Kwanini Unaamini Mungu yupo?

Toa ushahidi kwamba Bible ni kitabu cha Mungu........acha porojo mkuu.
Porojo ndio nini?ushahidi gani unaoutaka, tukupeleke mbinguni tukuoneshe Mungu huyu hapa ndo uamini. Mbona unakua hutumii akili zako vizuri! Ni bora uamini yupo hata usipomkuta hautapata shida, kuliko kuamini hayupo halafu umkute ndo utajua kilio cha kusaga meno kikoje
 
na wewe unauhakika gani kuwa havikuumbwa na Mungu, ipo siku nayo ni moja tutatoa hesabu, endelea kupotosha
Kwahiyo kila jambo linalokosa majibu ina maanisha Mungu ndiye aliyetenda?
 
Hata kama Mungu yupo, atawapenda zaidi wale wasiomwamini kwa moyo wa dhati kuliko wanaomwamini kwa mashaka mashaka.

Ndiyo maana nasema Mungu hayupo.
 
Kila MTU huvutia kwake kua dini take ni bora kuliko ya mwenzie ni bora kuamini kua Mungu yupo hio inatosha
 
"ni bora uamini yupo hata usipomkuta hautapata shida"
Hichi ndicho mnachofundishwa..?
kwa huo usemi tu huoni kama unatatanisha uwepo wa huyo mungu! okay haya kama mnaamini yupo na umesema kama ukiamini yupo hautapata shida na hao watakaotenda dhambi na wanaamini je hawatapata shida ya kutupwa motoni..?
 
Hata kama Mungu yupo, atawapenda zaidi wale wasiomwamini kwa moyo wa dhati kuliko wanaomwamini kwa mashaka mashaka.

Ndiyo maana nasema Mungu hayupo.
Sikushangai maana wewe unasema Mungu hayupo, kwani we ukisema ukweli utabadilika?,au ukweli utakuwa uwongo? Neno lako wewe haliwezi kubadili chochote mkuu, na wala imani yako kwa Mungu hata sio kikwazo kwa wanaomwamini Mungu, zaidi nakushangaa kwa jinsi ulivyopotoka na bado unadhihirisha upotofu na upofu wako!!
 
Km kitu ukijui haimaanishi akipo...
 
Naomba nikuulize, kama unaamini hayupo, je ukimkuta yupo utachukua uamuzi gani au utajisikiaje?
 
Mungu ameandika mimi nipo ambae nipo.
Biblia inasema Mungu ni roho.

Wewe unaangalia ndege , wanyama, wadudu unasema Mungu hayupo?

Labda nikuulize ulimwengu huu umetokeaje?
Ungeanza wewe kujibu Mungu ametokeaje?
 
kweli sayansi unaweza isijue uwepo wa sayari, nyota nk..
lkn pia ww unae amini Mungu yupo mbona hujiulizi chanzo chake?
 
Kwanini unaamin uwepo wa upepo umeshawahi kuuona??
Kwanini unaamini uwepo wa kujaa na kupwaa kwa maji ya bahari
Kwnn unaamin kua ipo siku utafufuka na ulipwe kwa ulilolitenda duniani?? Nani atakuhukumu kama sio mungu??
sijaona upepo, ila naona effect za upepo.
 
Hizo ndizo sababu za kuthibitisha mungu yupo?
 
Walevi wa Bible na Quran haya maswali hawana hata mda wa kuyafikilia..!

Wao wanachowaza ni pepo zisizoelezeka kwa uzuri wake!!
 
Watu wa Allah na Jehova/Elii wao huwa wanadai Mungu yupo kwa asilimia 100.
 
1. kwa sababu wazazi walinibatiza huko.
2. ndio ningebadili baada ya kujua ukweli.
3. hapana Mungu yupo kwa dini zote
4. Naamini kuna Mungu kwa sababu ya mpangilio wa mambo ulivyo lazima kuna nguvu ya ziada iliwezesha mpangilio huu kwa mfano mwili wako tu unavyofanya kazi, cell za mwili wako zifanyavyo kazi na kuwasiliana ni lazima kuna organising body.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…