Kwanini Unaishi !

Kwanini Unaishi !

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Swali sio kwamba Kwanini watu wanaishi nauliza kwanini wewe Unaishi ?

Dhumuni la swali ni kujaribu kueleweshana huenda watu tumesahau kwamba Binadamu tupo tofauti chema kwako ni kibaya kwa mwingine...; Ila mwisho wa siku kila mtu anahitaji Kusudi (Purpose); kitu kinachomsukuma kuamka asubuhi na kufanya anachofanya..., Iwe ni kumridhisha mwenza, kuhudumia familia, kutoa elimu, kutoa Tiba, Kutetea wenye shida, Kula Bata n.k.

Kama kila mtu ana kusudi (purpose) inayomfanya kufurahia maisha, kama Jamii hatuoni kwamba tunapotoka tunapodhani watu tunaishi ili kupata Pesa ?; Yaani mtu hapendi kujichanganya na watu tunamwambia awe daktari sababu inalipa au mwanasiasa Je huyu atafurahia maisha wakati anachofanya sio kusudi lake ?

Iweje Msanii / Muimbaji aseme kazi ya Usanii hailipi wakati hata asingelipwa angeweza kuifanya Bure ?!!!

Binafsi nadhani maisha ni simple sana watu ndio wanaya-complicate kwa kutaka kuishi kwa jicho la Jamii linavyokuona na sio wewe binafsi unataka nini au kutokujua ni nini tunataka, na kudhani the Grass is Greener on the Other Side - Hivyo kusahau kuishi bali kutumia muda wetu hapa duniani tuki-chase an ILLUSION....
 
Mkuu huwa mnawaza nini
Nadhani hili ndio wazo muhimu kuliko yote hususan kwenye maisha ya sasa ambapo watu wanawapangia watu maisha (mfano watoto wao) wanadhani labda sababu wao wanafurahi kwa wanachofanya au wanashida kwa walichokosa na wenyewe watafurahi, au kusikitika kama wao kwa kupata wanachopata au walichokosa; Mfano wewe ni Mwanasheria una Firm kubwa unamuandaa mtoto wako awe CEO; wakati yeye anapenda kuimba....

Unajikuta hapo unampa purpose mwanao ya kukufurahisha wewe, yaani kuishi kwa ajili yako na sio yeye kutafuta calling yake....

Ni sawasawa unampa kazi Mother Theresa ya kukusanya ushuru au ku-evict watu ambao hawajalipa Kodi...; Unadhani hata ukimlipa billions of money atafurahia...; Au vegetarian sababu hana pesa ya kula unamwambia akauze butcher wakati kuna kazi za kulima mchicha ungeweza ukampa.....

To each their own..., Na tunapoangalia maisha ya wengine kwa upeo wetu tunakosea..., Fikra na Mtizamo wa Mmasai huenda ukawa tofauti na Mchagga / Red Indian / Buddha au Rastafarian....
 
Swali sio kwamba Kwanini watu wanaishi nauliza kwanini wewe Unaishi ?

Dhumuni la swali ni kujaribu kueleweshana huenda watu tumesahau kwamba Binadamu tupo tofauti chema kwako ni kibaya kwa mwingine...; Ila mwisho wa siku kila mtu anahitaji Kusudi (Purpose); kitu kinachomsukuma kuamka asubuhi na kufanya anachofanya..., Iwe ni kumridhisha mwenza, kuhudumia familia, kutoa elimu, kutoa Tiba, Kutetea wenye shida, Kula Bata n.k.

Kama kila mtu ana kusudi (purpose) inayomfanya kufurahia maisha, kama Jamii hatuoni kwamba tunapotoka tunapodhani watu tunaishi ili kupata Pesa ?; Yaani mtu hapendi kujichanganya na watu tunamwambia awe daktari sababu inalipa au mwanasiasa Je huyu atafurahia maisha wakati anachofanya sio kusudi lake ?

Iweje Msanii / Muimbaji aseme kazi ya Usanii hailipi wakati hata asingelipwa angeweza kuifanya Bure ?!!!

Binafsi nadhani maisha ni simple sana watu ndio wanaya-complicate kwa kutaka kuishi kwa jicho la Jamii linavyokuona na sio wewe binafsi unataka nini au kutokujua ni nini tunataka, na kudhani the Grass is Greener on the Other Side - Hivyo kusahau kuishi bali kutumia muda wetu hapa duniani tuki-chase an ILLUSION....
MAda nzuri sana na mimi nitaganda hapa kufanya mjadala wa kina ili nipate elimu zaidi katika huu uzi.

Huu uzi ni muhimu sana lakini watu wengi kuna maisha hayajayapitia ambayo yakawafanya wawe na tafakuri imara kama hizi.

Watu wengi wako bize na hizi mbio za kutafuta maisha mazuri na yenye kuheshimika(rat race) huku wakisahau mambo ya msingi ya kuyaishi.

