Kwanini Unaamini Mungu yupo?

Kwanini Unaamini Mungu yupo?

Kwani matrilion wakiamini uwepo wake ndio inafanya awepo?? Usipende kuwa unafata mkumbo katika maisha
dbf246951cc873dc41c45df7b26bd695.jpg
 
Mungu alishampa mtu demokrasia kwa hiyo anachugua kile anachoona kwake ndo sa hihi mungu yupo na cha kukudhibitishia kwamba mungu yupo ni uko kuwa na Mwisho iko siku Mwisho wako utafika kungekuwa hakuna aliyekufanya ukawepo ungeishi milele hapa duniani firauni alijiita mungu kabisa yuko wapi sasa hapa duniani

Sent from my TECNO R7 using JamiiForums mobile app
 
Mungu yupo kwa ushahidi huu wakimazingira uwepo wa mbingu na ardhi, usiku na mchana, mke na mume, majini na nnchi kavu, wanyama na mimea, ndege na wadudu, wanaadam na majini. Ushahid Surat n'nabai (78:8) m/mungu anasema "na nimekuumbeni kwa jozi" hakika ni ushahidi tosha kuwa sote tumetoka kwa Allah. Kuhusu yy kama tunataka kumjua zaid, Surat Al-iqlas sura ya 112 m/mungu anasema "yy ni wapekee, yy ndio mkusudiwa, hakuzaa wala hakuzaliwa, wala hana mfanoe", kumbuka Qur'an an ni ujalizo wa Taurat, Zaburi na Injili vyote ni vitabu vya mungu vilivyo teremshwa kwa mitume wake Daud, Mussa, Issa, a.s na mtume Muhammad s.a.w iwe muongozo kwa wanaadam huwez letwa duniani bila muongozo, kama unapo nunua gari au chombo chochote cha electronic utapewa muongozo vip utumie so Allah ndio katuletea hii miongozo hata ukipinga mungu hayupo utashindwa pinga maut basi kubali mungu yupo na kuna maisha baada ya maut wabilah tawfiq m/mungu mjuzi zaid.
Unaamn vipi hayo maandiko kuthibitisha uwepo wa Mungu?je hayawezi kuwa ni utashi wa binadam tu?

sent from kitochi using jamii forum
 
MUNGU YUPO ILA KUNA WATU wameamua kujiita nao mungu

Dai lile lile alilolisisitiza Shetani
katika nyika ile ya majaribu bado linasisitizwa naye [papa] kupitia katika Kanisa la
Roma, na idadi kubwa sana ya watu wako tayari kumsujudu yeye.

“Tunashikilia hapa duniani
mahali paMungu Mwenyezi."
Papa Leo wa 13,
Katika Barua yake ya Utume,
Juni 20, 1894.

YHWH IS GOOD
 
!!!!!
hivi kwamfano binadamu akituma chombo anga za mbali sana hlf asiweke kitu chochote kitakachotambulisha kuwa hicho kifaa kimetengenezwa na binadamu kwa bahati nzuri au mbaya kifaa hicho kikashikwa na viumbe wengine huko anga za mbali je,hao viumbe watajua kuwa kifaa hicho kimetengenezwa na binadamu..?
Mkuu

Kwanini umesema hivyo...
Comment yako nimeipenda,ila nawaza unalenga nini..ngoja nijaribu kukujibu

Hao viumbe watakaokipokea hicho kifaaa,watasema kuna designer wa hicho...labda binadam au la..yaani hawawezi sema kimejiunda chenyewe

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
 
Kitabu cha Bibilia kimejaa kila aina ya uovu unaojulikana.Kinajipinga chenyewe wala hakina mantiki kwenye kuandikwa kwake.Hivyo hakifai kutumika kama ushahidi juu ya uwepo wa Mungu.
Je una ushahidi gani kwamba Bibilia ni kitabu cha Mungu?
Mkuu ni kweli hapa tusitumie biblia kama proving tool..
.but unaposema biblia inajipinga yenyewe,cijakuelewa,,unamaanisha nini mkuu?

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
 
Mantiki inakueleza Mungu yupo....

