Assumptions za wengi zinadisplay that you are thinking of the wrong god. Tatizo tunataka kum-fit Mungu katika mazingira ambayo tunayoishi sisi.
Kwa mfano wengine wanauliza kama Dunia iliumbwa na Mungu, basi Mungu alitokea lini? Jambo la kwanza la kutambua ni kwamba Mungu wa biblia hadhuriwi na muda (time), nafasi (space) wala maada (matter).
Kama anakuwa affected na time, space and matter huyo sio Mungu! Ninaomba kuanzia mbali kidogo;
1. 1. Time, space and matter inaitwa continuum (all of them has to come into existence at the same instance) vinategemeana. Sababu kama kuna matter but no space, WHERE would you put it? Kama kuna space and matter but no time, WHEN would you put it? Hauwezi kuwa na time, space or matter independently, they have to come into existence simultaneously.
2. 2. Sasa basi, Biblia inajibu haya maswali kwa maneno kumi; In the beginning (TIME), God created the heavens (SPACE) and the earth (MATTER).
3. 3. Sasa kuna time, space and matter, created a trinity of trinities: Time is PAST-PRESENT-FUTURE, Space has LENGTH-WIDTH-HEIGHT, Matter has SOLID-LIQUID-GAS.
4. 4. So tuna trinity of trinities created instantaneously, and the God who created them has to be OUTSIDE of them. IF HE IS LIMITED BY TIME HE IS NOT GOD!
Mtu aliye create hiyo device yako (simu au computer) hayupo ndani ya computer running around in there changing the screen. Likewise, the God who created the universe is outside the universe, He is above it, beyond it, in it, through it, He is unaffected by it!
Your questions assume a limited God na hapo ndio kuna tatizo, kama ningeweza kumuelewa Mungu kwa ubongo wangu asingestahili Ibada yangu!
When we try to fit God in the context of this universe (designed by Him) tunakua tunakosea mno! Ku-question the existence of God, metaphorically speaking, ni kama numbers za kwenye computer yako zikaanza ku argue kwamba hazijawa created au hakuna intelligent designer kwa sababu tu hazimuoni ndani.
Good Comment.[emoji106]
Kwanza nampongeza mleta mada. ameiwasilisha vizuri mada hii,
hajaihitimisha mwenyewe na amewaachia wachangiaji kuichambua.
Sisi binadamu tumejiona tu tupo, hatujui nani alituweka duniani, ambaye kwanza ametuumba na kutupa viungo vya kutuwezesha kutusaidia ktk shughuri za kila siku,
kama mikono, miguu,
macho nk
Pia tumewekwa kwenye mazingira ambayo yana vitu vya kutuwezesha kuishi kama hewa, chakula na maji.
Katika kujitafakari kwanini tupo, ikabidi tutafute vielelezo vinavyobainisha chanzo cha uwepo wetu, ndipo tukakutana na vitabu vya dini mbalimbali.
Hapo kila jamii ikawa na kitabu chake wanacho kiamini kuwa kina historia ya kweli ya chanzo cha binadamu na majukumu yake.
Vitabu hivyo vyote vinakiri na kuthibitisha kuwa kuna Mtawala Mkuu aitwaye Mungu ndiye aliyemwumba mwanadamu.
Akamweka duniani na kumpa majukumu ya kifanya, amri za kufuata na mwisho ni tendo la kumwabudu yeye peke yake.
Huo ni ushahidi wa kiimani.
Wanasayansi nao wakaja na Nadharia mbalimbali ya chazo cha mwanadamu na ulimwengu kwa ujumla, lakini nadharia hizo zimeshindwa kuthibitisha kuwa ulimwengu ulitokea kwa nguvu ya asili tu kama ya Evolution.
Kwa mfano
Wanasayansi hadi leo wameshindwa kututhibitishia ni kwanini dunia na sayari zake zinaelea bila kushikiriwa na mhimili wowote.
