Kwanini utajiri wa familia za Kitanzania sio endelevu vizazi kwa vizazi? Je chanzo ni Siasa na Utawala au ulozi?

Kwanini utajiri wa familia za Kitanzania sio endelevu vizazi kwa vizazi? Je chanzo ni Siasa na Utawala au ulozi?

Njanga Tz

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2015
Posts
843
Reaction score
655
Hili swali kila siku najiuliza sipati majibu sahihi. Utajiri wa mababu zetu umeenda wapi? Uhakika ni kwamba walifanya kazi na walikuwa na mali za kutosha lakini kwa sasa hazionekani tena.
 
Hili swali kila siku najiuliza sipati majibu sahihi. Utajiri wa mababu zetu umeenda wapi? Uhakika ni kwamba walifanya kazi na walikuwa na mali za kutosha lakini kwa sasa hazionekani tena.
Utajiri una kanuni zake....na mara zote huwa hazitamkwi kwa sauti....na kurasa zake zimefichika kwa ajili ya wateule wachache
 
Tatizo la Watanzania kuna usiri mwingi sana katika kila jambo.

Utakuta baba ana pesa nyingi lakini watoto hawajui hasa source ya kipato cha mzee ama ana mali nyingi kiasi gani. KIla jambo ili liendelee linategemea uwepo wa baba, hatima yake siku akianguka na mali zinaanguka na nyingine kupotea kabisa.

Wenzetu wa ngozi nyeupe mtoto anaambiwa kuhusu mali za familia akiwa mdogo kabisa, hata kama ikiwa ni mali ya ndumba. Anaanza kupewa majukumu kidogo kidogo mpaka akifika umri sahihi tayari anakuwa na experience pamoja na uelewa wa mali/biashara za familia. Hapo ikitokea hata baba akafariki hakuna kinachotetereka.

Hili swala la kushirikisha watoto mapema linasaidia pia kukuza mali. Kadri muda unavyokwenda uwezo wa wazee unapungua na kushindwa kuhimili maendeleo mfano ya kiteknolojia. Ikiwa watoto washashirkishwa inakuwa ni rahisi ku transion katika muelekeo wa hayo mabadiliko ya wakati. Mfano mzuri Bakhressa na watoto wake. Maendeleo yote ya kibiashara ya Bakhressa kwa sasa sio akili yake, ni watoto.
Ila angekomaa mwenyewe kama wabongo angeishia kuuza ice cream tu Livingstone.

Sasa kibongo bongo unakuta baba alikuwa mkulima na mfugaji mkubwa miaka ya 70. Mpaka leo 2023 anataka kuendelea kufuga ama kulima kizmani maana ndio njia pekee anayojuwa na watoto hakuwashirikisha kabla. Mwisho wa siku ikiwa hakufilisika basi siku akifa na mali zake zote bye bye.
 
Ndoto za wazazi na watoto ni tofauti.. mtoto akikuwa anataka atimize ndoto zake sio kuendeleza ndoto za wazazi...japo wachache wanaweza.

Baadhi ya wenye utajiri huo kuwa na mahusiano tofauti nje ya ndoa... watoto wa nje wengi kiasi kwamba hata mzazi akifariki bila wosia au hata na wosia usimamizi unakosekana ...mali zinaishia kuuzwa au vinginevyo
 
Najua wengi wetu hatuamini, mambo mengi yatendekayo duniani yana upande wa pili wa kiroho ambao unasaidiana na upande mwingine wa kimwili ili kufanikisha jambo au mambo fulani ya maisha ya binadamu!na upande wa kiroho una side 2 pia upande wa NURU na GIZA.
Sasa tuje kwenye topic ya utajiri asilimia kubwa ya utajiri hasa wa kiafrika, Asia unaambatana na nguvu za kiroho na ni mara chache sana kukuta Tajiri wa kupindukia amepata utajiri kwa juhudi zake binafsi mwanzo mwisho na hapa hatuzungimzii Matajiri mbuzi wenye maduka Kariakoo [emoji23][emoji23]
Sasa tuje tofauti ya Matajiri wa kiafrika na Kiasia.
Matajiri wa kiafrika utajiri wao unaambatana na maagano na makafara mengi sana yakiwemo kuwatoa ndugu zao, na mara nyingi aina hii ya utajiri hupotea pale muhusika anapopotea na yeye na pia utajiri wa kiafrika unaambatana na biashara za dhulma na Magendo ambazo mara chache mwenyewe akiondoka waliobaki wanashindwa kuzi maintains.

Kuna exception ya baadhi ya Matajiri wa kiafrika ambao wako kwenye hizi jumuiya za Siri (secret societies) hapa utajiri huwa unaendelea kizazi na kizazi provided hii imani inaendelea kurithishwa ndani yao.

Utajiri wa kiasia nao wanategemea nguvu za Majini na miungu wengine na wenyewe unategemea makafara na alikes lakini wenzetu uwa wanatengeneza empire ambayo inakubaliana na maamuzi ya familia katika kuudumisha huo utajiri, hii iko applied kwa jamii za Waarabu, Hindi, Chinese, Japanese nk

Mwisho tuzungumzie utajiri wa Kizungu hapa ndipo unapoweza kuta Tajiri ameanza na kushona mtaani na sasa anamiliki viwanda vya nguo! Though na wao wale ma Mogul wana husiana moja kwa moja na Secret societies!

In summary utajiri karibu wote na milki karibu yote ya duniani ina uhusiano wa moja kwa moja na Shetani kama ilivyoainishwa kwenye Biblia takatifu pale shetani alipomwambia Yesu amsujudie na atampa milki na utajiri wote wa duniani! So don't struggle to be rich except to achieve better life wewe na family yako otherwise you will be forced to bow to Lucifer.
 
Sababu za MTU kuwa masikini ndo sababu za MTU kuwa tajiri

Mali kuipata jambo moja Ila kumiliki kuikuza na kuiendeleza inahitaji umakini Sana .
 
Utajiri ni mtazamo

Utajiri wa wazee wetu ulikuwa katika mali kama mifugo mazao na ardhi

Hivi vitu vyao .havikuwekwa kwa mtindo wa biashara au teknolojia ambayo inakuwa kutokana na muda

Mimi naona wenzetu waliwekeza sana kwenye biashara na teknolojia na Elimu

Sasa wewe unaishia kufuata mikia ya ng'ombe tu utafika wapi sasa??

Kwa level ya familia wekeza kwenye hayo maeneo utaona baada ya miaja 15 hadi 20
 
Back
Top Bottom