Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita watu kazini?

IT siku hzi mbili tatu anapumua pushing za vijana zimepoaa sanaa dah au ndo tamati ya psrs kimenukiaa?
 
Kweli Hajui mbona kuna kazi kibao za Mkataba zimepitia Utumishi example Cereals and other produce Board(CPB),Tanroads Lakini pia ukisoma kanuni za Utumishi pia wanaeza kukaimisha usajili wao wakatuma wakaguzi.
Hizo kazi za mikataba zinazopitia utumishi si kama zile zinazosemwa NSSF. Kazi za mikataba zinazopitia utumishi mara nyingi ni kazi za kada ya juu na zile za muda mfupi kama miezi 3-6. Huko NSSF ni hizo mikataba mifupi mifupi na huwa wana-renew mara kwa mara!!
 
Zilikua ni mkataba wa Mwaka mmoja, Ila mara nyingi ukifanikiwa kupenya ni renewable mara nyingi.
 
Duu hongera nyingi kwake
 
Hatimaye Nimelamba Asali ndugu zangu nawashukuru team ya hapa ndani kwa namna tulivyopeana moyo na kufarijiana na mimi niwape moyo kuwa it is just a matter of time. Nimekaa mtaani tangu 2014 mpaka sasa.

Mapambano yaendelee

Hongera sana ndugu,

Hakika Mungu ni mwema sana, daima wakati wa Mungu ndio wakati sahihi kabisa. Nakutakia majukumu mema katika kazi yako, pia zingatia kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu katika utendaji wako.

Mwisho, jipongeze kwa mafanikio hayo uliyopata pamoja na ndugu na jamaa zako na pia kumbuka kutoa shukrani kwa jamii kwani haikuwa rahisi mpaka kufika hapo.
 
Nitakusaidia kufungua uzi juu ya hili kwa sababu haikubaliki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…