mungu hubariki sana.


Saidia Masikin, Yatima na wajane wenye uhitaji.
 
Noma sana ... mtu anaamini msaada ni lazima na haki yake ya msingi.
 
Kumpa Ndugu ,unatoa bila moyo kuugulia sababu unahisia za Undugu .

Kumpa MTU wasokua wa Damu yako, inahitaji upendo na huruma za hali ya juu sana, hivo Mungu hubariki sana.


Saidia Masikin, Yatima na wajane wenye uhitaji.
Aisee nimejifunza kitu
 
Mbona sisi tunaosaidia sana watu na wenye mioyo ya kutoa tukiwa nacho ni ngumu sana kwetu kutoboa japo tunapambana sana
 
Binafsi, kusaidia wasiojiweza huwa ni sadaka nzuri sana. Sio wale wa karibu yako Ila watu wenye shida halisi.

Huku kwingine toa kwa moyo mmoja kama unavyofanya kwa sasa Ila usitarajie kwamba nao watajitoa pale utapotetereka. Tena akheri ndugu atakusaidia japo kwa masimango ili kuepuka aibu ya kuonekana walikutelekeza Ila watu baki. Hawajali

Toa kwa moyo ukitaraji kwa Mungu Ila kwa binadamu papuuzie. Ubarikiwe sana mkuu
 
Ni upumbafu sna kutoa wasaidia ndugu zako ni ujinga na ni mwanasheria ubinafsi
 
mimi sio mtaalamu wa kiroho ila nina haki ya kuchangia

hubarikiwi sana bali unahisi hivyo

maneno tunayoyasikia kuhusu ndugu mara nyingi ni mabaya, hii inafanya tuone ndugu kama watu wabaya, tunafanya 'stereotyping'

kwahiyo tunadhani ndugu zetu wana hila, na hata wakikosea kidogo tu, tunakimbilia kuwahukumu, hiyo ni 'group attribution error'

na kupitia huko, tunachagua visa vyote vya ndugu kufanya makosa, mazuri hatuyapi kipaumbele, hiyo ni 'clustering illusion bias'

sasa kwa hali hiyo ukimsaidia mtu baki unaona kama umetumia busara sana kwasababu unadhani ndugu huenda asingekuwa na shukrani...

unajisikia vizuri, hizi kumbukumbu za kusaidia watu baki unakuja kuzihusisha na mafanikio yako kupitia misingi yako ya dini, hii ni 'selective perception'

hizi zote ni cognitive biases, shortcuts ambazo ubongo wa binadamu unapenda kutumia kurahisisha kazi zake nyingi.

kumbuka na wewe ni ndugu wa mtu, hujakamilika, huenda kuna mtu anakuchukulia hivyo hivyo.

tujitahidi kuwachukulia watu kwa upekee wao, tusipende ujumuishaji, ni mbaya.
 
Back
Top Bottom