Strong ladg
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 1,357
- 3,114
Kwanza nianze kwa kusema sijawahi kufika Ulaya, kila kitu nakiona kwenye TV na mitandao ya kijamii.
Katika kufuatilia kwangu kuna utofauti nimeuona kati ya Urusi na nchi nyingine za Ulaya. Wakati nchi nyingine za Ulaya hasa Magharibi mfano Ufaransa, Ujerumani, Uingereza wakiongea kuhusu haki zinazohusiana na masuala ya upinde, vyombo vya habari vya Urusi vimekuwa na maudhui yanayokemea masuala hayo. Kuna siku niliona video RT inaonesha askari wa Urusi wakivamia na kukamata wanaume katika klabu moja ya usiku kwa madai kuwa wanaume hao wanaeneza mambo ya upinde.
Vilevile Rais hata Putin katika baadhi ya hotuba zake zilizoziona kuna maneno ametumia kuhamasisha " traditional moral values" kinyume na " neo liberalism" ya nchi za Magharibi.
Vilevile nimeona mara kadhaa media za Urusi zikiliongelea Kanisa lao la Ordhodox kwa namna ya heshima na kama kitu cha kujivunia ,kitu ambacho ni nadra kukiona kwenye media za Ulaya Magharibi. Katika hoja zao dhidi ya Ukraine , baadhi ya maafisa wa Urusi wametumia maneno kama" Zelensky amekosa hata ile misingi ya kawaida ya kikristo"mfano baada ya ripoti kuwa serikali ya Ukraine imekataa kupokea miili ya wanajeshi wa Ukraine ambao Urusi ilikuwa tayari kukabidhi kwa Ukraine baada ya mazungumzo yaliyofanyika hivi karibuni huko Uturuki. Sikumbuki mara ya mwisho kumsikia kiongozi wa nchi ya Magharibi akitaja dini kama sehemu ya hoja fulani.
Swali: Imekuwaje Urusi bado haijapoteza dini yake na " traditional values zake" kama kutohamasisha masuala ya upinde ikilinganishwa na nchi nyingine za Ulaya zilizoendelea katika sayansi, teknolojia n.k?
Asante.
Naruhusu kurekebishwa kama nimekosea.