Labda tatizo lipo kwenye kutafakari tu na kufikiri.Mungu na dini ni vitu visivyohusiana moja kwa moja....
Mkuu eiyer

Tuweke wazi hapa mantiki hiyo,binafsi itanisaidia

Shukran

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
 
"ni bora uamini yupo hata usipomkuta hautapata shida"
Hichi ndicho mnachofundishwa..?
kwa huo usemi tu huoni kama unatatanisha uwepo wa huyo mungu! okay haya kama mnaamini yupo na umesema kama ukiamini yupo hautapata shida na hao watakaotenda dhambi na wanaamini je hawatapata shida ya kutupwa motoni..?
Si dini zote zinaamini kuwa moto upo,,,

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
 
Mimi binafsi nilikuwa mkristo nikabadili dini mkuu kwa sababu nyingi tu za kiimani
Mkuu,
Tuambie ili tufaidike nasisi,kwanini ulibadili dini???na huko kumekuwa nafuu vipi??

Natanguliza shukrani

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
 
Assumptions za wengi zinadisplay that you are thinking of the wrong god. Tatizo tunataka kum-fit Mungu katika mazingira ambayo tunayoishi sisi.

Kwa mfano wengine wanauliza kama Dunia iliumbwa na Mungu, basi Mungu alitokea lini? Jambo la kwanza la kutambua ni kwamba Mungu wa biblia hadhuriwi na muda (time), nafasi (space) wala maada (matter).

Kama anakuwa affected na time, space and matter huyo sio Mungu! Ninaomba kuanzia mbali kidogo;

1. 1. Time, space and matter inaitwa continuum (all of them has to come into existence at the same instance) vinategemeana. Sababu kama kuna matter but no space, WHERE would you put it? Kama kuna space and matter but no time, WHEN would you put it? Hauwezi kuwa na time, space or matter independently, they have to come into existence simultaneously.

2. 2. Sasa basi, Biblia inajibu haya maswali kwa maneno kumi; In the beginning (TIME), God created the heavens (SPACE) and the earth (MATTER).

3. 3. Sasa kuna time, space and matter, created a trinity of trinities: Time is PAST-PRESENT-FUTURE, Space has LENGTH-WIDTH-HEIGHT, Matter has SOLID-LIQUID-GAS.

4. 4. So tuna trinity of trinities created instantaneously, and the God who created them has to be OUTSIDE of them. IF HE IS LIMITED BY TIME HE IS NOT GOD!

Mtu aliye create hiyo device yako (simu au computer) hayupo ndani ya computer running around in there changing the screen. Likewise, the God who created the universe is outside the universe, He is above it, beyond it, in it, through it, He is unaffected by it!
Your questions assume a limited God na hapo ndio kuna tatizo, kama ningeweza kumuelewa Mungu kwa ubongo wangu asingestahili Ibada yangu!
When we try to fit God in the context of this universe (designed by Him) tunakua tunakosea mno! Ku-question the existence of God, metaphorically speaking, ni kama numbers za kwenye computer yako zikaanza ku argue kwamba hazijawa created au hakuna intelligent designer kwa sababu tu hazimuoni ndani.
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Mkuu
Napenda niwe open...
1.umeniimarisha kiimani ,,laiti viongozi wa dini au waaumini wa dini zetu,wangekuwa hivi,wangeleta angalau facts hizi,watu wangeendelea sana

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
 
Kama hayupo jaribu kujifanya wewe ndiye yeye

Sent from my TECNO-C7 using JamiiForums mobile app
 
Assumptions za wengi zinadisplay that you are thinking of the wrong god. Tatizo tunataka kum-fit Mungu katika mazingira ambayo tunayoishi sisi.

Kwa mfano wengine wanauliza kama Dunia iliumbwa na Mungu, basi Mungu alitokea lini? Jambo la kwanza la kutambua ni kwamba Mungu wa biblia hadhuriwi na muda (time), nafasi (space) wala maada (matter).