Je kwa kuanzia tu mkuu,najuaje kusudi langu mimi ?
 
Je kwa kuanzia tu mkuu,najuaje kusudi langu mimi ?
Kusudi: Ni Sababu ya kitu kufanyika..., kwa muktadha wa hii mada Kusudi ni sababu inayokupelekea wewe kufanya kitu fulani..., Ukiondoa mahitaji muhimu ambayo mtu unahitaji ili uweze kuishi (basic needs), sababu bila hayo huwezi hata kuwaza kufanya mengine..., jaribu kufanya mambo ambayo yanafurahisha moyo wako na si vinginevyo.... (tofauti ya hapo utakuwa mtumwa wa maisha)...

Sasa unaweza kuiba sababu upate Pesa (kusudi la wewe kuiba ni kupata Pesa kwa wakati huo) ila jiulize kwanini unahitaji hizo Pesa ? Je unapenda ile Adrenaline Rush na ujanja katika kufanya ule wizi ? Au unaiba ili uwalishe watoto nyumbani au Kumfurahisha mke wa Jirani (na Je mke wa jirani akikukataa hitimisho lako litakuwa limefanikiwa) ? Kwahio unaweza kuona hatari ya kufanya vitu kwa matazamio au furaha ya wengine yaani mtu unafanya kitu sio sababu ya wewe kupenda kukifanya au kiu ya kukifanya bali sababu ya mtu au watu wengine..... (kwahio mwisho wa siku furaha yako inakuwa mikononi mwa wengine)

Unakuta mzazi labda kusudi la kumsomesha mtoto wake sio ili aondoe ujinga na aweze kupambana na maisha ya mbeleni bali labda awe lawyer au aje kuendeleza mali alizochuma yeye (kumbe mtoto huenda yeye ndoto zake akachunguze maisha ya wanyama huko msituni) hivyo hapo unajikuta hakuna wa kumfurahisha mwingine bali wote kuharibiana maisha....

Nadhani kwa ufupi kusudi ni nishati inayokusukuma wewe kufanya kitu ili upate jambo fulani.., sasa cha maana inabidi uangalie hilo kusudi lako kama ni realistic na kweli ndicho unachodhani (yaliyomo yamo) au ni kama tu madawa ya kulevya ambayo unabugia alafu baada ya muda unagundua kwamba hakuna kitu hivyo unaendelea kutafuta zaidi....; Nikirudia tena mfano wangu kama wewe ni mwalimu na kusudi lako la kufundisha ni kuondoa ujinga au kama ni daktari na kusudi lako la kuona wagonjwa ni kuwatibu nadhani utakuwa na maisha realistic kwako na yenye furaha...., nenda kule au fanya kile roho inapenda, watu tupo tofauti kizuri kwako kwa mwingine ni kibaya.... Kawe mkulima sababu unapenda lifestyle ya wakulima na sio sababu Vanilla imepanda bei....
 
Tunaishi ili tufe...
Ukiishi lazima ufe, tungekuwa tunaishi ili tufe kuna shortcut tungechukuwa ya kukatisha maisha sasa hivi na sio baadae... na nadhani tungepewa uamuzi na kama tungekuwa hatuzeeki / Kuchoka ni wachache sana wangechagua Kifo (Hence dunia ingekuwa imeshafurika)
 
Tunaishi ili tufe...
Kama tunsishi ili tufe basi nature isingeruhusu tuzaliwe.

Kwa sababu kama lengo la kuzaliwa ni ili tufe maana yake ilikuwa lengo la kuzaliwa tumelifikia hata kabla ya kuzaliwa kwa maana kila mtu kabla hajazaliwa anakuwa kafa yaani hayupo duniani.

So hata mimi nadhani lengo sio kufa bali kufa ni hatua ya mwisho ya hapa Duniani baada ya kufanya tuliyofanya hapa Duniani.

Ni sawa na mimba tu,lengo sio kuzaliwa kwa mimba bali lengo ni mimba izaliwe na iishi hapa Duniani.
 
Naam ukizingatia Nature inafuata Law of the Fishes...; (Matsya Nyaya is an ancient Indian philosophy which refers to the principle of the Law of Fish. It is described as the fundamental law of nature explained by the proverb of the big fish devouring the smaller fish, hence strong devour the weak)...

Kwahio kwa upande wa nature wanyama wanaazaana wenyewe kwa kupenda ile furaha na kuzaana na hata mimea kuwepo kwa me na ke kunapelekea propagation (na wao binafsi aim yao ni kuzaana na wawe wengi na kizazi zao kisipotee) ila kwa jicho la nature specie moja ni chakula ya specie kingine (sisi tunakufa ili tuwe mbolea na chakula cha mimea, ili tule mimea ili tukifa tuwe chakula cha mimea) Imekuwa hivyo sababu hio ndio sustainable way inayofanya dunia iwe stable....

