Jane Lowassa
JF-Expert Member
- May 10, 2016
- 4,955
- 9,041
Kitabu cha "Cashflow quadrant" cha Robert Kiyosaki kinatuhusu sana hapa.
Jamaa anayaponda sana haya mabenki. Tabia ya mabenki ni kukopesha kwa riba kubwa lakini yenyewe yanauza hati fungani zao kwa riba ndogo sana. Lengo lao ni kupata faida kupitia hela ambayo hawajaifanyia kazi. Kwa kifupi, taasisi za kifedha si rafiki wa watu ila wapo kifaida.
Sasa hivi ni kweli mtu uweke mil 2 kwa mwaka halafu eti upewe 260,000 kama faida. Hivi hii inaingia akilini kweli?
Kutatua tatizo, Kiyosaki anashauri watu wawekeze muda wao kwenye Financial intelligence. Kila mtu akiwa na uelewa wa pesa atakuwa na jicho la tatu na kuona fursa zinazomzunguka na kuzifanyia
kazi kupata faida.
Fursa zipo nyingi sana. Tatizo ni kukosa macho ya kuziona. Kwa mfano mmoja tu: Kununua nafaka kipindi cha mavuno na kuziuza kipindi cha masika. Debe la mahindi kipindi cha mavuno maeneo ya Gairo huwa ni shs 7000. Lakini kipindi cha masika debe hilohilo hufika hadi shs 14,000. Kwahiyo ukiwa na mil 2 unanununua madebe 300. Baada ya miezi 5-6 unakuja kuyauza kwa shs 4000000. Ukitoa gharama za dawa na usafiri unabakiwa na 3.5 m. Unaweza kuona hapo profit margin.
Na huo ni mfano mmoja tu lakini kuna mifano lukuki ya aina hii. Tatizo kubwa tulilo nalo ni kutokuweka kipaumbele kwenye kuwekeza kwenye elimu ya fedha na biashara. Matokeo yake wanakuja hao watu wa NMB na kujifanya wanatupenda sana kiasi cha kutuhifadhia HELA ZETU ili zizae. Hawana upendo mkubwa kiasi hicho.
K