Kwanini umaskini na ujinga huenda pamoja?

Kwanini umaskini na ujinga huenda pamoja?

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Wakati ambapo unawaza namna gani ujikwamue kutoka kwenye umaskini; kuna mwingine anawaza namna gani azidi kukukandamiza kutokana na umaskini wako!

Hoja ya maskini mara nyingi huonekana kama ni malalamiko yasiyo na maana. Na hutafutiwa majibu ili kudhoofisha hoja hizo.

Maskini (iwe ni mtu binafsi au nchi) akisema jambo fulani suluhisho lake ni hili au lile, ni vigumu kuaminika. (Rejea kwa mfano matumizi ya miti shamba kutibu covid)

Maskini akisema maisha ni magumu, ataambiwa aache kulalamika, atafute hela!
Maskini na tajiri wakitoa hoja:
tajiri atapewa kipaumbele zaidi kuliko maskini.


Kwanini umaskini huchukuliwa kama kukosa maarifa (ujinga)?
 
We umetembea nchi zipi wanaochukulia hizo Nadharia ?

Kama ni Tanzania hiyo ni kweli maana Watanzania ni nchi iliyojaa wajinga 90% Kuanzia Viongozi Hadi raia wa kawaida.
 
Maadui wakubwa wa nchii hii ni UJINGA, Magonjwa na umasiki.
(Mwalimu J.K Nyerere)

NA TOZO!!!!
 
We umetembea nchi zipi wanaochukulia hizo Nadharia ?

Kama Ni Tz hiyo Ni kweli maana watz Ni nchi iliyojaa wajinga 90% Kuanzia Viongozi Hadi raia wa kawaida.
Si tu kwa watanzania wao kwa wao, bali hata mataifa yaliyoendelea kwa yale yanayoendelea (developed vs developing countries)

Kwa mfano Tanzania na America wakipendekeza suluhisho la jambo fulani, ni rahisi America kuaminika kuliko Tanzania. Hata kama jambo hilo lina madhara.
 
Maadui wakubwa wa nchii hii ni UJINGA, Magonjwa na umasiki.

(Mwalimu J.K Nyerere)
Nadhani ujinga ndio chanzo cha hayo mengine yote!

Mtu mzima na elimu yake, haoni suluhisho la matatizo ya kiuchumi kwa taifa zaidi kukusanya tozo za miamala!

Wanaona ni heri kufanya ziara na kuagiza magari mapya badala ya kujenga viwanda! Wanakosa usingizi ili kutafuta mbinu za kubana wananchi kwa kuweka tozo kila mahali! Wanashindwa kudhibiti mfumuko wa bei kwa kisingizio cha vita.

Ama kweli umaskini na ujinga huenda sambamba
 
Si tu kwa watanzania wao kwa wao, bali hata mataifa yaliyoendelea kwa yale yanayoendelea (developed vs developing countries)....
Swali ni kwamba, wewe ukipendekeza suluhisho la issue fulani, what's your contribution? Yaani pale home mmeenda likizo familia nzima, kuna project inatakiwa ifanywe na nyie watoto wa baba,

una mawazo mazuri lakini huna msaada wowote financially, hutasikilizwa, atasikilizwa mwenye kutoa suluhu ya pesa..hata 🇺🇸 vs 🇹🇿 ni the same. Kwenye UN general assembly wewe usikilizwe kama nani wakati kwanza ni ombaomba, kila siku misaada na mikopo tu.

Tujikwamue kwanza kiuchumi then nguvu zingine zitakuja tu.
 
Umasikini huleta njaa Sasa jiulize toka lini mtu mwenye njaa akafanya upembuzi yakinifu wa fikra zake mwenyewe naza viongozi zaidi ya kufikili kushibisha tumbo tu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom