Kwanini umaarufu wa Januari Makamba unashuka siku hadi siku amekosea wapi?

saidoo25

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
624
Reaction score
1,456
Mwanzoni mwa miaka 2012 hadi 2015 jina la Januari Makamba lilikuwa na mvuto mkubwa kwenye umma hasa mitandaoni na hata wengi tuliamini anafaa kwa nafasi ya Urais kama ambavyo aliingia kwenye mchakato na kufanikiwa kuingia Tano bora.

Nini kimesababisha umaarufu wa Januari Makamba kuporomoka kiasi hicho, nini kilimpandisha na nini kinamshusha sasa.
 
Umetumia kipimo gani tafadhali, au mawazo yako tu?
 
Kipaji chake ni uganga
 
Getrude Mollel jaribu kufanya utafiti mdogo tu ingia kwenye maeneo yote ambayo habari yake inawekwa iwe Facebook, Instagram, Twitter au Youtube alafu soma maoni yanayoandikwa na watanzania alafu rudi hapa unaweza kuja na majibu ya utafiti
Kwa hiyo ndicho kipimo ambacho umetumia hicho? Tanzania wengi hawamo kwenye mitandao ya kijamii. Mcheki Makamba kupitia field, mapokezi na metrics kutoka ground kabisa. Haya mambo ya mitandaoni mostly ni organized movements tu. Usichukuliwe sana na hayo mambo.
 

Kwahio uko kwenye field sio organized movements
 
Unataka awe maarufu Ili iwaje?
 
Hauko sahihi hujafanya tafiti fuatilia mambo yanayolalamikiwa na wananchi kupitia mitandao yanavyoshughulikiwa na Serikali mfano Tozo za Simu na punguzo lilofanywa na Serikali ni kelele za mitandao ambao ndio hao hao wananchi, umesahau tozo zilipitishwa na Bunge na hakuna mbunge aliyepinga zaidi ya wananchi kupitia mitandao ndio wakapaza sauti hadi serikali ikashusha viwango.

Pili fuatia sakata la mishahara umeona linajadiliwa bungeni au kikao chochote zaidi limeanzia mitandaoni na Serikali ikatoa kauli kwa hiyo huwezi kuidharau mitandao ndio inasimama kwa kiasi kikubwa kutetea wananchi.

Na nao unaowaita wa vijijini ndio hao hao wanaosema humu mitandaoni sio kama zamani kwamba mitandao ni kwa ajili ya watu wa mjini tu. Fanya tafiti pitia page za mitandao za TBC, CLOUDS, ITV, mwananchi, na nyinginezo utakubaliana nami
 
Kilichompandisha ni mtandao wa upigaji wakati ule akitumia ile bilioni moja aliyokopa kwa mgongo wa Bumbuli Saccos.

Kwa sasa pia kinachomshusha ni mtandao wa upigaji kupitia mikataba tete na tata anayoiingiza TANESCO nchini.

Kupitia wizara ya Nishati ambayo yeye ni mlamba Asali hapo.

Sasa tunaamini shukurani ya Nyuki ni Moto.
 
1. Utendaji kazi wake hauna tija/matokeo chanya unaoendana na majigambo yake kuwa yeye ni mtu smart upstairs.
2. Ameendekeza kiburi na dharau kwa watu akijua kuwa ana godmother ambaye hawezi kumtumbua hata akiboronga.
 

Ww jamaa January amekukosea nn? Msamehe Tu

We jamaa na January mnagombania mwanamke au ni nn?

Topic zako nyingi ni January Tu duh, unataka afukuzwe au unatakaje, na je akifukuzwa ww unapata faida gani?

Ni wivu tu
 
 

Attachments

  • Screenshot_20220726-103807.png
    146.4 KB · Views: 6
Mmoja wapo ni mm.... Ila jamaa kumbe ni empty set na nafikiri amewekwa nishati kimkakati kikwete nimtu mbadii saana akitaka kukumaliza anajua akuweke wap?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…