Ulichosema ni kweli kabisa mkuu, binafsi nilikuwa napata wakati mgumu sana kukubaliana na vile nilisikia kuwa gari yenye cvt inachanganya haraka kuliko Atf type 4 n.k
Nina washkaji zngu wanahizo gari ambazo ni toyota rumio na fielder 2009, kusema kweli zinapo anza kuondoka huwa zinalalamika sana yaaan nguvu inakuwa ndogo tena usiombe kuwe na kizuiz kama vile mchanga n.k.
Nikawa najisemea au zinatatizo hizi gari!? Sikuwahi kupata jibu hadi hapo ulvyozungumza aisee. Ila kwenye tambarare zipo vizuri sana na zinatumia mafuta vizuri sana aisee. Unawwza fika 80k/h rpm ipo kwenye 1000 (1).
Kwa gar nyingi ambazo hazitumii cvt speed kuanzia 80 kuendelea rpm lazma iwe chin kidogo ya 2000 (2) au zaid hataiwe kwenye mteremko.