Kwanini ununue gari ambayo gearbox ina gear ratios(more speed numbers) nyingi? Nini faida yake?

Kwanini ununue gari ambayo gearbox ina gear ratios(more speed numbers) nyingi? Nini faida yake?

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
3,381
Reaction score
9,744
Kiukweli unaweza usione faida yoyote lakini faida ipo tena kubwa tu.

Kuna faida kuu mbili

1. Gari ina accelerate faster

2. Gari inakuwa na matumizi mazuri ya mafuta.

Tuachane na gearbox za manual kwanza. Naomba tuzungumzie Automatic Transmissions tu.

Kila kila gear inayokuwa engaged huwa kunakuwa na range ya rpm ambapo hapo ndio maximum power inakuwa transfered kwenda kwenye matairi.

Below hiyo RPM power transfered inakuwa ndogo. Ndio maana itakuwa ni ngumu sana kuaccelerate faster ikiwa gari itaanza na gear namba 5 (let say). Gari itaondoka kwa shida sana.

Ukiwa na fewer gear ratios, utaspend muda mrefu sana kutoka gear moja kwenda gear nyingine. Wakati ukiwa ukiwa na gear ratio nyingi, muda mwingi utaspend katika band ambayo ndio power kubwa inakuwa transfered.

Gari yenye gear ratio nyingi ina accelerate faster kuliko kuliko gari yenye gear ratios chache...

Pia inakuwa na matumizi mazuri ya mafuta kwa sababu engine haiwi kwenye mzigo mkubwa muda mwingi ukilinganisha na gari yenye gear ratios chache...

Ndio maana gari nyingi za mzungu zinaaccelerate faster kuliko gari za mjapani sababu wao walishatoka huko kwenye 4 speed transmission ambazo zimejaa kwa mjapani.

Mjapani anatumia gearbox zenye gear ratios nyingi kwenye matoleo machache sana. Ila gari zake nyingi anaweka tu 4 speed transmission.

Wajapani wa JF karibuni.

Kama unahitaji Diagnosis na repair ya gari lako, 0621 221 606.
 
Mkuu hebu fafanua hapa,
Gari yenye gear ratios nyingi inachanganya faster kwa sababu unaspend muda mfupi sana kutoka kwenye gear ratio moja kwenda kwenye gear ratio nyingine hivyo muda mwingi kiasi kikubwa cha nguvu kinasafiri.

Tofauti na gari yenye gear ratios chache ambapo inatumia muda mwingi between gear ratios hivyo kuna nguvu kubwa inapotea.

Hapo ndio utofauti unapokuja.
 
Kuna mtu hapa ana IST anasema kuna siku kaichakaza Mercedez Benz E 350 7 G Tronic.. 😁😁😁😁.. huyu nimfanyaje aseee
 
Gari yenye gear ratios nyingi inachanganya faster kwa sababu unaspend muda mfupi sana kutoka kwenye gear ratio moja kwenda kwenye gear ratio nyingine hivyo muda mwingi kiasi kikubwa cha nguvu kinasafiri.

Tofauti na gari yenye gear ratios chache ambapo inatumia muda mwingi between gear ratios hivyo kuna nguvu kubwa inapotea.

Hapo ndio utofauti unapokuja.

Unaposema gear ratio nyingi au chache unamaana gani??
 
Waswahili ndio wanaita gear...

Yaani mtu anaposema Hii gari ina gear 4, gear 5 n.k.

Wenzetu wanaita 4 speed, 5 speed n.k

Hapo sasa nimekuelewa na hata mimi ndivyo nijuavyo isipokuwa nilidhani nilikuwa sijui.

Hivyo speed ratios sio sawa na speeds/idadi ya gear za gari yaani ni vitu viwili tofauti. Si ndio?!
 
4 speed na 9 speed zikikaa road ni ardhi na mbingu.
Labda ziwe zilikuwa speed afu zikakutana na mlima ..mwenye 4 speed hio four atashusha tatu ila mwenye 9 speed anayo gia ingne ambayo ipo katikati ya 4 na 3 kwenye 4speed ...more ratios hii gia box tunaita close ratio...

Kuna magari mengi yanayovunja rekord nyingi ni 7 speed tu

Cheki germany kule nurbugring
 
Haya matoyota Yana safari ndefu Sana ya kufanya competition na mjerumani... kwasababu asilimia 90 ya magari ya mjapan hapa Tanzania ni 4 speed transmission kitu ambacho Kwa magari ya kijerumani huwezi kuona hiyoo..
Huwa nawaonea huruma Sana madereva WA IST wanavyoingia kwenye ligi wasioweza kushinda
 
Watu wa IST wamekukosea nini ndugu mchangiaji?

Huwezi kuchangia bila kuwakejeli hao?
 
Back
Top Bottom