Kama anakuwa affected na time, space and matter huyo sio Mungu! Ninaomba kuanzia mbali kidogo;

1. 1. Time, space and matter inaitwa continuum (all of them has to come into existence at the same instance) vinategemeana. Sababu kama kuna matter but no space, WHERE would you put it? Kama kuna space and matter but no time, WHEN would you put it? Hauwezi kuwa na time, space or matter independently, they have to come into existence simultaneously.

2. 2. Sasa basi, Biblia inajibu haya maswali kwa maneno kumi; In the beginning (TIME), God created the heavens (SPACE) and the earth (MATTER).

3. 3. Sasa kuna time, space and matter, created a trinity of trinities: Time is PAST-PRESENT-FUTURE, Space has LENGTH-WIDTH-HEIGHT, Matter has SOLID-LIQUID-GAS.

4. 4. So tuna trinity of trinities created instantaneously, and the God who created them has to be OUTSIDE of them. IF HE IS LIMITED BY TIME HE IS NOT GOD!

Mtu aliye create hiyo device yako (simu au computer) hayupo ndani ya computer running around in there changing the screen. Likewise, the God who created the universe is outside the universe, He is above it, beyond it, in it, through it, He is unaffected by it!
Your questions assume a limited God na hapo ndio kuna tatizo, kama ningeweza kumuelewa Mungu kwa ubongo wangu asingestahili Ibada yangu!
When we try to fit God in the context of this universe (designed by Him) tunakua tunakosea mno! Ku-question the existence of God, metaphorically speaking, ni kama numbers za kwenye computer yako zikaanza ku argue kwamba hazijawa created au hakuna intelligent designer kwa sababu tu hazimuoni ndani.
Good Comment.[emoji106]

Kwanza nampongeza mleta mada. ameiwasilisha vizuri mada hii,
hajaihitimisha mwenyewe na amewaachia wachangiaji kuichambua.
Sisi binadamu tumejiona tu tupo, hatujui nani alituweka duniani, ambaye kwanza ametuumba na kutupa viungo vya kutuwezesha kutusaidia ktk shughuri za kila siku,
kama mikono, miguu,
macho nk
Pia tumewekwa kwenye mazingira ambayo yana vitu vya kutuwezesha kuishi kama hewa, chakula na maji.
Katika kujitafakari kwanini tupo, ikabidi tutafute vielelezo vinavyobainisha chanzo cha uwepo wetu, ndipo tukakutana na vitabu vya dini mbalimbali.
Hapo kila jamii ikawa na kitabu chake wanacho kiamini kuwa kina historia ya kweli ya chanzo cha binadamu na majukumu yake.
Vitabu hivyo vyote vinakiri na kuthibitisha kuwa kuna Mtawala Mkuu aitwaye Mungu ndiye aliyemwumba mwanadamu.
Akamweka duniani na kumpa majukumu ya kifanya, amri za kufuata na mwisho ni tendo la kumwabudu yeye peke yake.

Huo ni ushahidi wa kiimani.

Wanasayansi nao wakaja na Nadharia mbalimbali ya chazo cha mwanadamu na ulimwengu kwa ujumla, lakini nadharia hizo zimeshindwa kuthibitisha kuwa ulimwengu ulitokea kwa nguvu ya asili tu kama ya Evolution.
Kwa mfano
Wanasayansi hadi leo wameshindwa kututhibitishia ni kwanini dunia na sayari zake zinaelea bila kushikiriwa na mhimili wowote.
Majibu ya kuwa dunia inashikiriwa na (Force of Gravity) hayana mashiko kwani hawaelezi hiyo Gravity imejengwa katika msingi gani yaani yenyewe inashikiriwa na nini.
Kutokana na sayansi kushindwa kitoa ushahidi wenye kuaminika ndipo ushahidi wa vitabu vya imani (dini) unapoonekana unamashiko.
Vitabu vya imani vinaelezea chanzo cha kila kiumbe na hatima yake baadae.
Sayansi haisemi binadamu akifa anaenda wapi.