Majibu ya kuwa dunia inashikiriwa na (Force of Gravity) hayana mashiko kwani hawaelezi hiyo Gravity imejengwa katika msingi gani yaani yenyewe inashikiriwa na nini.
Kutokana na sayansi kushindwa kitoa ushahidi wenye kuaminika ndipo ushahidi wa vitabu vya imani (dini) unapoonekana unamashiko.
Vitabu vya imani vinaelezea chanzo cha kila kiumbe na hatima yake baadae.
Sayansi haisemi binadamu akifa anaenda wapi.
Nadharia za kihistoria zinaeleza tu kuwa binadamu alianza kama chembe hai, kiumbe, kiumbe kama sokwe, mtu asiyejitambua hadi binadamu kamili.
Chanzo cha hiyo chembe hai hakielezwi.
Ushahidi wa vitabu vya dini ndio unaoaminiwa na watu wengi kuhusu chanzo cha ulimwengu na binadamu kwa ujumla.
Mfano mmoja tunaona kuwa hata sheria zetu zinazotuongoza leo zimetoka kwenye sheria za Torati ambazo Mungu aliwapa wanadamu wazifuate, sheria hizo zimethibitishwa na wasomi kuwa ndizo sheria za kale zaidi ambazo ndizo chanzo cha sheria zote za sasa hivi.
Totati ndiyo iliyoanza kuelekeza taratibu za mahusiano ya wanadamu kama, ujirani, ndoa, ibada, magonjwa na matibabu, vitu haramu na najisi, hukumu, vita, uchawi na urozi, chakula, vinywaji, vileo, dhambi nk.
Miongozo hiyo ilitolewa kwa watu walioishi mashariki ya kati, jamii ambayo inaaminika kuwa iliyoanza
kustaarabika.
Inamaana ndiyo jamii iliyoanza kuishi maisha ya ustaarabu na maendeleo haya ya leo kwakuwa ilifuata miongozo ya Mungu.
Na ndio jamii iliyoanza kuhifadhi kumbukumbu zake kimaandishi.
Amri kumi za Musa ziliandikwa na Mungu mwenyewe.
Hadi leo bado wasomi wanavumbua maarifa mbalimbali mapya yaliyojificha kwenya ulimwengu.
Hapa inaonekena wazi kuwa bado hatujafikia upeo wa mwisho wa kuelewa mambo ya dunia hii.
Kama ndivyo hivyo tunawezaje kumwelewa Mungu kikamilifu basi
hadi leo hii tumeshindwa kugundua dawa ya kutibu Ukimwi, je tutaweza kumtafiti na kuhitimisha ushahidi wa uwepo wake kwa juhudi zetu binafsi ?
Hapa ili kumwelewa Mungu ni lazima Mungu mwenyewa aje kujitambulisha kwetu na tumwone, tumsikie na ikiwezekana tumguse ndipo tuamini.
Binadamu tuna milango Sita ya kutambua maarifa yaani kwa, kuona, kusikia,kunusa, kugusa, kuonja na kuhisi, (ndoto) (maono) (hayaaminiki kisayansi)
Ili tuthibitishe uwepo wa Mungu inabidi Mungu aje katika umbo la kuonekana, au kunusika, au kusikika, au kugusika au kuonjeka.
Hiyo ndiyo milango ya ufahamu wetu ilipoishia, ndo maana tuna soma Mungu alimtokea Musa kwa ishara ya kijinga cha moto ili aweze kumwona kwa macho na aguse hicho kijinga na kuhisi joto na aungue kidogo na asikie sauti yake ili
athibitishe.
Kama Mungu hajitokezi kwetu kwa namna ya kuhisiwa na milango yetu ya ufahamu ambayo iko limited hakika hatutaweza kumthibitisha kama yupo.
Inabidi tu tuwaamini Wahenga wetu akina Ibrahimu,Musa, Sulemani, Daudi, Yesu Kristo,
Muhamadi nk, ambao wametuthitishia kuwa waliwahi kumwona, na kumsikia, alipojitokeza kwao kwa ishara ya kuonekana na kusikika.
Poleni kwa kuwachosha