Kwanini uogope kuuza nyumba?

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,286
Reaction score
6,736
Najua wapo watakaonipinga, tena sana tu. Lakini kwa mtu unayejiamini mambo yameenda kombo, umri wako unaruhusu kuchakarika huna sababu ya kuogopa kuuza nyumba iwapo iko sehemu mzuri ambayo unaweza kupiga pesa ya maana.

Niliwahi kumshauri baba yangu kuuza nyumba moja mwaka fulani, alinisema sana na kusisitiza kuwa sina akili timamu.

Baada ya mambo kumbana mwenyewe akaamua kuuza. Kiasi fulani cha pesa tukaingiza kwenye biashara ya samaki aina ya Sangara.

Kwa watu wa kusini wanaelewa vizuri biashara hii.
Leo ana Mashamba na nyumba nyingine lakini chanzo ni mtaji uliotokana na kuuza nyumba.

Wadau wengi humu jukwaani ni waoga, wako tayari kumshauri mtu kuchukua mkopo wa riba huku nyumba akiiweka kwenye mikono ya benki lakini si kuuza nyumba.
 
Kwa kweli mkopo wa riba na kuingiza kwenye biashara sio uamuzi wa busara
Ila kama huna njia nyingine na huna kitu ila nyumba tu aaah uza tu na ujipange upya ila kama ipo maeneo mazuri na unauza kwa bei ya uhakika ambayo unaweza kupata eneo rahisi na kujenga hata kibanda kwanza na zingine ukafanyia kazi sawa
 
Sawa kabisa Mkuu.
 
Wengi wanakopa wanavamia biashara ambazo hawana utafiti wa kutoshaa
 
nimeshamshauri mtu badala ya kuchukua mkopo benk na kuweka rehani nyumba.. ni bora aiuze kwa hela nzuri... anunue ingine eneo nje ya mji ya bei nafuu.. hela inayobaki aiwekeze anapotaka sababu anahitaji milion 15 ila anataka weka rehani nyumba iliyopo eneo lenye thamani ya mamilioni kibao
 
Hii ndio akili inayochambua mambo.
 
Mtu mwenye mawazo ya kimasikini lazima wanaogopa vitu kama hivi.

Kuuza nyumba ni jambo la kawaida sana.

Mzee wangu alikuwa na nyumba 3. Kuna nyumba ilikuwa imekaa sehemu mbaya halafu uswahilini sana.

Nikamwambia aiuze apate mtaji. Akagoma sana ila alikuja iuza. Sahivi anaingiza hela ya kutosha.

Woga wako ndo umasikini wako.
 
Watu wengi ni waoga wa kuamua,hawana muda wa kutafakari na huendekeza sana ushauri. Maisha ni yako kunawakati inabidi uamue tu na hii ndiyo raha ya kutokuwa mtoto. Take responsibility!ukifaulu poa,ukifeli poa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…