Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Naona wameweka Tangazo la kazi la NIT.. nafasi zinatangazwa upya.. Ila Leo wadau tusichoke kufikia jioni mpaka usiku kitaeleweka tu maana washaanza kustua mitambo Mchana huu
Baadhi ya vyuo vimeshapata wakufunzi, na hatimaye wanarudia tena kutangaza upya kwenye zile nafasi ambazo hawakupata watu.

Wakati huo huo, vyuo vingine bado hata hawajaita interview ya mara ya kwanza, na wakati huo tarehe za kufungua vyuo zimekaribia.
Hii nchi unaweza ukaletewa MBOLEA wakati wewe ndio UNAVUNA.
 
Mkuu kazi ushapata kilichobaki ni hizo process tu.

Subiri uende kazini halafu ukiwa na mood ya shule utatokea huko kazini, kuna faida ya kusoma ukiwa tayari una kazi.

Ukirudi kazini baada ya masomo, maslahi yatanona.
 
Hivi TA ni lazima aanze masomo ya Master pindi anapoajiriwa?

Mimi huwa najua ataanza kusoma muda wowote akitaka pindi akiwa kashaanza kazi.

Mfano, kuna Mwl wangu yeye aliajiriwa uTA mwaka 2014, then mwaka 2015 ndio alianza kusoma Master huku akiendelea na majukumu ya kufundisha kama kawaida.

Labda kwa upande mwingine hii inaweza ikawa inatokana na taratibu za Chuo kama ulivyotolea mfano UDSM.
 
Leo Kuna muda website ya utumishi ilikua nzito kufunguka nikajua huenda kuna kitu kinono kinapakiwa humo,ila sasa imekaa poa tu na hakuna lolote lililopakiwa.
Hahahahaaa.
Wanacheza sana na fikra zetu
 
TA sio lazima uanze kusoma ukishaajiliwa inakuaga wanakupa muda kama miaka mitatu hivi lazima uwe umeanza kujiendeleza
 
Duu, kwamba walikanda watu hadi wakakosa wenye sifa..

Haya wasaka mrija ingieni ulingoni tena.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kwamba majobless wote walidandia mtumbwi wa vibwengo hahhhh
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Jobless tunapata tabu sana
 
TA alikua anafundisha level gani ? Diploma ?
 
Kwa sheria za vyuo vikuu TA ni ajira mafunzoni, unatakiwa ukasome masters mapema iwezekanavyo maana hakuna kazi unaweza kufanya pale chuoni (as a teaching staff) kwa hizo qualifications za bachelor. (Wewe nk "mtoto mdogo" in TID's voice).

Special case ni pale ambapo chuo kinakua kinatoa kozi za diploma. Ukiwa na bachelor unaruhusiwa kufundisha diploma.
 
Na wanaofundisha diploma kwenye vyuo vya kati wanaitwa TUTOR mfano veta, ADEM, vyuo vya Ualimu vitoavyo diploma n.k ila vyuo vikuu ndio uitwa TUTORIAL ASSISTANT japo wote sifa ni degree japo chuo kikuu wanaangalia na GPA wanataka ya 3.8 +
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…