Kwanini Urusi ndio iliumia kuvunjika kwa USSR kuliko washirika wengine

Kwanini Urusi ndio iliumia kuvunjika kwa USSR kuliko washirika wengine

Leo hii unapotazama wanaoipigia promo sana kurudi kwa USSR ni Urusi tu na ndio maana wananchi wa Beralusi walipotaka muondosha Rais wao mwenye mfumo wa Urais unaoendana na Urusi.

Urusi aliingilia kati na akafanikiwa kulinda madaraka ya Rais wa Belarusi, Ingawa kwa Rais Pro Russia wa Ukraine ilishindikana kabisa.

Hata katika upigaji wa kura wakati wa anguko la USSR wananchi wa Urusi ndio walipiga kura umoja huo uendelee.

Wakati Urusi akiwa dhaifu baadhi ya wananchi wanachama wengi wakakimbilia NATO na alipoanza imarika wengi wakazidi hamia upande wa pili.

Na sasa akiwa katika kilele cha uimara wake hata nchi ambazo hazifungamani na yoyote wamejiunga na umoja huo.

Je, Urusi alizitawala kimabavu

Au ndio umoja wa Masikini haudumu tofauti na Matajiri
Hali halisi USSR ilikuwa Milki ya Urusi ya Kifalme kwa umbo tofauti. Na milki ile ilikuwa tokeo la karne nne za ukoloni wa Kirusi. Je ni ajabu kwamba wengine walichukia nafasi ya kupata uhuru? Na Warusi kusikitika ? HAta Uingereza kuan watu wanaolia hadi leo wakikumbuka siku walipokuwa milki kubwa pamoja na Afrika, Kanada, Australia na Uhindi. Walie tu.
 
Back
Top Bottom