SOMA
Ushauri Bora.
Unapoenda dukani kununua kitu chochote lazima uulize manual ya bidhaa hiyo ili ujue imetengenezwaje, inatumikaje, inatunzwaje nk.
Hata unapoenda kinunua mbegu ya mmea, kama una ka busara kidogo ni lazima uulizie manual ya hiyo mbegu ili uiamini na kuinunua.
Swali kwa nyie wenye busara
Je umewahi kuiulizia manual yako wewe binafsi ?
Kama hujawahi je zile bidhaa za dukani ni bora kupita wewe ?
Kama sivyo basi wewe utakuwa ni (ashakum sio matusi) mpumbavu sana, kwani unaulizia manual ya redio kaseti na unadharau kuulizia manual yako.
Ewe mwenye busara
Umeshawahi kuiona manual yako ?
Kama hujawahi nakuomba chonde chote anza kuitafuta nina uhakika utaipata, kama manual ya kiberiti inapatikana basi na yako ipo.
Ewe mwenye busara,
Itafute kwanza manual yako inayokuelezea wewe umetengenezwa na kampuni gani, umetengenezwaje (umbo lako), unadumu miaka mingapi, unahalibiwa na nini, unatumikaje nk.
Kama huijui manual yako mwenyewe vipi uiulizie manual ya Mungu ?
Ewe mwenye busara,
kama huijui manual inayokuelezea wewe binafsi basi usiisumbukie ya Mungu ambaye hujawahi kumwona.
Ewe mwenye busara,
ni jambo la ajabu kama vitu dhaifu vina manual, lakini wewe mwenye nguvu na hekima huna manual inayoeleza ASILI na HATIMA yako.
Ewe mwenye busara,
Kama hujawahi kuiona na kuisoma manual yako.
Ni upumbavu uliopindukia kama utajidai eti unaiulizia manua ya Mungu.
(ashakum sio matusi ila ni kuelimishana tu)
Uwe mwenye busara, kuanzia leo jiite mjinga ili uaze kuiulizia manual yako na kujisoma mwenyewe na kujitambua.
Mimi nina busara na ninaijua manual yangu.
BIBLIA TAKATIFU ni manual yangu.
Inaeleza wazi jinsi nilivyotengenezwa, chakua nitakacho kula, masharti nitakayozingatia ili niishi vizuri, umri wa miaka nitakayo ishi, miiko na makatazo ninayopaswa kuyakwepa kufanya, nitakavyo owa mke na kuzaa watoto, nitakavyozeeka, nitakavyo kufa, nitakavyofufuka, nitakavyo enda mbinguni, na huko nitaishi milele nk.
Ewe mwenye busara,
Nani alikuruhusu ule chakula unachokula, maji unayokunywa, mavazi unayovaa, miaka unayoishi, dawa unazokunywa nk ?
Hatima yako ninini baada ya kuzeeka ?
Ivi kifo ndio mwisho wako na busara zako zote hizo ?
Ha..ha...ha..ha...
Niambie Ewe mwenye busara,
Kama huijui manual yako utaijuaje manual ya Mungu ?
Ewe mwenye busara,
Kumbe inaoneka wewe ni mpumbavu uliyepindukia.
Hata mwenyewe hujijui kumbe..!
Usikate tamaa anza kuitafuta manual yako kwanza, muda bado upo, nakuhakikishia utaiona.
Ewe mwenye busara, wacha upumbavu.
Ewe mpumbavu.