Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

Hii sio sawa kabisa ni swala la kukemewa, hizi zilipaswa kupitia utumishi au hata km wameamua kuajiri basi iwe wazi kwa vijana wote wenye vigezo wajaribu bahati zao
 
Nyinyi mna matatizo sana... Suluhu la hizi kelele hapa ni moja tu, na sisi tuingie hukohuko siasani
 
Kuumaliza huu utata ni kuingia A/c ya twitter Utumishi ....
Kutoa ushauri zaidi ... wanasiasa upinzani watazibeba kama agenda
 
Kuumaliza huu utata ni kuingia A/c ya twitter Utumishi ....
Kutoa ushauri zaidi ya wanasiasa upinzani watazibeba kama agenda
Selika inatoa vibali vya ajira, interview inatumia mwaka mzima kumbe ni mgomo hawataki watu kutoka psrs. Kuna
jamaa ameniambia wao walinuniwa kabisa, ni vita njaa kali, kila mtu anataka mwanae aishi vizuri, nimsuguano huko yaani ajira zipo mashirika hayataki kupokea watu, bora wawe na intern hata miaka saba, jiulize NSSF kwanini hawakuomba kibali muda wote huo, ubinafsi kunzia BOT,TRA, NSSF, TANROAD kote ina maana hii nchi ni yao wao, hii sio sawa kabisa,inaumiza sana
 
Kuna wakati natamani ata izo nafasi zao kuanzia ubunge, sijui uspika, uwaziri, na unaibu wake, wakuu wa wilaya,mikoa, makatibu, nafasi zotee za kuteuliwa I wish kama nawao wangefanyiwa usail, zitongazwe waombe kwa interview nawahakikishieni huu upumbavu na ulegevu wao wa fikra ungefika mwisho.
 
Nenda uko kote kwenye bahari za asali angalia maboss wa juu wote wameteuliwa, yaan imekuwa kama izo ofisi ni zao nao wakateua watu wao wakawapachika umo na hao watu wao ndo sasa nao wanachagua na kupachika tena watu wao, imekuwa kama urithi sasa, ndo maana madudu hayaishi umo, ofisi zinakuwa na matabaka, ukabila, na nyingine ata udini, utendaji ovyo chuki za ovyo ovyo.
 
Vijana miaka yote wanaulizia jamani mbona hatujawahi kuona nafasi za kazi za Nssf zikitangazwa au hawana uhaba wa watumishi? , kumbe wenzetu wana watu takribani 400 wanajitolea huko, dah nimeamini kweli Serikali ina sirikali
 
Vijana miaka yote wanaulizia jamani mbona hatujawahi kuona nafasi za kazi za Nssf zikitangazwa au hawana uhaba wa watumishi? , kumbe wenzetu wana watu takribani 400 wanajitolea huko, dah nimeamini kweli Serikali ina sirikali
Na wametoa tangazo la kazi nafasi 392 na hii ni internal announcement, barua lazima ipitie kwa meneja wa mkoa.. jamaniii

Kuna jamaa angu akaniambia niforce nipeleke tu kulaleki wakaitupe wenyewe kwenye dustbin hukohuko
 
Vijana miaka yote wanaulizia jamani mbona hatujawahi kuona nafasi za kazi za Nssf zikitangazwa au hawana uhaba wa watumishi? , kumbe wenzetu wana watu takribani 400 wanajitolea huko, dah nimeamini kweli Serikali ina sirikali
[emoji40][emoji2297]...Mungu atusaidie!!!!
 
Hata kuna mmoja alihamia taasisi kufika pale anakuta watu wana mikataba mwaka wa 6 wanarenew tu. Wakienda psrs wanakandwa.
 
Dah! Tunaenda wapi jamaniiiii
 
Ni kweli ndio maana mashirika na taasisi za Serikali zimekuwa ni mzigo kwa Serikali hii ni kutokana na Manpower iliyopo kuwa imeingia hapo za kwa vigezo vya uwezo bali ni kujuana pia hakuna anayeweza kumchukulia mwingine hatua kwa sababu ya kujuana huko, mwisho wa siku ni haya mashirika kuperform chini ya kiwango ili hali kulipana mishahara minono na marupurupu ndio kipa umbele.
Serikali inatakiwa kulitazama jambo hili kwa upana sana , hili la NSSF limeshtua sana, inatia shaka hata huo usaili wa TRA wa wiki ijayo unaweza kuwa ni kutimiza taratibu tu watakaopata ajira ni haohao waliopo TRA wanaojitolea.

Fikiria tu kwamba , mwezi wa kwanza vijana takribani 700 walifanya oral upande wa Tax management officer kati ya hao 184 ndio walioitwa kazini, kwa hiyo inaonesha vijana wengi kati ya idadi hiyo walikuwa data base ya utumishi, sasa swali ni kwanini isengetumika busara kwa hizi nafasi za sasa 206 za tax management officer kuwapa vijana waliokuwa data base ya utumishi ,kisha wakati ujao ndio hawa TRA wangeendelea wenyewe na mchakato wao wa kuajiri., ukizingatia kuwa hawa vijana waliingia data base mwezi wa kwanza na TRA wametangaza kazi mwezi wa tano, takribani ni miezi 3 tu ambayo kwa life span ya data base ilikuwa bado sana.

Ndio maana nikiitazama hii hali naona kuna jambo nyuma ya pazia.

Nampongeza sana Mh. Rais Dr. Samia Hassan kwa kufungua fursa za ajira nyingi sana kwa vijana kipindi hiki cha uongozi wake, ila changamoto hii aitazame kwa jicho jingine kabisa kama kuna watu wanamshauri ndivyo sivyo ni vema akapingana na mawazo yao maana itamharibia kazi yake nzuri aliyoianzisha ya kufungua fursa za ajira kwa vijana.

Jambo muhimu ni kuwa ajira zitangazwe watu waombe wakashindane , atakaeshinda apate nafasi lakini siyo kama ilivyojitokeza hili la NSSF limeta taswira mbaya sana kwa taifa.
 
Na Mimi nauliza je ? Kesho likitoka tangazo la kazi halmashauri wilaya ya mtwara , na wakitaka wana mtwara tu?? Huu utakuwa ubaguzi au sio ubaguzi??
Kama NSSF wakiruhusiwa na kuachwa watimize huo ubaguzi waliouanza, kila mwajiri atakuwa na haki ya kuajiri "wa ndani". Kila halmashauri inaweza kutumia huo mwanya, na kila mwajiri anaweza kutumia huo mwanya. NSSF lazima waambiwe kuwa hilo ni shirika la umma na linaendeshwa na kodi za watanzania wote, na linachangiwa michango na watanzania wote!! Hawana haki ya kuwatenga baadhi ya watanzania!! Napoendekeza wajitokeze mawakili kufungua kesi mahakamani kupinga UBAGUZI huu!!
 
Ni kwel mkuu angalia report ya CAG taasisi zilizofanya ovyo ingia deep interior reasons unaibukia mulemule nenda tena kwanini hawachukuliwi hatua reasons iyo iyo, wapi tunaelekea jaman
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…