Nadharia za kihistoria zinaeleza tu kuwa binadamu alianza kama chembe hai, kiumbe, kiumbe kama sokwe, mtu asiyejitambua hadi binadamu kamili.
Chanzo cha hiyo chembe hai hakielezwi.
Ushahidi wa vitabu vya dini ndio unaoaminiwa na watu wengi kuhusu chanzo cha ulimwengu na binadamu kwa ujumla.
Mfano mmoja tunaona kuwa hata sheria zetu zinazotuongoza leo zimetoka kwenye sheria za Torati ambazo Mungu aliwapa wanadamu wazifuate, sheria hizo zimethibitishwa na wasomi kuwa ndizo sheria za kale zaidi ambazo ndizo chanzo cha sheria zote za sasa hivi.
Totati ndiyo iliyoanza kuelekeza taratibu za mahusiano ya wanadamu kama, ujirani, ndoa, ibada, magonjwa na matibabu, vitu haramu na najisi, hukumu, vita, uchawi na urozi, chakula, vinywaji, vileo, dhambi nk.
Miongozo hiyo ilitolewa kwa watu walioishi mashariki ya kati, jamii ambayo inaaminika kuwa iliyoanza
kustaarabika.
Inamaana ndiyo jamii iliyoanza kuishi maisha ya ustaarabu na maendeleo haya ya leo kwakuwa ilifuata miongozo ya Mungu.
Na ndio jamii iliyoanza kuhifadhi kumbukumbu zake kimaandishi.
Amri kumi za Musa ziliandikwa na Mungu mwenyewe.
Hadi leo bado wasomi wanavumbua maarifa mbalimbali mapya yaliyojificha kwenya ulimwengu.
Hapa inaonekena wazi kuwa bado hatujafikia upeo wa mwisho wa kuelewa mambo ya dunia hii.
Kama ndivyo hivyo tunawezaje kumwelewa Mungu kikamilifu basi
hadi leo hii tumeshindwa kugundua dawa ya kutibu Ukimwi, je tutaweza kumtafiti na kuhitimisha ushahidi wa uwepo wake kwa juhudi zetu binafsi ?
Hapa ili kumwelewa Mungu ni lazima Mungu mwenyewa aje kujitambulisha kwetu na tumwone, tumsikie na ikiwezekana tumguse ndipo tuamini.
Binadamu tuna milango Sita ya kutambua maarifa yaani kwa, kuona, kusikia,kunusa, kugusa, kuonja na kuhisi, (ndoto) (maono) (hayaaminiki kisayansi)
Ili tuthibitishe uwepo wa Mungu inabidi Mungu aje katika umbo la kuonekana, au kunusika, au kusikika, au kugusika au kuonjeka.
Hiyo ndiyo milango ya ufahamu wetu ilipoishia, ndo maana tuna soma Mungu alimtokea Musa kwa ishara ya kijinga cha moto ili aweze kumwona kwa macho na aguse hicho kijinga na kuhisi joto na aungue kidogo na asikie sauti yake ili
athibitishe.
Kama Mungu hajitokezi kwetu kwa namna ya kuhisiwa na milango yetu ya ufahamu ambayo iko limited hakika hatutaweza kumthibitisha kama yupo.
Inabidi tu tuwaamini Wahenga wetu akina Ibrahimu,Musa, Sulemani, Daudi, Yesu Kristo,
Muhamadi nk, ambao wametuthitishia kuwa waliwahi kumwona, na kumsikia, alipojitokeza kwao kwa ishara ya kuonekana na kusikika.

Poleni kwa kuwachosha
 
Kuna nyakati mambo kadhaa hunijia ya kimaisha na ninayakosea majibu wala utatuzi na kubaki nikisubili lolote litokee,ila basi..kabla halijatokea hilo lolote nashangaa napata utatuzi usiokua wa uwezo wangu wala akili yangu,ni kama nimesaidiwa na nisichokiona hivi.hii inamaanisha JAH amenipa msaada.isipokua kumthibitisha siwezi coz sijawahi kumuona kwa macho wala kusikia sauti akinisemesha ila naamini tu.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
 
Kwanza jiulize wewe mwenyewe umetokea wapi! Nayo ni alama ya uwepo wake

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom