Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Kuna pdf la nafasi 300+ za kazi NSSF ila ni internal job opportunities kwa wanaojitolea na wenye temporary contract tu. Madhara ya taasisi kujitegemea sasa yanaanza rasmi kuonekana
AJIRA ZA TEMPORARY NA MKATABA UTUMISHI HAWAZISIMAMII MBONA ZINASIMAMIWA NA TAASISI
 
msajili wa hazina- mchechu
Naona lengo lao linataka kutimia, hii nchi inaviongozi wa ovyo kuliko nchi zote duniani, wabinafsi wajatumbo na wasiofikiria, yaan wanatumia misuli ya kichwa kufikiria bila kushirikisha ubongo, mama Rais uko ulipo Mungu akushukie ulione ili. haki inauzwa, inaporwa, jobless tusio na connection hatuna pa kukimbilia dah, inasikitisha sana
 
Walianza harakati zao hiz toka mwezi wa 4 mwaka huu pale bungeni kwa kuanza na mapendekezo yao ya "wanaojitolea wapewe kipaumbele" speaker akiwa msitari wa mbele kupigia chapuo hii kitu. Kuna kitu walikua wana kiandaa apa kwani baada tu hili pendekezo pale bungeni, TRA walijitoa PSRS na kutangaza nafasi za kazi wakiwa wao kama wao yan bila mkono wa PSRS kama ilivyokua huko nyuma. TRA ni sample tu na Mpaka apo target yao walishaifikia ni suala la mda tu.

Hili suala la kujitolea Kuna uhuni mwingi sana apa kati..

Ni nani asiyetaka kujitolea NSSF, TRA ama WCF n.k?
Hao wana ojitolea waliipataje hiyo nafasi?
Tuseme mfano hao watu 300+ wanaotakiwa na NSSF, je waliingiaje pale?

Tuseme kuna TAESA. sote tunafahamu contract ya TAESA ni only 1 year sasa hawa wa 5 years wako ofisin miaka nenda rudi kwa mgongo wa kujitolea. Je wanastahili hiyo favour wakati wameingia kihuni bila fair competition?

Maswali n mengi sana na Hayana majibu. Hiv kwel vile vichwa vyote pale bungeni hakuna aliyeona hili likija?
Inakera sana.

Hakuna kiumbe selfish kama mwanasiasa.
 
AJIRA ZA TEMPORARY NA MKATABA UTUMISHI HAWAZISIMAMII MBONA ZINASIMAMIWA NA TAASISI
Tatizo ni kwamba inalazimishwa hao wenye kujitolea na wenye mikataba mifupi wapewe kipaumbele kwenye ajira!! Hiyo si haki maana haiwezekani watafutaji wote wa ajira waweze kujitolea!! Haki ni kutoa fursa sawa kwa wote kwenye kugombania ajira!!
 
Mie nilishtuka sana hiii kauli ya watu wa kujitolea inakaziwa ,,mbali na hapo taasisi za kiserikali zijiendeshe zenyewe,,,, yaaani hizi kauli kwa watoto masikini ni kama kuwafukuza na kuwabakizia nafasi za LGAs ila nafasi nzuri nzuri wanaenda kwa kujuana ....Wanasiasa Wanatafuta sehem,wakipiga simu mpokeeni huyu kijana

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
PSRS nafasi 6000+ mmeamua kutuchinjia mbali...
Zaidi tunaona viburi +ubaguzi wa taasisi katika Ajira....!!!!!
 
Hapo ndio uandae kesho ya mwanao kwa kujiwekeza hata tufanyeje serikali haiwezi kuajiri watu million 20+.

Suluhisho ya kudumu ni kustawi kwa private sector na hakuna mtu atapataka serikalini kama ajira za kumwaga zipo private sector.

Pambana kwaajili ya mwanao.
 
Ndio hata forgery kwenye masuala ya vyeti itarudi ,moja ya sababu ya psrs kuanzishwa ilikuwa ni hiyo kucheki validity ya academic credentials za wasailiwa ,Magumashi yanarudi tena kwa kasi ,kmamae .
Nchi inatia hasira hii we acha tu
Nafasi za ajira kwenye taasisi hizi zipo nyingi tu lakini hawataki kuzitangaza sababu ndugu zao wamezishika kwa kigezo cha kujitolea/mkataba. Sasa hivi wamepewa rungu utaona zitakavyomiminika.
 
Wamefanya maamuzi yatakayo cost Taifa ajira saizi ni kwaheri mpaka taratibu zitakapo badilishwa haya ni madhara ya kubadilisha utaratibu, kila kiongozi akiingia anashahriwa ujinga ili wafanye yao, kila kiongozi anafanya yake ndio maana taifa la ajabu, tutahangaika sana mpaka tuje kujitambua sio leo ni watoto wa vigogo watafaidi watu wa chini basi tena.
 
Ndugu zangu, utaratibu wa kipindi hiki bado ni mpya, endapo kuna yoyote atakayepeleka malalamiko TRA kuhusu hizi ajira na akasikilizwa, tafadhali tufahamishane ili na wengine wenye changamoto mbali mbali waweze kujua kwamba nafasi ya kusaidiwa ipo.
 
Sasa nani kasema wote lazima wapate serikalini issue iliopo mezani ni kuzingatia kanununi, taratibu na sheria za ajira wapi kuna kanuni au sheria inayotaja kuwa mtu anayejitolea apewe kipaumbele kwenye ajira kama sio utashi wao walio shikiria mpini kwenye mataasisi makubwa.
 
Ni sahihi sio ndio maana hao NSSF umeona wamekaa miaka mingi bila kuajiri kumbe wana vijana takribani 400 wanaojitolea huko, inasikitisha kwa kweli.
Yaani unampa mkurugenzi mbinafsi na HR njaa aajiri taasisi kama NSSF, TRA nazinfine zote anagalia nafasi 492 zote ni internal sasa, hao watu kama walikuwa kwa mkataba kwanini wasitangaze kwa uwazi hizo nafasi hapo ndo wanapo create hasira na gape katibya watanzania, saizi ajira zitkuwa ni ngumu zaidi.Kw staili hii huo utaratibu urudi bungeni uangaliwe upya hii nchi sio ya vigogo peke yao na watoto wao ambao wapo kwenye taasisi nyeti
 

Nimelenga suluhisho la muda mrefu, take it or leave it. Kama hautochukua hatua za makusudi kujinasua utabakia kulaumu mpaka destiny yako itakapo kuwa decided na your Creator.

Take action.
 
Na Mimi nauliza je ? Kesho likitoka tangazo la kazi halmashauri wilaya ya mtwara , na wakitaka wana mtwara tu?? Huu utakuwa ubaguzi au sio ubaguzi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…