Inakuwaje wanajamvi!
Sisi wote watanzania ni wezi katika nafasi zetu husika. Ukiibiwa potezea. Unaenda kujaza mafuta Sheli ukiibiwa unakimbia humu kuanzisha uzi ukilia lia wakati huko ofisini unapiga panga, ama una duka unaibia chenji wateja ama unakwepa kodi halafu ukilizwa unabaki kulia lia.
Ukiibiwa potezea tu kwasababu na huyo aliyekuibia naye atalizwa na mwengine na huyo mwengine pia.
Unakuta mtu anawadhulumu wengine yeye akidhulumiwa anakuwa mbongo na kutaka kuua kwanini usipotezee tu.
Utakuta Wafanyakazi wanaibia kampuni wakicheleweshewa mishahara wanaandamana why?
Unakuta jambazi ama kibaka nalo linaweka fensi na milango na madirisha ya chuma linaogopa kuibiwa.
Ukiibiwa potezea tu kwasababu pia wewe unaiba kwenye nafasi yako. Faraja inakuja anayekuibia naye ataibiwa tu na mwengine.