Lakini individually sidhani kama Swala anaweza kukuelewa ukimwambia yupo pale ili Simba aweze kupata mlo (yeye Binafsi yupo pale ili aweze kuishi as long as possible na kula majani) Na kundi la Swala lipo pale ili liweze kuzaana na kizazi chao kisipotee....;
 
Unachozungumza uko sahihi sana kwa wenye uelewa,kuna mahala nilishawahi kuwaeleza watu kidogo kuhusu jinsi gani nature ina operate,wengi wao waliishia kusema mi nimeanza kula bangi!
 
Unachozungumza uko sahihi sana kwa wenye uelewa,kuna mahala nilishawahi kuwaeleza watu kidogo kuhusu jinsi gani nature ina operate,wengi wao waliishia kusema mi nimeanza kula bangi!
Haya mambo ukiyszungumza kwa watu ambao hawafikirishi bongo zao bila shaka watakuona unazingua na unavuta bangi tu,ni mambo yanahitaji ubongo uliotulia
 
Kwa Nini naishi, swali msingi la kuelekea kwenye ukamilifu wa roho

Any way kama tulivyochukia math ndivo tunavochukia na maswali magumu,,
 
Kila mtu ana sababu yake ya kuishi , hata kama akili yako haijui ,tambua wewe unajua. ,

Jitafute utajua sababu yako ni nini !!!!!
 
Kila mtu ana sababu yake ya kuishi , hata kama akili yako haijui ,tambua wewe unajua. ,

Jitafute utajua sababu yako ni nini !!!!!
Nadhani hilo ndio swali..., Sio kwanini tunaishi bali kwanini unaishi... na hiyo ndio theme ya Mada ukizingatia sababu yako wewe binafsi huenda sio sababu yangu hivyo kukupangia nakosea ukizingatia hio sababu yako ndio inakupa motivation ya kufanya unachofanya...

INGAWA inawezekana wewe sababu yako ni kufika Mlimani au Kwenye Bonde na unadhani huko ndipo unapokwenda ila kumbe ile njia unayopitia kwa sasa haikupeleki kwenye Bonde wala mlima bali kwenye Mto..., thus unajikuta maisha yako yote unakimbiza kitu ambacho hakipo au siku ukifika unapata frustrations sababu ulichodhani sicho....
 
Hakika
 
Kwa upande wangu ninaishi ili kizazi kijacho kuishi.
Kuishi haimaanishi ujue lengo la kuishi maana kuishi kwenyewe ni kusudio tosha bila kujali unaishije.

Kuna watu wanaishi kwa makusudio ya watu wengine yaani nje kabisa na vile wao wanataka kuishi. Aidha wazazi, mke, marafiki, ajira, siasa, mapenzi, mazingira. N.k
Hivyo unajikuta maisha yanakuwa yamejaa maswali mengi, stress, vurugu za kila aina sababu tu haupo katika kusudio lenyewe la kuishi.

Ukiwa mtoto maisha ni raha sana lakini kadri unavyokua na kujaribu kujua mambo mengi ndio njia ya kuipoteza furaha.

Hii ni kwa sababu matamanio yachukua nafasi yake na kitu Tamaa hakijawahi kumuacha mtu salama hakijitoshelezi ni endelevu. Hapa huwezi kuwa na furaha mpaka mauti yanakukuta.
 
Tunaishi ili tufe...
Nimechakata Jibu lako kwenye Grey Matter na Logically lina-make sense kwa mtizamo wa kwamba tunaishi ili baadae tufe (sio nife....); Kwa mtizamo wa Ecosystem....

Yaani ni kama unafuga kuku akifa akiwa kifaranga huenda usipate faida kama akiliwa akiwa amekua mkubwa....

Hivyo nadhani kwa Binadamu kwa macho ya Nature..., ukishakuwa na umbo la kutosha (mbolea ya kutosha) ukaongeza kizazi (watu kama wewe) utakuwa umekamilisha kazi ya kuwa chakula cha mimea na viumbe wengine
 
Tunaishi ili tujifunze.

Au kama mtoa mada unavyosisitiza basi: mimi ninaishi ili nijifunze.

Maana nikiangalia maisha ni mtiririko wa kutolewa katika uzoefu mmoja kupelekwa kwenye uzoefu mwingine.

Mwisho wa siku nafsi yangu iupate uzoefu kamili wa kuishi kwa amani na mapendo na nafsi za watu wengine.

Nahisi hili ni kusudi la msingi la maisha ya utu wetu wa ndani. Experience!

Au nyie ndugu zangu mnadhani ni kwa nini mtoto asizaliwe na kufa tu? Ni nini cha muhimu anachosubiri hadi miaka 8090704020 etc. Au kipi hasa ni cha tofauti anachokuwa nacho mtu wakati anazaliwa? Na wakati anakufa!?

Seee!! Experience........ what has he/she learned nakaribisha michango
 
Back
Top Bottom