GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,286
- 6,736
Najua wapo watakaonipinga, tena sana tu. Lakini kwa mtu unayejiamini mambo yameenda kombo, umri wako unaruhusu kuchakarika huna sababu ya kuogopa kuuza nyumba iwapo iko sehemu mzuri ambayo unaweza kupiga pesa ya maana.
Niliwahi kumshauri baba yangu kuuza nyumba moja mwaka fulani, alinisema sana na kusisitiza kuwa sina akili timamu.
Baada ya mambo kumbana mwenyewe akaamua kuuza. Kiasi fulani cha pesa tukaingiza kwenye biashara ya samaki aina ya Sangara.
Kwa watu wa kusini wanaelewa vizuri biashara hii.
Leo ana Mashamba na nyumba nyingine lakini chanzo ni mtaji uliotokana na kuuza nyumba.
Wadau wengi humu jukwaani ni waoga, wako tayari kumshauri mtu kuchukua mkopo wa riba huku nyumba akiiweka kwenye mikono ya benki lakini si kuuza nyumba.