Kwanini ukoo wako ni masikini?

Kwanini ukoo wako ni masikini?

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Unmaskini unarithishwa?

Unaweza kukomaa bila mafanikio kumbe kuna madesa ya jadi uliyoaminishwa kimyakimya (subliminally) yanakuvuta shati.

Mfano, moja ya ukoo nilioufuatilia

1: Ukiwa tajiri utalogwa hadi uwe kama wenzako

2: Waliofanikiwa kidogo wanastrago kuhakikisha kila mwana ukoo anawategemea wao tu.

3: Baba, Mama, Ukoo mzima unajuhudi kubwa katika kulaani na sio kubariki, kukuza mabaya badala ya mema.

Ukiona ukoo au familia ina hizi mentality piga chini kwa hekima lakini. Ikiwezekana kaa mbali hizo ni tabia za kimasikini. Hama hata mkoa ukaanzishe ukoo na familia mpya maana utaambukizwa.
 
Sisi kwenye ukoo wetu kila mwisho wa mwaka tukienda 'kuhesabiwa' lazima tuulizane kila anaekwama kwenye mambo yake tujadili namna ya kuinuana.

Malengo yetu ni kuona kila mmoja akifanikiwa na kupunguza utegemezi. Tunataka kila mwana ukoo awe financially independent.
 
Si wanasema hizo evil spirits zinaweza kukufuata popote ulipo
Usipokuwepo hutaathiriwa na
Maneno
Kuona
Kugusa

Kwa kutazama tunabadilishwa

Hizo spirit ni nadharia tu, Ukiwa nje ya hiyo belief system hazifanyi kazi. Ndio maana watu wa Bible wanajua Ibrahim alikuwa tajiri baada ya kutoka kwenye uchawi wao huko ur ya wakaldayo.

Spirit za ujingaujinga wa kijadi zilikoswa support ugenini
 
Sisi kwenye ukoo wetu kila mwisho wa mwaka tukienda 'kuhesabiwa' lazima tuulizane kila anaekwama kwenye mambo yake tujadili namna ya kuinuana.

Malengo yetu ni kuona kila mmoja akifanikiwa na kupunguza utegemezi. Tunataka kila mwana ukoo awe financially independent.
Hii ni ya kuigwa asee.
 
Nzuri hii
 
Hio ndio system ya Ujamaa. Tanzania system ya ujamaa ya Nyerere ilitusaidia nini? Ina-sound vizuri ila bado ktk ndugu kuna wavivu wengi. Wale wachapa kazi watanyonywa damu na wavivu. Mwisho mambo ya wote yatafeli kabisa.
 
Ni kweli mkuu...

Lakini nini maana ya kua na pesa mingi huku ndugu zako wanateseka na umasikini...

Huu mfumo wa kusaidiana ni best sana mkuu.
 
ni kweli mkuu...

lakini nini maana ya kua na pesa mingi huku ndugu zako wanateseka na umasikini...

huu mfumo wa kusaidiana ni best sana mkuu.
Ndugu ni wengi sana. Na shida zao haziishi. Na wana wivu sana. Na wanataka uwape msaada hadi ulingane nao. YANI DUNIA YA LEO UKITAKA KUFELI, Kuwa karibu na ndugu kama umefanikiwa. Najua mifano kibao watu waliajiri ndg kwa biashara nzuri zikafa kabisa.

Mimi nilishaacha kusaidia ndugu. Na nilivyoacha ndio mambo yangu yamekuwa yananyooka kweli kweli. Kwanza kufanikiwa nimepambana mwenyewe tu na Mungu wangu. Wao kwani nani aliwazuia wasipambane kama mimi? Yani mimi afadhali nisaidie mjane au mtu mgeni kuliko ndugu. Hao wasio ndugu wana shukrani sana. Ila ndg wanaona ni wajibu wako.
 
Kaukoo ketu nikaajabu sanaa,mwenye nazo wachacheee wanataka muwasujudie...usipo jipendekeza hawakupi ramani wala msaada,ukijiweka mbalii Ni majungu na lawama oooh mtoto wa Fulani anajiskia....Mara anajitenga na wezake,michango hatoi dah hizi Koo nyingine basi ingekiwa naweza ningehamaa ukoo.....laana na kulaaniana ndo usisemeee,kulogana Nako....
 
