Kwanini utumie x badala ya s?

ndo maana kuna formal and informal language inategemea na social context nitumie lugha ipi kapate somo la stylistic wewe....mnataka hadi jf tufwate kanuni ka naandika barua kwa boss haaaa mtatuua nyie xaxa!

Ni wajinga tu wachache kama wewe ndio watatetea huo ujinga mtu anaandka "co" badala ya "so" na "xixi" badala ya "sisi" ni stylistics gani uliyofundishwa wewe? Labda kama ulifundishwa na mwalimu wa voda fasta aliyepata E ya english advance.

Hebu fuatilia comments za wazungu kwenye english wanaweka lugha imenyoka na kama ni kifupisho ni kile ambacho kinakubalika sio hawa washenzi wanaandika si kifupisho wala nini ila ni kuharibu lugha tu
 

Walewale...Under 18 kichwani umri over 25.
 
Bora wao, kuliko wewe unaejifanya unajua kumbe hujui. Badala ya heruei kubwa mwanzo wa sentesi wewe umeweka ndogo.. Ama kweli nyani hacheki [color=#ff000]kundule lake[/color].

Hapo ni nini? mkuu.
 

Jamaa unamuelimisha vinzuri, lakini na wewe umeboa kutoa mfano kwa wanzungu
 

mpaka hapa nimegundua hujui sayance ya lugha unaendeshwa na politics za bakita nyie ndo mnaotuletea maneno ya ajabu kama kipanya,jokofu,mdalahisi,tonaridi mnaishia kukiua kiswahili badala ya yakukijenga xababu ya ukiritimba wenu,,
 
Hizo herufi zao zimenifanya nisimtumie binamu yangu hela ya mahafali,
eti kaandika
"xaxa kaka utanitumia lini hela ya mahafali"?

Acha visingizio si useme kuwa ulikuwa hauna kitu...ukamtafutia sababu..
 
Kusema kweli huo uandishi wa x badala ya s unakera sana.Wahusika waache huo ujinga!
 
Ni mambo ya msimu yataisha kwa kuelimishana matusi na kuzodoana inasaidia kidogo. kwa ambao wanasoma andika hivyo kwenye mitihani utaona matokeo yake.
 
Kitoto kimoja nimekitongoza juzi tena kizuri nikawa najua nimepata mchepuko wa maana alivyo anza kuniandikia huo upuuzi wa xaxa sijui nini, nikapiga chini hapo hapo yaaani sijajibu msg hata moja na simu nimeblock kabisa

Hahaha.... Mkuu we ni noma. Unaacha mchepuko kisa matumizi ya x badala ya s.
 
Wakuu mie naona mnabishana tu na kitu kisicho maana. Labda hamfahamu kuwa kila kitu kina mitindo yake ambayo huibuka na baada ya mda kupotea kwa mfano hata mavazi huwa na mitindo yake ambayo huibuka na kupotea pia kuna misimu katika lugha ambayo pia huibuka na kupotea, kwa hiyo kama una uelewa wa dhana niliyoielezea halo juu huna haja ya kuboreka wala kushangaa kwa sababu ni vitu vya kawaida. Pia mitindo ya uandishi huzingatia muktadha ambamo maandishi unshusika wakuu. Kwa hyo si kitu cha kustaajabu.
 
Ugomvi upo kwenye lugha mama ya Kiswahili, mpaka sasa hatuna herufi X.

Kwenye lugha nyingine za nchi za Magharibi na Mashariki ya mbali, herufi hii X imebeba maana pana sana. Huu ni mfano tu, kuna ukiukaji mwingi sana wa kiuandishi katika kiswahili kuchanganya namba na herufi.

Mfano...wa2 wackuhizi wagumu kuckia...n.k wengi hatuvutiwi na uandishi huu wenye sura ya utoto, ulimbukeni au uhuni.
 
hanna cha kuoka muda wala kufupisha..maana xaxa na sasa zote zina herufi tano, xo na so zote mbili n.k....wanaboa tu
 
xaxa tufanyeje kwa xababu mimi pia wananiboa xaaana!
 
Umenena, si suala la kufupisha, na kweli kama ni swaga zinaboa, hasileti maana eti, heri kuandika mfano m2 badala ya mtu, n.k. inaeleweka kuliko hizo x zao.
hanna cha kuoka muda wala kufupisha..maana xaxa na sasa zote zina herufi tano, xo na so zote mbili n.k....wanaboa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…