Hio ndio system ya Ujamaa. Tanzania system ya ujamaa ya Nyerere ilitusaidia nini? Ina-sound vizuri ila bado ktk ndugu kuna wavivu wengi. Wale wachapa kazi watanyonywa damu na wavivu. Mwisho mambo ya wote yatafeli kabisa.
Ujama unapromote ujinga na uvivu unaosukumwa na wivu.

Ila hii ya kukutana kusaidiana na kupeana mbinu sio ujamaa ni akili
 
Kaukoo ketu nikaajabu sanaa,mwenye nazo wachacheee wanataka muwasujudie...usipo jipendekeza hawakupi ramani wala msaada,ukijiweka mbalii Ni majungu na lawama oooh mtoto wa Fulani anajiskia....Mara anajitenga na wezake,michango hatoi dah hizi Koo nyingine basi ingekiwa naweza ningehamaa ukoo.....laana na kulaaniana ndo usisemeee,kulogana Nako....

unaweza kuona wanazo kumbe na wao wako kwenye mateso makali na wanachoweza kukusaidia ni labda 100K za kula na kutatua mkwamo tu wa leo na kesho il kukusaidia kama kukusaidia nawewe ukasonga hawawezi maana walichonacho kinaweza kuwasaidia wao tu....
 
Tatizo la waafrika ni kutegemeana. Yani mtu akipata vihela tu kidogo ukoo mzima unaanza kumkodolea macho.
Hilo ni tatizo kubwa sana kwenye jamii zetu za Kiafrika. Shida inakuja pia kuwa watu huwa hawaangalii long term solutions kwenye haya masuala.

Sawa mtu hali yake ni mbaya na anahitaji kusaidiwa asaidiwe lakini mkae muangalie suluhu ya muda mrefu. Ambapo mnaweza kuchanga hela mkapata mtaji mtu akafanya biashara akajiingizia kipato so next time hatakuwa tegemezi. Lakini ikiwa ni kusubiri mtu apate shida ndio ndugu muanze kuchangia hiyo haifai.

Kuna msemo wa kichina unasema.

"Give a man a fish, and you feed him for a day. Teach a man to fish, and you feed him for a lifetime."

So kumpa mtu msaada wa hela kila siku sio suluhisho bali kumpa mbinu na uwezo wa kutengeneza kipato chake mwenyewe ndio suluhisho la kudumu.

DocJayGroup
 
Kaukoo ketu nikaajabu sanaa,mwenye nazo wachacheee wanataka muwasujudie...usipo jipendekeza hawakupi ramani wala msaada,ukijiweka mbalii Ni majungu na lawama oooh mtoto wa Fulani anajiskia....Mara anajitenga na wezake,michango hatoi dah hizi Koo nyingine basi ingekiwa naweza ningehamaa ukoo.....laana na kulaaniana ndo usisemeee,kulogana Nako....
Mimi ketu nilikapa likizo mwaka ili nipumzike kidogo. Nilianzishiwa msako mkali na Tiss wa ukoo. Wanakata kujua Nimekaa kimya nimetoboa au naungaunga. Walipo pata habari mbaya wakaanza kutangaza kajamaa kamelaaniwa walipopata habari njema wakabadili gia jamaa amejitenga na ukoo, hataki ndugu hahahahaha

Busara na hekima kubwa sana zinahitajika kuvua belief system za kijinga ambazo bado ndio uti wa mgongo wa koo nyingi
 
Kheri uwe broken, kuliko kuwa litajiri la majini yaan una ishi a ndoa ya majini...kuna chalii mmoja yupo Korogwe dogo ana hela ila kila mwezi kunantarehe ikifika dogo anajinyea .(involuntary)

Kuna dogo mwengine yupo kibaha picha ya ndege ..dogo na yy ana mpunga kajenga vijumba vya kupangisha lkn vina masharti kama kambi ya jeshi..mm huwa naviita bijumba vyake kambi ya majini..ktk bijumba ivyo mkristo hupangi nyumbaa wala frame zake, kula kiti moto marufuku, kuuza bia ktk frame zake ni marufuku..

Sasa kwa scenario izo chache hapo ivi huo utajiri utaufurahia kweli ?
 
Back
Top Bottom